JW subtitle extractor

“Uwe Jasiri na Imara na Uanze Kazi”!

Video Other languages Share text Share link Show times

‎Yehova anathamini sana ujasiri
wa waabudu wake washikamanifu.
‎Ujasiri wa kweli huonekana
kupitia matendo,
‎kama ilivyo na
sifa nyingine nzuri.
‎Kwa mfano, “imani bila
matendo imekufa.”
‎Vivyo hivyo, upendo unapaswa
kuonyeshwa, si kwa maneno tu,
‎bali kama Biblia inavyosema,
‎“kwa tendo na kweli.”
‎Ndivyo ilivyo
na ujasiri.
‎Tunahitaji kumtegemea Yehova
‎ili kukabiliana
na hali ngumu,
‎lakini matendo yetu yanapaswa
kuonyesha tunamtegemea.
‎Kutochukua hatua,
‎kutofanya uamuzi,
‎au kuwa goigoi
‎ni ishara za
kukosa ujasiri.
‎Ujasiri unapaswa kutuchochea
tuzungumze na kutenda bila woga.
‎Naye Yehova
‎atabariki ujasiri wetu
na kutusaidia tufanikiwe.
‎Hilo linaonekana vizuri
kupitia simulizi la Biblia kumhusu Daudi.
‎Ilipohusu kufanya
mapenzi ya Yehova,
‎Daudi alionyesha
ujasiri kwa matendo.
‎Hata alipojikwaa
na kuteseka sana,
‎Daudi aliendelea kuwa mshikamanifu
kwa Yehova maisha yake yote.
‎Muda mfupi
kabla ya kufa,
‎Daudi alimkabidhi rasmi
mwanawe Sulemani
‎kazi ya kujenga
hekalu la Yehova.
‎Wazia jinsi
Sulemani alivyohisi
‎Daudi alipomkabidhi
‎ramani za ujenzi zilizoongozwa
na Yehova Mungu mwenyewe!
‎Bila shaka, Sulemani alihisi
kwamba kazi hiyo ni ngumu.
‎Lakini Daudi baba
yake alimwimarisha
‎kwa maneno yanayoweza
kutuimarisha leo
‎tunapokabili
hali ngumu.
‎Tunawakaribisha nyote,
kutia ndani watoto na vijana,
‎mfungue Biblia zenu
‎na tufuatane tunaposikiliza
simulizi lililo katika
‎1 Mambo ya Nyakati 28:1-20.
‎Nitawapa muda
wa kufungua.
‎ 1 Mambo ya Nyakati sura ya 28,
‎kuanzia mstari wa 1.
‎Kisha Daudi
akawakusanya Yerusalemu
‎wakuu wote wa Israeli:
‎ wakuu wa makabila,
‎viongozi wa vikundi
vilivyomhudumia mfalme,
‎wakuu wa maelfu
na wakuu wa mamia,
‎wasimamizi wa mali
zote za mfalme
‎na mifugo yake
na wa wanawe,
‎pamoja na maofisa wa
makao ya mfalme
‎na kila mwanamume
hodari mwenye uwezo.
‎Halafu Mfalme Daudi
akasimama na kusema:
‎Nisikilizeni,
‎ndugu zangu
na watu wangu.
‎Moyo wangu ulitamani
kujenga nyumba ambamo
‎sanduku la agano
la Yehova lingekaa
‎na ambayo ingekuwa kiti cha
miguu cha Mungu wetu,
‎nami nilifanya
matayarisho ya kuijenga.
‎Lakini Mungu wa
kweli akaniambia,
‎‘Hutajenga nyumba
kwa ajili ya jina langu,
‎kwa maana wewe
ni mtu wa vita,
‎nawe umemwaga damu.’
‎Hata hivyo, Yehova
Mungu wa Israeli
‎alinichagua kutoka katika
nyumba yote ya baba yangu
‎niwe mfalme wa
Israeli milele,
‎kwa maana alimchagua
Yuda kuwa kiongozi
‎na kutoka katika
nyumba ya Yuda
‎aliichagua nyumba
ya baba yangu,
‎na kati ya wana
wa baba yangu
‎ alinikubali mimi
‎niwe mfalme wa
Israeli yote.
‎Na kutoka kati ya
wanangu wote—
‎kwa maana Yehova
amenipa wana wengi—
‎alimchagua Sulemani
mwanangu
‎aketi kwenye kiti
cha ufalme wa Yehova
‎juu ya Israeli.
‎Akaniambia,
‎“Sulemani mwana wako
‎ndiye atakayeijenga
nyumba yangu
‎na nyua zangu,
‎kwa maana nimemchagua
yeye kuwa mwanangu,
‎nami nitakuwa
baba yake.
