JW subtitle extractor

Ripoti ya 9 ya Baraza Linaloongoza

Video Other languages Share text Share link Show times

Ni furaha kubwa kwangu
kuzungumza kwa dakika kadhaa
pamoja nanyi
watumishi wapendwa wa Yehova.
Kama mjuavyo,
tumekuwa tukikabiliana na madhara
ya ugonjwa huu wa corona
kwa muda mrefu sana.
Je, umechoka kuvaa barakoa?
Au, umechoka kukaa mbali na wengine?
Bila shaka, ungependa kukutana tena
na ndugu na dada zako.
Kwa kuwa hali hii
imeendelea kwa muda mrefu,
huenda ukashawishika
kupunguza umakini
na kuacha kuchukua tahadhari
ambazo tumekuwa tukizingatia,
lakini kama mjuavyo,
idadi ya watu walioambukizwa
imeongezeka sana
katika nchi moja baada ya nyingine
Kwa kweli, idadi ya maambukizi
na vifo ulimwenguni pote
imeongezeka
kuliko wakati mwingine wowote
wa janga hili la COVID-19.
Huu si wakati unaofaa
wa kuacha kuchukua tahadhari.
Methali 28:14 inasema hivi:
“Mwenye furaha ni mtu aliye
chonjo sikuzote,
lakini yeyote anayeufanya moyo wake
kuwa mgumu
ataanguka katika msiba.”
Ikiwa ‘sikuzote tuko chonjo’ kama mlinzi
hilo litatusaidia kuepuka msiba.
Katika ripoti hii
tungependa kuzungumzia
kwa nini tuendelee kujilinda
na jinsi ya kufanya hivyo.
Pia, tutasikiliza masimulizi
yanayoonyesha manufaa
ya kuendelea kuwa chonjo.
Kwanza, acheni tuzungumzie
kwa nini tunahitaji kuendelea kujilinda
na kuwalinda wengine.
Kadiri ambavyo miezi imepita,
ikiwa sisi
au watu wa familia yetu hawajapatwa na
ugonjwa wa COVID-19,
huenda ikawa rahisi kufikiri,
‘Mimi na familia yangu hatutaambukizwa.’
Hata hivyo, Biblia inatuonya
tusijiamini kupita kiasi.
1 Wakorintho 10:12 inasema:
“Basi yule anayefikiri amesimama
na ajihadhari asije akaanguka.”
Kupatana na kanuni hiyo,
badala ya kujiamini kupita kiasi
na kuepuka kuchukua tahadhari
tukifikiri ‘siwezi kuambukizwa,’
tunasababu nzuri ya “kujihadhari”
na kuendelea kuwa chonjo.
Kwa kusikitisha,
kufikia Desemba 20,
zaidi ya ndugu na dada 7,500
ulimwenguni pote
wamekufa kutokana
na ugonjwa huu wa corona.
Tunawapa pole nyinyi nyote
ambao mmepoteza
watu wa karibu wa familia
na marafiki.
Na kwa kusikitisha
madhara ya janga hili la
ugonjwa wa corona
hayajakwisha bado.
Ofisi fulani za tawi zinaripoti
kwamba idadi ya ndugu walioambukizwa
katika mwezi uliopita
imeongezeka mara mbili au tatu
kuliko idadi ya
walioambukizwa mwaka mzima!
Kwa hiyo, tuendelee kuchukua tahadhari.
Katika video ifuatayo,
msikilize Ndugu Peter Canning
kutoka kwenye ofisi ya tawi ya Kroatia
anavyoeleza jinsi kuchukua tahadhari
kumewasaidia akina ndugu
kuendelea kuwa salama
kadiri wawezavyo.
Mwanzoni mwa mwezi wa Juni,
hali nchini Kroatia ilianza kuonekana
kuwa inarudi kuwa kawaida.
Siku fulani hata zingepita
bila hata kuwa na ripoti
za maambukizi mapya nchini kote.
Kwa hiyo, biashara na mikahawa
ilifunguliwa upya
na watalii walianza kumiminika tena
nchini Kroatia.
Baadhi ya akina ndugu walijiuliza
iwapo tunaweza kuanza utendaji fulani
labda mahubiri ya hadharani.
Lakini Baraza Linaloongoza
likatoa mwongozo
kwamba ofisi zote za tawi
zisirudie mahubiri ya hadharani
mpaka taarifa itakapotolewa.
