JW subtitle extractor

Danieli: Alionyesha Imani Maisha Yake Yote —Sehemu ya 1

Video Other languages Share text Share link Show times

Mfalme
Unasemaje?
Jiji halina chakula
lakini Yehoyakini
hataki kukutana nasi
Makubaliano yenu
mimi hayanihusu
lakini uzembe wako
ndio unaonikasirisha
Waangamize
la sivyo nitakuua
Sawa mfalme
Hivi ndivyo Yehova
wa majeshi anasema;
Kwa sababu hamkutii
maneno yangu
nchi yote hii
itakuwa magofu,
nanyi mtalazimika
kumtumikia mfalme wa Babiloni
kwa miaka 70.
Danieli,
ulikuwa wapi
mbona umerudi jioni sana?
Samahani mama
nilikuwa hekaluni
nikimsikiliza Yeremia.
Sawa,
chakula kiko tayari.
Ulikuwa hekaluni leo
Ndio
Ili kuutazama
uzuri wa Yehova
Na kutazama
kwa uthamini hekalu lake
Hii ni zawadi yako
Ili sikuzote
uwe na Neno la Yehova
Asante baba,
Uko sawa?
Sijui ni nini
kitakachotupata?
Sikuzote Yehova
hawaachi watumishi
wake waaminifu
Usihofu
Yehova ni ngao yetu
Chakula tayari,
Mama ulimwona
jirani yetu leo?
Sijamwona, kuna nini?
Nilishangaa,
yaani Eli ana
matatizo sana
Yaani Eli huwa
hakosi vituko
Acha tuimbe,
Mwanangu chagua wimbo
Yehova Nuru yangu
na Wokovu wangu
kila siku
unauchagua huohuo
Hushimu
Yehova ni nuru,
wokovu wangu,
siogopi
Danieli,
njoo tucheze
Saa hii naondoka na Baba
Ukirudi tutacheza
kama safina ya Noa
Eeh, wewe utakuwa nani?
Nitakuwa simba,
Aha,
na mimi nitakuwa tembo
Yehoyakini amesalimu amri
Nyumba ya Eberi,
wa kabila la Yuda,
Fungua haraka
Tayari wameingia
kusanyeni vitu,
tuondoke
Tuondoke,
tunaenda wapi?
Hatutaishi tena hapa.
Hushimu, chukua mizigo
Sikupendi huku
Ah, tuingie
ndani mwanangu.
Fungua mlango
Wote wanne tokeni nje,
angalia vyumba vya nyuma.
Kwa amri ya Mfalme
mtaondoka na sisi
Wewe ni Danieli
wa kabila la Yuda,
Utapata mazoezi
katika nyumba
ya mfalme mkuu
Nebukadneza
Yaani niondoke nyumbani?
Wakuu wanaishi
kwenye nyumba ya mfalme
Yeye si mkuu
ni mvulana tu
Danieli,
Kama mnataka mtumishi
nichukueni mimi
La!, Nataka huyu mvulana
Danieli
Subiri,
tunaweza kumuaga
Sawa,
na usitucheleweshe
Uwe imara mwanangu,
Yehova yuko pamoja nawe
Danieli,
Ah Mishaeli,
umekutana na mtu
yeyote tunayemjua?
Unafikiri tungekuacha
uje peke yako,
Ah, Azaria, Eeh Hanania
Hawa ni Khislon na Ahitubu
Nafurahi kuwafahamu
Twende,
Kwani tunaenda wapi?
Nafikiri kwenye
nyumba ya mfalme
Kwa hiyo tutakuwa
kama Yosefu
kwenye nyumba
ya Farao eeh
Ah wapi kama
Yosefu gerezani
Ah lakini si kubaya sana
Duh Khisloni,
wasichana warembo
Ukikataa mimi
nitaongea nao
Eh mambo?
Safi,
twende
urudi tena sawa
Hawa ndio wale
vijana Wayahudi
ambao Ashipenazi
alisema waletwe
Mmechaguliwa
kwa sababu mna hekima
Lakini nyinyi si wasomi,
mtajifunza maandishi yetu
na lugha yetu
Mtapewa majina mapya,
baada ya miaka mitatu,
mtamtumikia mfalme
mkuu Nebukabneza
Leo, ninyi ni wageni,
kesho eh,
miungu wakipenda
mtakuwa wababiloni
Meshaki,
ah, hilo jina linakufaa
Haya majina ni
kama ya miungu yao,
Majina mapya, lugha mpya,
mwishowe watatuambia
tuabudu miungu yao
Tulia,
baba yangu ana sanamu
na bado anamwabudu Yehova
Hili jiji ni zuri,
kitovu cha ulimwengu,
na tutakula kwenye
meza ya mfalme,
Kwani Wababiloni hula nini?