‎Nitauimarisha kabisa
ufalme wake milele
‎ikiwa atazishika kwa
dhati amri zangu
‎na sheria zangu,
‎ kama anavyofanya sasa.”
‎Basi, nasema machoni pa
Waisraeli wote,
‎kutaniko la Yehova,
‎na masikioni mwa
Mungu wetu:
‎ Shikeni kwa uangalifu
‎na mtafute amri zote
za Yehova Mungu wenu,
‎ili mwimiliki
nchi nzuri
‎na kuwaachia wana wenu kuwa
urithi wa kudumu baada yenu.
‎“Nawe, Sulemani mwanangu,
‎ mjue Mungu wa baba yako
‎na kumtumikia
kwa moyo kamili
‎na kwa nafsi
yenye shangwe;
‎kwa maana Yehova
‎huichunguza kabisa
mioyo yote,
‎naye hutambua
kila mwelekeo wa fikira.
‎Ukimtafuta,
‎atakuruhusu umpate,
‎lakini ukimwacha,
‎atakukataa milele.
‎Ona kwamba Yehova
amekuchagua
‎wewe ujenge nyumba
‎ili iwe mahali
patakatifu.
‎Uwe jasiri, anza kazi.
‎Kisha Daudi akampa
Sulemani mwana wake
‎ramani ya ujenzi wa ukumbi
na ya nyumba zake,
‎maghala yake,
‎vyumba vyake vya darini,
‎vyumba vyake vya ndani,
‎na nyumba ya
kifuniko cha upatanisho.
‎Alimpa ramani ya kila kitu alichoambiwa
kupitia mwongozo wa roho
‎kuhusu ujenzi wa nyua za
nyumba ya Yehova,
‎vyumba vyote vya
kulia chakula vilivyoizunguka,
‎hazina za nyumba
ya Mungu wa kweli,
‎na hazina za vitu vilivyofanywa
kuwa vitakatifu;
‎pia kuhusu vikundi vya
makuhani na Walawi,
‎kuhusu kazi zote za utumishi
wa nyumba ya Yehova,
‎na kuhusu vyombo vyote vya
utumishi wa nyumba ya Yehova;
‎pia kuhusu uzito
wa dhahabu,
‎dhahabu ya vyombo vyote
vya utumishi mbalimbali,
‎uzito wa vyombo
vyote vya fedha,
‎na vyombo vyote vya
utumishi mbalimbali;
‎pia uzito wa vinara
vya taa vya dhahabu
‎na taa zake za dhahabu,
‎uzito wa vinara mbalimbali
‎vya taa na taa zake,
‎na uzito wa vinara
vya taa vya fedha,
‎uzito wa kila kinara
cha taa na taa zake
‎kulingana na
matumizi yake;
‎pia kuhusu uzito
wa dhahabu za
‎meza za mikate
ya tabaka,
‎ uzito wa kila meza,
‎na pia fedha kwa ajili ya
meza za fedha,
‎kuhusu nyuma,
‎mabakuli,
‎magudulia ya
dhahabu safi,
‎na uzito wa mabakuli
madogo ya dhahabu,
‎uzito wa kila
bakuli dogo,
‎na uzito wa mabakuli
madogo ya fedha,
‎uzito wa kila
bakuli dogo.
‎Pia alimpa uzito
wa dhahabu safi
‎kwa ajili ya madhabahu
ya uvumba
‎na kwa ajili ya mfano
wa lile gari,
‎yaani, wale makerubi wa dhahabu
walionyoosha mabawa yao
‎na kulifunika sanduku
la agano la Yehova.
‎Daudi akasema:
‎Mkono wa Yehova
ulikuwa juu yangu,
‎naye alinipa ufahamu
wa kuandika mambo yote
‎kuhusu ramani
hii ya ujenzi.
‎Kisha Daudi akamwambia
Sulemani mwanawe:
‎Uwe jasiri na imara
na uanze kazi.
‎Usiogope wala usihofu,
‎kwa maana
Yehova Mungu,
‎Mungu wangu,
‎ yuko pamoja nawe.
‎Hatakuacha wala kukutupa,
‎lakini atakuwa
pamoja nawe
‎mpaka kazi yote ya utumishi wa
nyumba ya Yehova itakapokamilika.
‎Wazia kazi ya Sulemani!
‎Hakuagizwa tu kujenga nyumba
ya pekee kwa ajili ya ibada ya kweli
‎bali hekalu hilo lilipaswa kuwa
“na utukufu usio na kifani,”
‎umaarufu na umaridadi wake
ungejulikana “katika nchi zote.” ’
‎Ingawa hivyo,
‎Sulemani hakuwa na
uzoefu wa kujenga.
