JW subtitle extractor

Je, Ni Kazi ya Ubuni? Chungu Wanaepukaje Msongamano Barabarani?

Video Other languages Share text Share link Show times

Kila siku,
mamilioni ya chungu
hutoka kwenye makao yao
na kwenda kuwinda
bila msongamano wowote.
Jinsi gani?
Siafu wanapotoka nyumbani,
silika huwaongoza kuzunguka
ili wasikutane
na wale wanaoleta chakula
kwa sababu hawawezi
kutembea vizuri.
Chungu wafyeka majani
wanapokutana na
chungu wanaotembea polepole
kwa kuwa wamebeba mizigo,
wanapunguza mwendo,
wanafanyiza kikundi,
na hivyo kutembea pamoja.
Watafiti wanasema
hilo huwasaidia chungu hao
kufika upesi zaidi nyumbani
kwa kuwa wanaruhusiwa
kupita kwanza
ili wasigongwe na
chungu wenzao
wanaotoka nyumbani.
Kwa kuongezea,
chungu wanaweza kuwasiliana
kwa kugusishana vipapasio,
na hivyo kushughulikia
hali yoyote inayoweza
kutokeza msongamano.
Tofauti na wadudu hao,
wanadamu hupoteza
mabilioni ya saa kila mwaka
kutokana na
msongamano wa magari.
Wanasayansi wanataka kuiga
uwezo huo wa chungu
unaotegemea silika
kwa kuunda mfumo wa kuongoza
magari utakaoyasaidia kuendelea
kusonga hata hali
barabarani zinapobadilika.
Una maoni gani?
Je, uwezo wa chungu wa kuepuka
msongamano ulijitokeza wenyewe?
Au je, ni kazi ya ubuni?