Watumishi wa mfalme hupewa
vyakula bora kama hivi,
Hatuwezi kula hiki chakula,
kwani kuna shida gani?
kwa sababu si safi
Kuna shida yoyote?
Mungu wetu haturuhusu
kula chakula kama hiki
Mnamwogopa Mungu wako?
Ndio
Hata mimi
ninamwogopa,
bwana wangu mfalme,
ambaye ameniagiza
niwape vyakula
na vinywaji hivi
Anataka mle vyakula hivi
ili muwe na nguvu na afya,
Itakuwaje akiona kwamba
afya yenu ni mbaya
kuliko ya vijana wengine,
Mtanifanya niwe na
hatia mbele za mfalme,
Lazima nimtii mfalme,
wewe pia, nyinyi nyote
Chakula kikiandaliwa,
lazima mkile
Wewe si msemaji wetu
Ni sawa,
unaweza kujiamulia
unalotaka,
Kwani wewe hujamsikia,
hatuna la kufanya
Tuko nchi nyingine,
na lazima tufuate
sheria zao
Haijalishi chakula
kina damu,
ni chakula tu
Lakini Yehova
ametuamuru tusile damu
Hiyo ni tafsiri yako
Hampaswi kula
damu yoyote,
hilo liko wazi
Itakuwa vizuri tukisali
kuhusu jambo hili,
Kusali, hapa
Kwa nini tusali,
Yehova yuko Israeli,
na sisi tuko Babiloni
Kwani huamini Yehova
yuko hapa pia?
Yehova amesema
sisi ni Mashahidi wake,
watu watamwonaje Yehova
ikiwa tutavunja
sheria zake?
Chakula tayari.
Hamjanisikia au?
Asante,
lakini tukila
vyakula hivyo,
tutamkosea
Mungu wetu
Mnataka kufa
njaa, siyo?
Hapana lakini,
Mungu ametukataza
kula damu
na vyakula ambavyo
anaona si safi
Tafadhali,
tujaribu sisi watumishi
wako kwa siku kumi,
Tupe mboga za majani
na maji ya kunywa.
Mboga eeh
Tupe siku kumi tu
Halafu tutendee kulingana
na jinsi tunavyoonekana
Tupe siku kumi,
Ah, safi sana,
asante Yehova
Onjeni kidogo hii
nyama ni tamu
Mmewahi kula
chakula kama hiki
Ah,
Safi Yeeh
Ashpenazi anawaita
Bwana wangu
vijana hawa ndio wale
Nawajua
Tumekuwa tukiwafuatilia,
nyinyi nyote
Hamziinamii sanamu zetu,
mnasali kwa Mungu wenu tu,
Na hamli vyakula vyetu eeh
Walisisitiza kwamba
Mungu wao,
Lakini
naona mna afya
nzuri kuliko wengine,
endelea kuwapa
chakula walichoomba.
Belteshaza
Nimeona una kipawa,
usikipoteze
Kundi linalofuata
Jumla itakuwa Kuru 15,
panu 2 na sutu 5
Vizuri sana
Mfanyabiashara anapaswa
kutoza riba kiasi gani
kwa pesa na nafaka?
Asilimia 40 bwana wangu
Asilimia 40 eeh,
yaani miaka hii mitatu
umekuwa ukijifunza wizi eeh
Na wewe Meshaki?
Ni asilimia 20
Vizuri sana
Nyota ipi ya Enlil
inayong’aa zaidi
katika kundi la Urgula?
Unajua?
Ni nyota ya Lugali
Eeh vizuri,
Kuna mnara mrefu
lakini hauna kivuli,
ni mnara gani?
Ziggurati
Bure kabisa
Wewe unajua jibu?
Ni mwanga wa
jua bwana wangu
Sahihi
Wanaume wangu
wenye hekima
hufundisha kwamba miungu
hupanga mambo yote,
Ikiwa ndivyo,
kwa nini watu
wazuri huteseka
na waovu wanafanikiwa?