‎Daudi alifikiria hali ngumu
ambazo angekabili.
‎Isitoshe, Sulemani
angekabili upinzani
‎ndani na nje ya familia yake.
‎Kwa hiyo, Daudi alimhimiza
mwanawe awe mtiifu
‎na mshikamanifu
kwa Yehova.
‎Pia alimhimiza Sulemani
‎‘awe jasiri na imara
na aanze kazi.’
‎Sulemani angelemewa
na woga.
‎Akifikiria kwamba mgawo wake
ulikuwa mgumu sana,
‎huenda angeahirisha au
hata kuacha kazi hiyo.
‎Hilo lingemkasirisha
sana Yehova.
‎Basi, Daudi alirudia ushauri
huu: “Anza kazi.”
‎Daudi alielewa kwamba ujasiri
na kumtegemea Yehova
‎kunapaswa kuambatana
na matendo.
‎Alijua hivyo kutokana na
mambo aliyojionea.
‎Acheni tuchunguze baadhi ya
matukio katika maisha ya Daudi
‎yaliyohitaji ujasiri.
‎Tunaposoma masimulizi
haya, jiulize,
‎‘Je, Daudi aliahirisha
mambo,
‎alisitasita,
‎au kuogopa alipokabili
hali ngumu?’
‎Kwa mfano, fikiria
hali zilizokuwepo
‎Daudi alipotiwa mafuta
kuwa mfalme wa Israeli.
‎Bado Mfalme Sauli
alikuwa akitawala,
‎lakini Yehova
alikuwa amemkataa
‎Sauli kwa sababu ya kutotii.
‎Fuatana katika Biblia yako
tunaposikiliza maneno ya
‎1 Samweli 16:1-23. 1 Samweli 16:1-23.
‎Mwishowe Yehova
akamuuliza Samweli:
‎Kwa kuwa nimemkataa Sauli
asitawale akiwa mfalme wa Israeli,
‎utaendelea kumwombolezea
mpaka lini?
‎Jaza pembe
yako mafuta,
‎uende.
‎Nitakutuma kwa
Yese Mbethlehemu,
‎kwa sababu
nimejichagulia mfalme
‎kutoka miongoni
mwa wanawe.
‎Lakini Samweli
akasema:
‎Nitaendaje?
‎Sauli akisikia
habari hii,
‎ataniua.
‎Yehova akamwambia:
‎Nenda na ng’ombe
mchanga, useme,
‎“Nimekuja kumtolea
Yehova dhabihu.”
‎Mwalike Yese
kwenye dhabihu;
‎kisha nitakujulisha
utakalofanya.
‎Utamtia mafuta kwa ajili yangu
yule nitakayekuonyesha.
‎Samweli alifanya mambo
aliyoambiwa na Yehova.
‎Alipofika Bethlehemu,
‎wazee wa jiji walitetemeka
walipokutana naye,
‎wakamuuliza:
‎Je, umekuja
kwa amani?
‎Akajibu:
‎Nimekuja kwa amani.
‎Nimekuja kumtolea
Yehova dhabihu.
‎Jitakaseni, mje pamoja
nami kwenye dhabihu.
‎Kisha akamtakasa
Yese na wanawe,
‎halafu akawaalika
kwenye dhabihu.
‎Walipokuwa wakiingia,
‎Samweli alimwona Eliabu
na kusema:
‎Hakika mtiwa-mafuta wa Yehova
amesimama hapa mbele zake.
‎Lakini Yehova
akamwambia Samweli:
‎Usitazame sura yake
wala urefu wake,
‎kwa maana
nimemkataa.
‎Kwa kuwa Mungu haoni kama
mwanadamu anavyoona,
‎kwa maana mwanadamu huona
kinachoonekana kwa macho,
‎lakini Yehova huona
ndani ya moyo.
‎Kisha Yese akamwita
Abinadabu,
‎akampitisha mbele
ya Samweli,
‎lakini Samweli akasema:
‎Huyu pia Yehova
hajamchagua.
‎Kisha Yese akampitisha
Shamma,
‎lakini Samweli akasema:
‎Hata huyu
Yehova hajamchagua.
‎Basi Yese akawapitisha wanawe
saba mbele ya Samweli,
‎lakini Samweli
akamwambia Yese:
‎Yehova hajamchagua
yeyote kati ya hawa.
‎Mwishowe Samweli
akamuuliza Yese:
‎Je, hawa ndio
wana wako wote?
‎Akajibu:
‎Aliye mdogo zaidi
ameachwa mpaka sasa;
‎anawalisha kondoo.