Mwanzoni haikuwa rahisi kuelewa
umuhimu wa kuchukua
tahadhari kubwa hivyo,
hasa kwa sababu hali ilionekana ni
salama kufanya mahubiri ya hadharani.
Lakini huo ulikuwa ni uamuzi
wenye hekima sana.
Baada ya majuma machache,
idadi ya maambukizi
ilianza kuongezeka
na sasa maelfu ya watu
wanaambukizwa kila siku.
Mambo tuliyojionea yametufanya
tuazimie hata zaidi
kukazia uangalifu mwongozo
tunaopata kutoka kwa tengenezo
na kuwa tayari kuufuata.
Ni muhimu kuendelea kuwa chonjo.
Kama Ndugu Canning alivyosema,
lazima tuendelee kuwa chonjo.
Ni nini kitatusaidia kuendelea kuwa salama?
Mwezi wa Juni,
katika Ripoti ya 4 ya Baraza Linaloongoza,
Ndugu Morris alitaja kanuni tatu
muhimu sana
ambazo zingetuongoza.
Ulikuwa ushauri mzuri wakati huo.
Na sasa kwa kuwa maambukizi
yanazidi kuongezeka,
ni ushauri unaotufaa sasa.
Acha tupitie tena kanuni hizo.
Kanuni ya kwanza:
Heshimu sana uhai.
Ingawa huenda tahadhari unazochukua
zikakuzuia kufanya mambo fulani,
kumbuka
zinalinda uhai wako
na wa familia yako pia.
Kanuni ya pili:
Sikiliza mamlaka.
Tunapofuata miongozo yao ya usalama,
tunaonyesha tunaheshimu
mpango wa Yehova.
Na tunaonyesha kwamba
tunawajali sana
jirani zetu.
Jambo ya tatu:
Epuka mtazamo wa kutojali.
Kwa muda wote ambao
ugonjwa huu utaendelea.
Tafadhali usiache kuwa makini
hizo ni kanuni tatu muhimu sana.
Sasa, nitaomba ujiulize swali hili:
‘Je, maamuzi yangu yanaonyesha kwamba
ninaheshimu sana uhai,
ninasikiliza mamlaka
na nimeepuka kusitawisha
mtazamo wa kutojali?’
Unapofanya uamuzi wowote ule,
fikiria hili:
Maamuzi unayofanya
hayakuathiri wewe tu,
bali pia familia yako yote,
ndugu na dada zako,
na jamii kwa ujumla.
Ni jambo zito unapolifikiria hivyo, sivyo?
Unapofikiria jinsi wewe na familia yako
mtakavyojiendesha katika miezi ijayo,
tunawasihi
mwendelee kufuata
miongozo ifuatayo ya usalama
ya msingi.
Kumbuka jinsi ugonjwa
wa corona unavyoambukizwa
na unapaswa kufanya mambo gani
ili kujilinda mwenyewe.
Zingatia mambo haya machache,
wataalamu wa afya
wanakubaliana kwamba
njia kuu ambao
ugonjwa huu unaambukizwa
ni kupitia hewa.
Kwa hiyo, wakati wowote
mtu aliyeambukizwa anapokohoa
kupiga chafya,
kuzungumza,
au hata kupumua
anaweza kueneza ugonjwa huo.
Hata ikiwa mtu
aliyeambukizwa ugonjwa wa corona
haonyeshi dalili zozote,
bado anaweza kuwaambukiza wengine
ugonjwa huo.
Kuna hatari kubwa zaidi
ikiwa tutakuwa karibu na wengine
au katika eneo lenye watu wengi
au ndani ya nyumba
Moja wapo ya njia bora zaidi ya
kuepuka kueneza ugonjwa wa corona
ni kuvaa barakoa
na kudumisha
umbali unaofaa kutoka kwa wengine.
Ili kujikumbusha tahadhari
unazoweza kuchukua ili kujilinda,
tumetayarisha video mpya ya
vibonzo kwenye ubao yenye kichwa
Unaweza Kufanya Nini Magonjwa
ya Mlipuko Yakitokea?
Video hiyo tayari inapatikana
kwenye tovuti ya jw.org
na itapatikana katika
lugha nyingine hivi karibuni.
Tafadhali tenga wakati uitazame.
Bila shaka utakubali kwamba
jitahada zinahitajika
ili kuchukua tahadhari.
Lakini kufanya hivyo kunatunufaishaje?
Je, unakumbuka tulichosoma mapema
kwenye Methali 28:14?
“Mwenye furaha ni mtu aliye
chonjo sikuzote.”