Hakuna aliyeweza kujibu
Kama usemavyo
eeh mfalme,
wenye hekima
hawapati chakula sikuzote,
wala werevu
hawawi na utajiri sikuzote,
wala wenye ujuzi
hawafanikiwi sikuzote,
kwa sababu wakati
na matukio yasiyotarajiwa
huwapata wote.
Hayo ni maneno ya nani?
Sulemani
Alijulikana kwa
hekima yake
Lakini chanzo
chake Mungu wake,
Mungu wetu, Yehova
Waondoe hapa
Tutarudi tena
Hamtarudi,
rudini nyumbani,
hamfai kitu
Belteshaza,
nyinyi wanne msiondoke,
ninataka kuzungumza nanyi
Simjui Mungu wenu
lakini mmethibitika
kuwa bora mara kumi
kuliko makuhani
na wafanya
mazingaombwe wote
niliokutana nao
Ashpenazi atahakikisha
mnatumikia hapa
na waume wenye hekima
Ikiwa mlipoteza vipawa
vyenu Yerusalemu,
hapa mtavitumia vizuri
Tumekamilisha
ushindi Yerusalemu
Majeshi yetu yanajitayarisha
kuzingira Tiro
Wanapaswa kukumbuka
kilichompata Sedekia
Miungu iko pamoja nasi
Yera kuna nini?
Kuhusu Yerusalemu
Unaenda wapi?
Kuiona familia yangu
Mwaka huu tumelazimika
kuishi kwa vitu vichache
Danieli
Njoo ule
Uko sawa
Kuna shida
Ni Yerusalemu,
wamebomoa kuta,
wameteketeza minara yake
Wengi wamekufa na
wameteketeza
nyumba ya Yehova
Kwa nini watu
wetu hawakusikiliza,
kweli walifikiri Yehova
hatayaona matendo yao
Hekalu lilipokuwepo
watu walikuwa na tumaini
Kwa kuwa Yehova yupo
tuna tumaini
Lakini ametukataa
kwa sababu tumetenda
mambo maovu
Lakini hajamkataa kila mtu,
Yehova alimwambia Ezekieli
kwamba machoni pake,
Wewe
ni mwadilifu kama Noa
na Ayubu
Alisema hivyo
Ndiyo
Ikiwa Yehova
anatujali sana,
kwa nini bado
tuko uhamishoni?
Kwa nini haturudi nyumbani
na kwa nini hatuko pamoja?
Upo nyumbani mwanangu.
Sina majibu
yote mwanangu,
kaa karibu na Yehova,
naye atakubariki
Waite wanaume
wenye hekima
Nimeota ndoto,
na inanifadhaisha,
ninataka kujua nilichoota?
Eeh mfalme
na uishi milele,
tuambie ulichoota,
nasi tutakwambia
maana yake
Aahaa,
msiponiambia
ndoto yangu
na kunieleza maana yake,
mtakatwakatwa,
na nyumba zenu zitageuzwa
kuwa vyoo vya umma,
lakini mkiniambia
ndoto yangu
na maana yake
mtapata zawadi,
na tuzo
na heshima kubwa
Tunahitaji kupata muda
wa kuwasiliana na miungu,
Hati zitatuambia alichoota
inabidi tupange mikakati
Anataka tumwambie
ndoto yake
Ndiyo,
lakini hakuna mtu aliyewahi
kuuliza jambo hili.
Sasa tufanyeje?
usimpe jibu mapema
ili tuwasiliane na miungu
Mmekubaliana kunidanganya
na kunihadaa
mkitumaini hali
itabadilika eeh
Eti kukudanganya,
Mnanidanganya
Hakuna yeyote duniani
anayeweza kufanya jambo
unaloagiza mfalme.
Jambo unaloomba
eeh mfalme ni gumu,
hakuna yeyote anayeweza
kukwambia isipokuwa miungu.
Arioko wakamate.
Wauwe
Wakamate watu wote
wenye hekima haraka
Nenda, nenda,
nenda, nenda, nenda
Kwa agizo la mfalme
wakamateni wote
Yera
Uko hatarini,
Nini kimetokea?
Sijasikia kila kitu,
lakini watu wenye hekima
wamemkasirisha mfalme
Watauawa kabla ya asubuhi
Kawaite Hanania,
Mishaeli na Azaria,
ninahitaji kujua kilichotokea
Ndio, Wakaldayo,
Wamisri, Wayahudi,
wanaume wote
wenye hekima
Arioko
Belteshaza,
hukupaswa kuwa hapa
Kwa nini mfalme
ametoa agizo kali hivi?