‎Kisha Samweli
akamwambia Yese:
‎Mtume mtu akamwite,
‎kwa sababu hatutaketi
kula chakula
‎ mpaka atakapokuja hapa.
‎Basi akamtuma
mtu amwite,
‎ Yese akamleta ndani.
‎Kijana huyo
alikuwa mwekundu,
‎ mwenye macho yanayovutia,
‎ na mwenye sura nzuri.
‎Ndipo Yehova akasema:
‎Simama,
‎mtie mafuta,
‎kwa maana
huyu ndiye!
‎Basi Samweli akachukua
ile pembe ya mafuta
‎na kumtia mafuta
mbele ya ndugu zake.
‎Na roho ya Yehova ikaanza
kumtia nguvu Daudi
‎kuanzia siku hiyo
na kuendelea.
‎Baadaye
Samweli akainuka
‎na kwenda zake Rama.
‎Sasa roho ya Yehova
ilikuwa imemwacha Sauli,
‎na roho mbaya kutoka kwa
Yehova ilikuwa ikimtesa.
‎Watumishi wa Sauli
wakamwambia:
‎Unaona kwamba roho mbaya
kutoka kwa Mungu inakutesa.
‎Tafadhali, bwana wetu,
‎waamuru watumishi wako
walio mbele yako
‎wamtafute mtu mwenye
ustadi wa kupiga kinubi.
‎Wakati wowote roho mbaya
kutoka kwa Mungu inapokujia,
‎atapiga kinubi,
nawe utahisi vizuri.
‎Basi Sauli akawaambia
watumishi wake:
‎Tafadhali, nitafutieni mtu
anayepiga kinubi vizuri,
‎ mumlete kwangu.
‎Mtumishi mmoja akasema:
‎Tazama!
‎Nimeona mwana fulani
wa Yese Mbethlehemu
‎anavyopiga kinubi kwa ustadi,
‎ni mtu jasiri na shujaa hodari.
‎Ana ustadi wa kuongea,
‎ana sura nzuri,
‎na Yehova yuko
pamoja naye.
‎Ndipo Sauli akawatuma wajumbe
kwa Yese na kumwambia:
‎Mtume mwana wako
Daudi aje kwangu,
‎yule anayechunga kondoo.
‎Basi Yese akapakia mikate,
‎kiriba cha ngozi
chenye divai,
‎na mwanambuzi
juu ya punda,
‎akamtuma Daudi mwana wake
kwa Sauli akiwa na vitu hivyo.
‎Kwa hiyo Daudi akafika kwa
Sauli na kuanza kumtumikia.
‎Sauli akampenda sana,
‎naye Daudi akawa
akimbebea silaha zake.
‎Sauli akamtumia
Yese ujumbe huu:
‎Tafadhali, mruhusu Daudi
aendelee kunitumikia,
‎kwa sababu amepata
kibali machoni pangu.
‎Wakati wowote roho mbaya
kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli,
‎Daudi alichukua
kinubi na kukipiga,
‎kisha Sauli alipata
kitulizo na kuhisi vizuri,
‎na roho hiyo
mbaya ilimwacha.
‎Je, unaweza
kuwazia kijana Daudi,
‎baba yake, na ndugu
zake wakiwa wamesimama
‎ mbele ya nabii Samweli?
‎Kisha Yehova akamchagua
Daudi awe mfalme
‎ na kumwagiza Samweli
‎amtie mafuta mvulana huyo.
‎Hata hivyo, Sauli
aliendelea kutawala,
‎akijulikana na wengi kuwa
mfalme halali wa Israeli.
‎Kwa kweli Daudi alihitaji
ujasiri wakati huo.
‎Sauli angetendaje baada
ya kujua kwamba
‎Daudi ametiwa
mafuta awe mfalme?
‎Bila shaka, Sauli angetafuta
njia ya kumuua.
‎Basi wazia jinsi
Daudi alivyohisi
‎alipoagizwa aende kwenye
nyumba ya Sauli ili kumhudumia!
‎Kwa kweli,
alikuwa na wasiwasi.
‎Namna gani sisi leo?
‎Huenda tukawa na wasiwasi
kwa sababu ya matatizo ya familia,
‎ugonjwa,
‎matatizo ya kifedha,
‎mateso,
‎au mwelekeo wetu
wenye dhambi.
‎Lakini hatupaswi kuruhusu
matatizo hayo yatulemee kiroho.
‎Tunapokabili matatizo hayo
‎tunapaswa kutafuta msaada
wa Yehova kupitia sala,
‎Neno lake, na kutaniko.
‎Mara nyingi,
tunaweza kupata njia
‎za kupunguza
matatizo hayo.
