JW subtitle extractor

Kwa Nini Uwe Mnyoofu?

Video Other languages Share text Share link Show times

Kila mtu angependa kuwa mshindi.
Lakini je,unaweza kuwa mshindi
ikiwa kila wakati wewe ni mnyoofu?
Hakuna mtu anayempenda mwongo.
Lakini wakati fulani
inaweza kuonekana kwamba
watu wasio wanyoofu wanafanikiwa.
Basi kwa nini wewe peke yako uwe mnyoofu?
na hasa ikiwa hakuna mtu yeyote anayeumia.
Tatizo ni kwamba
uongo una madhara mengi
kuliko faida.
Na ukishaanza kutueleza kwenye njia
hiyo ya kudanganya,
ni vigumu sana kuaacha.
Na ikiwa utafanikiwa kwa sababu ya uongo wako
inaelekea utadanganya tena.
Lakini huenda ukijiambia si vibaya
kusema ukweli nusu nusu
lakini bado huo ni uongo
ikiwa utawapotosha wale wanaostahili
kujua ukweli kamili.
Kuna ubaya gani kutia chumvi kidogo?
Hasa ikiwa unataka kupata marafiki
Unapojifanya uonekane tofauti na ulivyo kikweli
hiyo pia ni aina ya uwongo.
Kadiri unavyoendelea kufanya hivyo,
huenda usione kuwa una tatizo
mpaka utakapogundua kwamba
umekuwa mtu tofauti kabisa.
Huwezi kuwa na amani ya akili ukidanganya
ni vigumu zaidi kukumbuka uongo uliosema
kuliko ukweli.
Na punde si punde matokeo ya kusema
uongo yataka kulipukia.
Kwenye Methali ishirini na moja sita
Biblia inasema kwamba
faida zozote tunazopata kwa kusema uongo
ni kama ukungu unatoweka.
Huenda familia yako ikaacha kukuheshimu
na kukuamini
huenda pia ukapoteza marafiki wako
na ikiwa utazoea kudanganya maishani mwako,
Eh huenda utapata madhara makubwa hata zaidi.
mbali na hayo yote
kusema uongo
kuna madhara yaliojificha
kunabadili jinsi unavyohisi kujihusu
lakini unaweza kuchagua kuwa mnyoofu
na uone jinsi utakavyonufaika.
ukishawishiwa kujinufaisha kutokana udanganyifu
kataa mmm utajiheshimu
kwa sababu matokeo uliopata,
yalitegemea jitihada ulizofanya.
Acha watu wa familia wakuheshimu na kukuamini
kwa kuwaeleza ukweli kamili.
Huenda ukapata adhabu
lakini utajifunza kutokana na makosa yako.
Na utapata marafiki wanaokupenda
kwa jinsi ulivyo
Kuna faida kubwa zaidi kuwa mnyofu
kuliko kuwa mwongo
Katika familia pamoja na marafiki
na kwako mwenyewe