Aliota ndoto
na hakuna mtu
yeyote anayeijua
Toroka sasa hivi,
ukifanya hivyo
kabla ya mapambazuko,
unaweza ukasilimika.
Hivi kwa nini
nilikwambia uwalete
na hujawaleta?
Kwa nini miungu
haiwasiliani nao?
Ninataka wao
na watu wote wa familia zao
waletwe hapa,
nataka kujua
Wachuneni ngozi
na kuwatundika mtini,
acha miungu
ione miili yao,
na muitupe
kwenye mto Efrati
Ashipenazi
Kuna faida gani
ya kuwa na watu
wenye hekima,
ikiwa hawana hekima
Unafanya nini hapa?
Nahitaji kuzungumza
na mfalme
Unahitaji kuondoka
Tafadhali niruhusu
niongee naye
Bwana wangu,
Belteshaza angependa
kuzungumza nawe
Eeh mfalme,
Mungu wangu Yehova
anajua maana ya ndoto
Anajua ulichoota
na maana yake,
Mungu wako yuko wapi?
Yuko wapi?
Ninaamini,
ninajua yeye atanifunulia,
tafadhali nipe
muda kidogo
Tuna muda mfupi sana
Wa kufanya nini?
Wa kumfunulia
mfalme ndoto yake
Kuna lolote ambalo
Yehova amekufunulia?
Hapana, hajasema lolote.
Lakini Yehova aliahidi
atakwambia maana yake,
sivyo?
Mh, hapana
Una uhakika wowote
kwamba Yehova atakufunulia?
Aah sina uhakika
Unahitaji kuwa
na uhakika.
Jina lake linahusika,
ikiwa atafunua ndoto hii
atathibitisha yeye
ni Mungu wa kweli.
Na asipofunua?
Kuna jambo lolote
tunaloweza kufanya?
Tusali,
tusali Yehova
atuonyeshe rehema.
Eeh Yehova,
kwa hakika
hujatuleta hapa ili tufe
Watu watasemaje,
tuliwaambia kwamba
wewe ni Mungu
wa mbinguni
Mungu pekee
anayeweza kufunua siri
Tafadhali
litetee jina lako
Yera
Nimempata mwanamume
fulani kutoka Yuda
anayeweza kukueleza
maana ya ndoto yako
Ninamjua
Je, kweli unaweza
kuniambia ndoto niliyoota
na maana yake?
Kuna Mungu mbinguni
ambaye ni mfunuaji wa siri
Nawe amekujulisha
wewe mfalme Nebukadneza
mambo yatakayotukia katika
kipindi cha mwisho
cha zile siku.
Hii ndiyo ndoto yako.
Uliona sanamu kubwa sana.
Sanamu hiyo
ilisimama mbele yako.
Wewe
ndiye kichwa
cha dhahabu.
Baada yako
ufalme mwingine utainuka,
ulio dhaifu kwako.
Kisha, ufalme mwingine,
wa tatu, wa shaba
ambao utaitawala
dunia yote.
Kuhusu ufalme wa nne,
utakuwa na nguvu
kama ya chuma.
Ufalme huo utagawanyika.
Vidole vya miguu
vilikuwa kwa sehemu chuma
na kwa sehemu
udongo wa mfinyanzi.
Hivyo ufalme huo
utakuwa na nguvu
kwa sehemu na
dhaifu kwa sehemu.
Katika siku za wafalme hao,
Mungu wa mbinguni
atausimamisha Ufalme
ambao haitaangamizwa kamwe.
Ufalme huo hautakabidhiwa
watu wengine wowote.
Utaziponda ponda
na kukomesha
falme hizi zote
nao pekee utasimama milele.
Ndoto hiyo ni ya kweli
na maana yake
inategemeka.
Fanyeni haraka,
mvalisheni vazi bora
na mkufu wa dhahabu.
Fukizeni uvumba
mbele yake.
Kwa kweli Mungu wako
ni Mungu wa miungu,
na Bwana wa wafalme
na mfunuaji wa siri.
Mungu wako na aheshimiwe
kwa heshima ninayokupa.
Kuanzia sasa,
wewe ni mtawala
wa mkoa wote wa Babiloni.
Ee mfalme,
watumishi hawa pia
wanamwabudu
Mungu wa mbinguni.