‎Hata matatizo yasipokwisha,
‎tunapaswa kufanya mapenzi
ya Yehova kwa bidii
‎kulingana na uwezo wetu,
‎hata tunapokabili matatizo.
‎Huo ni ujasiri wa kweli!
‎Daudi alipoitwa na Sauli,
‎hakulemewa na woga.
‎Alikuwa imara na jasiri,
‎na akaanza kazi!
‎Alikubali mgawo huo,
‎akijua kwamba Yehova
angempatia hekima
‎ili kutimiza mgawo wake.
‎Baadaye, Mfalme Sauli
alimpenda sana Daudi,
‎na Daudi akawa mtumishi
aliyembebea Sauli silaha.
‎Tafadhali tuambatane na
usomaji wa 1 Samweli 17:1-51.
‎Ni sura inayofuata—
‎1 Samweli sura ya 17,
kuanzia mstari wa 1.
‎Hii ni hadithi yenye kusisimua
ya Daudi na Goliathi.
‎Simulizi hilo linaonyesha jinsi
Daudi alivyotenda kwa hekima
‎ na kuonyesha ujasiri.
‎Sasa Wafilisti wakakusanya
majeshi yao kwa ajili ya vita.
‎Walikusanyika huko Soko,
‎jiji la Yuda, wakapiga kambi
kati ya Soko na Azeka,
‎kule Efes-damimu.
‎Sauli na wanaume wa
Israeli wakakusanyika
‎na kupiga kambi
katika Bonde la Ela,
‎nao wakajipanga kivita
ili kupigana na Wafilisti.
‎Wafilisti walikuwa upande
mmoja wa mlima,
‎na Waisraeli walikuwa
upande ule mwingine,
‎na bonde lilikuwa
katikati yao.
‎Kisha shujaa mmoja akatoka
katika kambi za Wafilisti;
‎ aliitwa Goliathi,
‎kutoka Gathi,
‎alikuwa na urefu wa mikono
sita na shubiri moja.
‎Alikuwa na kofia ya
shaba kichwani,
‎naye alivaa koti la vita lenye
magamba yanayolaliana.
‎Koti hilo la vita la shaba
lilikuwa na uzito wa
‎shekeli 5,000.
‎Alikuwa na mabamba ya shaba
yaliyokinga miguu yake
‎na fumo la shaba lililoning’inia
katikati ya mabega yake.
‎Mpini wa mbao wa
mkuki wake
‎ulikuwa kama mti wa
wafumaji wa nguo,
‎na kichwa cha chuma
cha mkuki wake
‎kilikuwa na uzito
wa shekeli 600;
‎na mtu aliyembebea ngao
alitembea mbele yake.
‎Basi akasimama na kuviita
vikosi vya Israeli akisema:
‎Kwa nini mmekuja
kujipanga kivita?
‎Je, mimi si Mfilisti nanyi je,
si watumishi wa Sauli?
‎Jichagulieni mwanamume,
‎aje kupigana nami.
‎Akiweza kupigana
nami na kuniua,
‎tutakuwa watumishi wenu.
‎Lakini nikimshinda
na kumuua,
‎ mtakuwa watumishi wetu,
‎nanyi mtatutumikia.
‎Kisha Mfilisti
huyo akasema:
‎Ninavitukana vikosi
vya Israeli leo.
‎Nipeni mwanamume,
nipigane naye!
‎Sauli na Waisraeli wote
‎waliposikia maneno
hayo ya Mfilisti huyo,
‎wakashikwa na hofu
na kuogopa sana.
‎Basi Daudi alikuwa
mwana wa Yese,
‎Mwefrathi kutoka mji wa
Bethlehemu wa Yuda,
‎ambaye alikuwa
na wana wanane
‎na ambaye katika siku za
Sauli alikuwa tayari amezeeka.
‎Wana watatu wakubwa
wa Yese walikuwa
‎wameenda na Sauli vitani.
‎Majina ya wana hao
watatu walioenda vitani ni
‎Eliabu mzaliwa
wake wa kwanza,
‎Abinadabu mwana
wake wa pili,
‎na Shamma mwana
wake wa tatu.
‎Daudi ndiye aliyekuwa
mdogo zaidi,
‎na wale watatu wakubwa
walikuwa wameenda pamoja na Sauli.
‎Daudi alikuwa akienda na
kurudi kutoka kwa Sauli
‎ili kuchunga kondoo wa
baba yake huko Bethlehemu.
‎Wakati huo, yule
Mfilisti alikuwa akija
‎na kuwadhihaki kila asubuhi
na kila jioni kwa siku 40.
‎Ndipo Yese akamwambia
Daudi mwana wake:
‎Tafadhali, chukua hii efa ya
nafaka iliyokaangwa
‎na mikate hii kumi,
‎uwapelekee haraka
ndugu zako kambini.
