JW subtitle extractor

Je, Ni Kazi ya Ubuni? Rangi za Ndege Zisizofifia

Video Other languages Share text Share link Show times

Rangi ya vitu
vingi vinavyotengenezwa
na wanadamu hufifia
kama ya nyumba
au ya nguo.
Lakini sivyo ilivyo kuhusu
rangi za ndege wengi.
Manyoya yao
hudumisha mng’ao wake
na ni yenye kuvutia.
Hilo linawezekanaje?
Watafiti walichunguza
manyoya ya ndege
anayeitwa Eurasian jay
wakagundua kwamba
rangi yake haitokani na
rangi za asili,
bali inatokana na
muundo wa manyoya yake.
Mwanga wa jua unaoakiswa
hugawanyika na
kutokeza rangi tunazoona
ikitegemea muundo
wa manyoya yake.
Na kwa kuwa muundo wa
manyoya haubadiliki
kadiri ndege anavyozeeka,
rangi zake hazififii kamwe.
Ugunduzi huo utawasaidia
wanasayansi kupata
mawazo mapya ya kubuni.
Dakt. Andrew Parnell anasema:
“Ikiwa rangi ya manyoya ya ndege
imetokezwa kiasili,
basi sisi tutaweza
kuitokeza kiwandani.”
Sasa, watafiti wanajaribu
kutengeneza vitu kwa kuiga
muundo huo.
Huenda wakatengeneza rangi
ambazo hazitawahi kufifia,
au labda hata
nguo ambazo hazipauki licha ya
kuoshwa mara nyingi.
Una maoni gani?
Je, rangi za manyoya ya ndege
zisizoweza kufifia
zilijitokeza zenyewe?
Au je, ni kazi ya ubuni?