Ninaomba wao pia
wawe wasimamizi wa mkoa.
Litekeleze ombi hilo.
Umethibitisha wewe
ni bora zaidi
kuliko hawa wanaojiita
wenye hekima.
Ninakuweka rasmi
kuwa msimamizi wao mkuu.
Ulisikia alichosema
Nebukadneza?
Aliposema
Mungu wako ni
Mungu wa miungu
na Bwana wa wafalme?
Yehova amejibu sala yako.
Yehova amejibu sala zetu.
Kwa hiyo ni nini kitakachofuata?
Tutarudi Yerusalemu?
Sijui kitakachotokea
lakini maadamu
tuko karibu na Yehova,
sikuzote atakuwa pamoja nasi,
maadamu tuna
imani kwake.
Nyota hazionyeshi
eti ufalme utaponda
ufalme mwingine.
Ni kweli.
Kuna kamchezo hapa.
Lakini alijuaje
ndoto hiyo?
Amarutu!
Amarutu kuna ujumbe gani
kutoka kwa miungu?
Nimechunguza ini la kondoo.
Una wakati ujao mzuri.
Ile nyota kubwa ya shabatu
inaeleza tu kuhusu
utukufu wako.
Na mimi ndiye
kichwa cha dhahabu.
Yehova amesema.
Ndoto yako ilifunua
mambo mengi mazuri,
lakini huyu Belteshaza
ni Myahudi tu.
Ni kweli,
ni Myahudi mwerevu.
Hakuwa na uwezo
wa kutafsiri ndoto
kabla ya kuja Babiloni.
Alihitaji kwanza
kuelimishwa hapa
na kupewa jina la kibabiloni.
Jina linalomtukuza
mungu wetu mkuu, Beli.
Beli alitumia kijana huyo
aliyetekwa kukufunulia
mambo makubwa.
Ni Beli,
si Yehova uliyemshinda
huko Yerusalemu.
Kwa hiyo mti ni
adui zangu, sio?
Huyu anayetajwa
baada ya nyakati
saba kupita ni nani?
Eh, ni wewe tena,
eeh mfalme mkuu.
Ninyi ni wajinga kabisa.
Hatimaye!
Belteshaza,
mkuu wa makuhani
wanaofanya uchawi.
Hawa wote wameshindwa
kunifafanulia ndoto yangu.
Lakini wewe unaweza.
Niambie maana
ya mambo niliyoota.
Uliota nini?
Niliona mti
katikati ya dunia.
Nao ulikuwa
mrefu kwelikweli.
Mrefu sana.
Mti huo ulikua na kuimarika
na kilele chake
kikafika mbinguni.
.. kikafika mbinguni
na mti ukaendelea kukua.
.. ukaimarika..
.mtakatifu.
..nikamwona mlinzi.
..ukateni na
kuuangusha mti huu.
.. ukaimarika..
kwa pingu ya
chuma na ya shaba.
Basi mti huo ni nani?
Ee bwana wangu,
ndoto hii na iwahusu
wale wanaokuchukia
na maana yake itimie
kwa maadui wako.
Mti ulioona
ambao ulikua mpaka
ukawa mkubwa na kuimarika,
ambao kilele chake
kilifika mbinguni,
na ambao ulionekana
duniani pote,
ulikuwa na majani
yanayopendeza,
matunda mengi
na chakula kwa ajili ya wote.
Na ambao chini yake
wanyama wa mwituni waliishi
na ndege wa angani
hukaa kwenye matawi yake,
ni wewe, Ee mfalme.
Wewe mfalme
ulimwona mlinzi mtakatifu,
akishuka kutoka
mbinguni akisema,
ukateni na
kuuangusha chini
mti huu na kuuharibu
lakini kiacheni kisiki
na mizizi yake ardhini
kikiwa na pingu ya
chuma na ya shaba.
Na acheni umande
wa mbinguni ukiloweshe,
na acheni fungu lake
liwe pamoja na
wanyama wa mwituni
mpaka nyakati saba zipite.
Ee mfalme
hii ndiyo maana yake.
Ni agizo la aliye juu zaidi
utafukuzwa mbali kutoka
miongoni mwa wanadamu.
Nawe utaishi na
wanyama wa mwituni
nawe utapewa majani
ule kama ng’ombe dume
na utalowa kwa
umande wa mbinguni.