‎Nawe umpelekee
mkuu wa elfu
‎mafungu haya
kumi ya jibini;
‎pia, angalia ndugu
zako wanaendeleaje
‎na uniletee kitu
fulani kutoka kwao.
‎Walikuwa pamoja na Sauli na
wanaume wengine wote wa Israeli
‎katika Bonde la Ela,
‎wakipigana na Wafilisti.
‎Kwa hiyo Daudi akaamka
asubuhi na mapema
‎na kuwaacha kondoo
mikononi mwa mtu mwingine;
‎ kisha akapakia vitu hivyo
‎na kwenda kama Yese
alivyokuwa amemwamuru.
‎Alipofika kambini,
‎jeshi lilikuwa likienda
kwenye uwanja wa vita
‎huku likipiga kelele za vita.
‎Waisraeli na Wafilisti
wakajipanga kivita
‎wakikabiliana
uso kwa uso.
‎Mara moja Daudi
akaiacha mizigo yake
‎mikononi mwa mtu
aliyetunza mizigo,
‎akakimbia kwenda
kwenye uwanja wa vita.
‎Alipofika, akaanza kuulizia
habari za ndugu zake.
‎Alipokuwa akizungumza nao,
‎akaja yule Mfilisti shujaa
aliyeitwa Goliathi,
‎ kutoka Gathi.
‎Alitoka katika
vikosi vya Wafilisti,
‎akasema maneno yaleyale
aliyozoea kusema,
‎na Daudi akamsikia.
‎Wanaume wote wa Israeli
walipomwona mwanamume huyo,
‎wakaogopa sana
na kumkimbia.
‎Wanaume wa Israeli
walikuwa wakisema:
‎Je, mnamwona mwanamume
yule anayekuja?
‎Anakuja kuwatukana Waisraeli.
‎Mfalme atampa utajiri mwingi
mtu atakayemuua mwanamume huyo,
‎atampa pia binti
yake mwenyewe,
‎naye ataiondolea wajibu nyumba
ya baba yake katika Israeli.
‎Daudi akaanza kuwauliza
wanaume waliokuwa
‎wamesimama karibu naye:
‎Mtu atakayemuua
yule Mfilisti
‎na kuwaondolea Waisraeli
aibu atafanyiwa nini?
‎Kwani huyu Mfilisti
asiyetahiriwa ni nani
‎hata avitukane vikosi
vya Mungu aliye hai?
‎Basi watu hao
wakamwambia
‎maneno yaleyale
yaliyokuwa yamesemwa:
‎Hivi ndivyo atakavyofanyiwa
mwanamume atakayemuua.
‎Eliabu ndugu yake mkubwa
alipomsikia Daudi
‎akizungumza
na wanaume hao,
‎akamkasirikia Daudi
na kumwambia:
‎Kwa nini
umeshuka huku?
‎Na wale kondoo wachache
nyikani umemwachia nani?
‎Najua vizuri kimbelembele chako
na nia mbaya ya moyo wako;
‎umeshuka tu ili
kutazama vita.
‎Daudi akamwambia:
‎Sasa nimefanya nini?
‎Nilikuwa
nikiuliza swali tu!
‎Ndipo Daudi akamwacha,
‎akamgeukia mtu mwingine
na kumuuliza swali lilelile,
‎na watu wakamjibu
vilevile kama mwanzoni.
‎Watu wakasikia maneno
aliyosema Daudi,
‎wakamwambia Sauli.
‎Basi Sauli akaagiza aitwe.
‎Daudi akamwambia Sauli:
‎Mtu yeyote asife moyo
kwa sababu yake.
‎Mimi mtumishi wako nitaenda
kupigana na huyo Mfilisti.
‎Lakini Sauli
akamwambia Daudi:
‎Huwezi kwenda kupigana
na huyo Mfilisti,
‎kwa sababu wewe
ni mvulana tu,
‎naye amekuwa mwanajeshi
tangu alipokuwa kijana.
‎Ndipo Daudi
akamwambia Sauli:
‎Mimi mtumishi wako nimekuwa
nikichunga kondoo wa baba yangu,
‎na simba akaja,
na pia dubu,
‎na kila mmoja wao akamchukua
kondoo kutoka kundini.
‎Nilimfuata, nikamuua
‎na kumwokoa kondoo
kutoka kinywani mwake.
‎Aliporuka ili kunishambulia,
‎nilimkamata manyoya yake,
nikampiga, na kumuua.
