JW subtitle extractor

Je, Ni Kazi ya Ubuni? Sanaa ya Wanyama

Video Other languages Share text Share link Show times

Sanaa hutuvutia.
Iwe ni yenye
kutokeza sana
au la,
bado sanaa
hugusa moyo wetu.
Na wakati mwingine
tunaipata mahali ambapo
hata hatukutarajia.
Kwa mfano,
konokono wa baharini
wana rangi zinazong’aa
nazo hufanya
maadui wasi wasiwasogelee.
Lakini sisi tunapowaona
tunaona rangi maridadi
zilizopangwa vizuri.
Kinyonga
hubadilika-badilika rangi
ili kutoa onyo,
na wakati mwingine
hata anapotafuta mwenzi.
Baadhi ya wanyama
wanatofautiana sana
lakini wana sanaa ileile
kama buibui huyu
ambaye anafanana
na tausi.
Mchoro
haubadiliki
lakini wanyama
wanaweza kufanya
rangi zao
zikatokeza zaidi
au hata kubadili
mwonekano wao
kwa njia fulani
ndani ya muda mfupi.
Mmoja kati ya mabingwa
ni ndege huyu maridadi.
Ndege huyu
anayeitwa kibisi
anafanya maonyesho ya
sanaa ya kipekee
pamoja na mwenzi wake.
Njia yao ya kucheza
ina upatano usioelezeka.
Kwa kweli,
hii ni dansi juu ya maji.
Ndege huyu wa kiume
ana usanii wa aina yake
anapanga vijiti
na mbegu mbegu
kwa njia ambayo
inavutia macho yetu.
Kuna mnyama
mmoja mdogo
lakini mbunifu sana.
Kazi yake ya sanaa
ni kubwa
na inavutia.
Bunju mwenye
madoa meupe
ni samaki anayetengeneza
maumbo maridadi
kwenye sakafu ya bahari.
Samaki wa kiume
anayefanya kazi hiyo
anatazamia kwamba
jike akiona tu sanaa yake
atamkubali.
Una maoni gani?
Je, sanaa ya wanyama
ilijitokeza yenyewe?
Au je, ni kazi ya ubuni?