Katika video ya mahojiano ifuatayo,
ona jinsi Dada Louise Slender,
ambaye ni mjitoleaji
anayefanyia kazi akiwa nyumbani
katika ofisi ya tafsiri nchini Marekani
amenufaika kwa kuendelea kuwa chonjo.
Pia, utaona
madhara ambayo ugonjwa wa corona
umewasababishia watu wake wa ukoo
ambao si Mashahidi.
Ninaishi kwenye nchi ya Navajo,
Eneo linaloitwa Tuba City, Arizona.
Ugonjwa wa corona ulipoaanza,
nilijiambia,
tunaishi mbali sana
kwenye eneo la vijijini
huku Tuba City hatutaathiriwa.
Lakini familia yangu iliathiriwa sana.
Wakati wa awamu ya kwanza
nilipoteza watu 15 wa familia
kisha baada ya hapo
wengine walilazwa hospitali.
Na kufikia sasa,
nimepoteza watu 35 wa familia yangu
na wengine bado ni wagonjwa,
wamelazwa hospitali.
Na hilo limenifanya niwe na huzuni
kwa sababu ni jambo baya sana limetokea.
Sasa hapa kwangu tunaishi watatu.
Na yeyote aliye nje ya nyumba yetu
anaweza kuambukizwa.
Ni hali ngumu sana
kwa sababu kwa miaka mingi sana
tulizoea kuwa pamoja nao
halafu na sasa ghafla hili limetokea.
Kwa hiyo sasa ninajihadhari
kwa sababu mtu yeyote
anaweza kuwa ameambukizwa,
kwa hiyo mimi hudumisha umbali unaofaa.
Singependa kuambukizwa ugonjwa huo.
Ninahakikisha
ninajihadhari kwa sababu sisi.
Tunaposoma Neno la Yehova,
ninasoma kwamba sisi ni watu safi,
watu wa Yehova ni safi.
Kwa hiyo ni lazima tuendelee
kudumisha safi.
Tunavaa barakoa na kunawa mikono
na kupangusa
kila kitu kinachoingia nyumbani,
kutia ndani barua tunazopata.
Ugonjwa huu wa corona ni hatari sana
COVID-19 ni ugonjwa
ambao unaowachukua wapendwa wako
(watu unaowapenda),
inahuzunisha sana.
Umesababisha vifo vya watu wengi
wenye kupendeza,
kama vile watu wangu wa ukoo.
Walikuwa watu wenye akili sana;
walikuwa na ustadi katika sanaa;
walifanya kazi nyingine;
walikuwa na nyumba zao.
Na sasa tunaona
vifaa vyao vya kazi
na hakuna mtu wa
kushughulikia mashamba yao.
Walikuwa tu
wametayarisha mashamba yao
lakini hata hawakupanda mbegu.
Nyumba zao
na magari yao
yapo tu.
Kwa hiyo tahadhari zote zinazotolewa,
kwa kweli ni tahadhari
halisi sana
na ni muhimu sana
kwamba tuzifuate.
Tunasikitika sana pamoja na
Dada Slender na familia yake yote.
Je, simulizi lake
halionyeshi manufaa
za kuendelea kuwa chonjo?
Kufuata mwelekezo wa
kuchukua tahadhari
kumemlinda sana Dada Slender,
mume wake,
na mwana wake!
Kwa hiyo kufikia hapa,
tumezungumzia nini?
Huu si wakati
wa kuacha kuwa makini
na kuacha kuchukua tahadhari.
Usiache kuwa chonjo.
Usifikiri wewe na familia yako
hamwezi kuambukizwa.
Lakini hata baada ya kuchukua tahadhari
huenda baadhi yenu
mkaambukizwa ugonjwa huo.
Tunaendelea kusali kwa ajili yenu
na familia zenu.
Tunatamani siku ambapo
Yehova atatimiza ahadi yake kwamba
“hakuna [yeyote] atakayesema kwamba:
‘Mimi ni mgonjwa.’”
Tafadhali endeleeni kujilinda,
usikae mbali na kutaniko lako,
na zaidi ya yote,
kaa karibu na Yehova.
Kwa msaada wa Yehova,
tuna uhakika unaweza kukabiliana
na changamoto yoyote unayopata.
Ni pendeleo langu
kuwaletea nyinyi
salamu changamfu za
Baraza Linaloongoza.
Tunawapenda sana nyinyi nyote.
Kutoka kwenye Makao Makuu
ya Ulimwenguni Pote
ya Mashahidi wa Yehova.
Hii ni JW Broadcasting®.