‎Mimi mtumishi wako nilimuua
simba na dubu pia,
‎na huyu Mfilisti asiyetahiriwa
atakuwa kama mmoja wao,
‎kwa sababu amevitukana
vikosi vya Mungu aliye hai.
‎Kisha Daudi akasema:
‎Yehova, aliyeniokoa
‎kutoka katika makucha
ya simba na ya dubu,
‎ndiye atakayeniokoa kutoka
mikononi mwa Mfilisti huyo.
‎Ndipo Sauli
akamwambia Daudi:
‎Nenda, na Yehova
awe pamoja nawe.
‎Basi Sauli akamvisha
Daudi mavazi yake.
‎Akamvisha kofia
ya shaba kichwani,
‎halafu akamvisha
koti la vita.
‎Kisha Daudi akajifunga upanga
wake juu ya mavazi yake,
‎akajaribu kutembea
lakini akashindwa
‎kwa sababu
hakuwa ameyazoea.
‎Basi Daudi
akamwambia Sauli:
‎Siwezi kwenda nikiwa
nimevaa vitu hivi,
‎ kwa maana sijavizoea.
‎Kwa hiyo Daudi akavivua.
‎Kisha akachukua
fimbo yake mkononi,
‎akajichagulia mawe
matano laini
‎kutoka katika
bonde la kijito,
‎akayaweka kwenye kifuko
ndani ya mfuko wake wa mchungaji,
‎na kombeo lilikuwa
mkononi mwake.
‎Naye akaanza kumkaribia
huyo Mfilisti.
‎Mfilisti huyo akaanza kumkaribia
Daudi zaidi na zaidi,
‎na mtu aliyembebea ngao
alikuwa mbele yake.
‎Mfilisti huyo alipotazama
na kumwona Daudi,
‎akaanza kumdhihaki
kwa dharau
‎kwa sababu alikuwa tu mvulana
mwekundu mwenye sura nzuri.
‎Basi Mfilisti huyo
akamuuliza Daudi:
‎Je, mimi ni mbwa hivi
kwamba unijie na vijiti?
‎Ndipo huyo Mfilisti akamlaani
Daudi kwa miungu yake.
‎ Akamwambia Daudi:
‎Nikaribie tu,
‎nyama yako nitawapa
ndege wa angani
‎na wanyama
wa mwituni.
‎Daudi akamjibu
hivi huyo Mfilisti:
‎Unakuja kupigana nami kwa
upanga, mkuki, na fumo,
‎lakini mimi naja
kupigana nawe
‎kwa jina la Yehova
wa majeshi,
‎Mungu wa vikosi vya Israeli,
‎ambaye umemtukana.
‎Siku hii ya leo
‎Yehova atakutia wewe
mikononi mwangu,
‎nami nitakuua na
kukata kichwa chako;
‎na siku ya leo nitawapa
ndege wa angani
‎na wanyama
mwitu wa dunia
‎maiti za kambi ya Wafilisti;
‎na watu wote duniani
‎watajua kwamba kuna
Mungu katika Israeli.
‎Na watu wote
waliokusanyika hapa
‎ watajua kwamba Yehova
‎haokoi kwa upanga
wala kwa mkuki,
‎kwa sababu vita
ni vya Yehova,
‎naye atawatia ninyi nyote
mikononi mwetu.
‎Basi Mfilisti huyo
akasimama,
‎akazidi kukaribia ili
akutane na Daudi,
‎lakini Daudi
akakimbia haraka
‎kuelekea kwenye uwanja wa vita
kukutana na Mfilisti huyo.
‎Daudi akautia mkono wake
ndani ya mfuko wake,
‎akachukua jiwe kutoka humo,
na kulirusha kwa kombeo.
‎Akampiga Mfilisti huyo
kwenye paji la uso,
‎na jiwe hilo likapenya
katika paji la uso wake,
‎akaanguka
chini kifudifudi.
‎Basi Daudi akamshinda Mfilisti
huyo kwa kombeo na jiwe;
‎ alimpiga Mfilisti
huyo na kumuua,
‎ingawa Daudi hakuwa na
upanga mkononi mwake.
‎Daudi akaendelea kukimbia
na kusimama juu yake.
‎Kisha akaushika upanga
wa Mfilisti huyo
‎na kuuchomoa kutoka
katika ala yake,
‎akahakikisha
kwamba amekufa
‎kwa kumkata kichwa
kwa upanga huo.
‎Wafilisti walipoona kwamba
shujaa wao amekufa, wakakimbia.
‎Tunajifunza kuhusu ujasiri
‎kutokana na simulizi
la Daudi na Goliathi.
‎Pia tunajifunza kuhusu
kutumia hekima
‎na kuonyesha
imani kwa matendo.
‎Daudi alikuwa
akifanya kazi
‎baba yake alipomwambia
awapelekee ndugu zake
‎ chakula vitani.
‎Kwa hiyo,
‎Daudi alitarajia kufanya
mambo mawili wakati uleule.
‎Angewatunzaje kondoo
wa familia yake
‎na wakati huohuo kuwapelekea
chakula ndugu zake
‎waliokuwa umbali wa
kilomita kadhaa?
‎Alitumia hekima.
‎Pia, alionyesha
kwamba alitegemeka.
‎Biblia inasema:
‎“Daudi akaamka
asubuhi na mapema
‎na kuwaacha kondoo
mikononi mwa mtu mwingine;
‎kisha akapakia vitu
hivyo na kwenda
‎kama Yese alivyokuwa
amemwamuru.”
‎Muda mfupi
baadaye,
‎alikabili hali
yenye kutia hofu.
‎Daudi alipokuwa
akiwatafuta ndugu zake
‎aliona jeshi la Israeli
likiwa limetishwa
‎na ukubwa wa Goliathi
na dhihaka zake.
‎Papo hapo,
‎Daudi alitenda
kwa ujasiri.
‎Aliuliza kwa nini
hakuna mtu
‎aliyekuwa amemuua
mtu huyo mwenye
‎kimbelembele
aliyemdhihaki Yehova.
‎Hata hivyo, Eliabu,
‎ndugu ya Daudi
alimkemea hadharani,
‎akatilia shaka nia yake,
‎akamwita mwenye
kimbelembele,
‎na akadai kwamba amewaacha
kondoo wa baba yake.
‎Hata hivyo, Daudi alijitolea
kupigana na Goliathi,
‎lakini mfalme
akampuuza.
‎Sauli alimwambia kwamba
hangeweza kumshinda Goliathi
‎kwa sababu Daudi
alikuwa “mvulana tu”!
‎Daudi alitendaje alipokabili
hali hizo zenye kuvunja moyo?
‎Alitenda kwa ujasiri.
‎Ujasiri huo ulimchochea kiroho
na kihisia ili aanze kazi.
‎Alikumbuka mambo ambayo
Yehova alimtendea zamani.
‎Daudi hakusahau kamwe
‎jinsi Yehova alivyomkomboa
kutoka kwa dubu na simba—
‎wanyama wenye mbio na
nguvu kuliko wanadamu.
‎Yehova hakumwokoa
tu Daudi
‎bali pia alimwezesha kuwaua
wanyama hao hatari.
‎Daudi angeweza kusema
hivi kwa uhakika:
‎“Yehova, aliyeniokoa
kutoka katika
‎makucha ya simba
na ya dubu,
‎ndiye atakayeniokoa kutoka
mikononi mwa Mfilisti huyo.”
‎Tunapokata tamaa au
kushuka moyo,
‎tunaweza kufaidika
kwa kutafakari
‎jinsi Yehova alivyotukomboa
tulipokabili matatizo
‎yaliyoonekana kuwa
makubwa sana, sivyo?
‎Daudi alikuwa jasiri
na akaanza kazi.
‎Alifanya maamuzi na
akapata matokeo mazuri.
‎Kwa mfano, Sauli alipompa Daudi
mavazi yake mazito ya vita,
‎Daudi alijaribu kuyavaa.
‎Lakini akatambua
kwamba angelemewa
‎kwa kuvaa kofia ya shaba,
‎koti la vita,
‎na kufunga upanga
juu ya vazi lake.
‎Basi, alifanyaje?
‎Kwa kweli,
‎alirahisisha mambo!
‎Aliuondoa mzigo huo.
‎Namna gani sisi?
‎Kwa miaka mingi,
‎huenda tumejaza maisha
yetu vitu tusivyohitaji
‎au shughuli
zisizo za lazima.
‎Vitu hivyo vinaweza
kutuathiri kiroho.
‎Ikiwa hali yako
iko hivyo,
‎kwa nini usianze kazi?
‎Orodhesha vitu vyako
na mazoea yako,
‎na uondoe vitu
visivyo vya lazima.
‎Tukirahisisha
maisha yetu,
‎itakuwa rahisi zaidi
kwa jicho letu
‎kukazia utumishi
kwa Yehova.
‎Kama sisi, Daudi
hakuwa mkamilifu.
‎Lakini matendo
yake ya ujasiri
‎yalimfanya awe na urafiki
wa karibu na Yehova.
‎Kwa hiyo, mwishoni mwa
maisha yake ya uaminifu,
‎Daudi akiwa na uhuru
mwingi wa kusema
‎angeweza kumwambia
hivi mwanawe:
‎“Uwe jasiri na imara
‎na uanze kazi”!