Na nyakati saba zitapita
mpaka utakapojua
kwamba Aliye Juu Zaidi
ni mtawala katika
ufalme wa wanadamu
na yeye humpa ufalme
yeyote anayetaka.
Lakini kwa sababu
walisema kisiki
kiachwe na mizizi yake,
utarudishiwa tena ufalme wako
baada ya kujua kwamba
mbingu zinatawala.
Geuka uziache dhambi zako
kwa kutenda yaliyo sawa
na uache uovu wako
kwa kuwaonyesha
maskini rehema.
Huenda
muda wa ufanisi
wako ukarefushwa.
Belteshaza anajua
mambo haya yatatukia lini?
Hapana,
lakini watu wenye hekima
wanatilia shaka tafsiri yake.
Hebu fikiria.
Miungu ya Misri
iliwaambia Wamisri
kwamba watatushinda,
lakini wewe ukawashinda.
Basi kwa nini tumwamini
Mungu wa Wayahudi.
Angalia mambo uliyotimiza.
Miungu iko pamoja nawe.
Umefanya Babiloni
kuwa ufalme mkubwa
zaidi duniani.
Belteshaza
anataka ujinyenyekeze
kama mtumwa.
Wewe!
Mfalme imara,
ufalme wenye nguvu.
Acha tuendelee
na mazungumzo yetu
kuhusu nyota za enlili.
Nyota ya lugali
ndiyo nyota inayong’aa zaidi
katika kundi la urgula.
Nyota zinategemeka
si kama miungu ya
mataifa yaliyoshindwa.
Rudi Yerusalemu.
Oh, ungeweza
ikiwa kungekuwa na
chochote kilichobaki.
Je, Yehova amefunua
jambo lolote jipya?
Miezi kumi imepita
na mfalme hana dalili
yoyote ya uenda wazimu.
Ninamwamini Mungu wangu.
Na sisi pia tunaamini
tunaposoma nyota
lakini tunaamua ujumbe
utakavyotafsiriwa.
Utawajibishwa
kwa maneno uliyosema.
Lakini mtu mwenye hekima
anaposema uongo.
Nilizungumza tu kile
ambacho Yehova alifunua.
Umesahau
kilichowapata wale walioshindwa
kutafsiri ndoto ya ile sanamu?
Walihukumiwa kifo.
Na ukajipendekeza
kwa mfalme
kwa kumwambia
eti ndiye kichwa
cha dhahabu.
Na sasa umemwambia
atakuwa mwenda wazimu
na hakuna kilichotokea.
Lazima itokee.
Litatokea au lisitokee,
lakini maneno yako
yalimkasirisha mfalme.
Ni uhaini mkubwa
na hakuna atakayekutetea.
Miezi kumi imepita
na hakuna kilichotokea
lakini maneno yako
yalimkasirisha mfalme
na mfalme hana dalili
yoyote ya uendawazimu
ni uhaini mkubwa
na hakuna atakayekutetea
Ili sikuzote uwe
na Neno la Yehova
Nifundishe njia yako
Ee Yehova.
Usinitie mikononi
mwa maadui wangu.
Kwa maana
mashahidi wa uwongo
wameinuka dhidi yangu
nao wanatoa vitisho
vya kunitendea kwa ukatili.
Ningekuwa wapi
ikiwa nisingekuwa na imani
kwamba nitauona
wema wa Yehova
katika nchi ya walio hai?
Tafadhali tujaribu sisi
watumishi wako kwa siku kumi
lakini naona mna
afya nzuri kuliko wengine
Endelea kuwapa
chakula walichoomba
Simjui Mungu wenu
lakini mmethibitika
kuwa bora mara kumi
kuliko makuhani
na wafanya mazingaombwe wote
niliokutana nao
Aliota ndoto
na hakuna mtu
yoyote anayeijua
Yehova amejibu sala yako
Mtumaini Yehova,
uwe jasiri
na uwe na moyo mkuu.
Naam, mtumaini Yehova.
Tayarisheni dhabihu kwa Beli.
Kwa miungu!
Kwa miungu!
Kwa miungu!
Jiji hili,
ndilo kuu duniani,
lango la ishtari, mabustani.
Zigurati ni mrefu sana
unafika kwa miungu.
Hakuna anayeweza kubisha.
Haipatani na akili kwamba
miezi 12 tu iliyopita
ilisemekana utakuwa
mwenda wazimu.
Je, hii siyo Babiloni kubwa
ambayo nimeijenga
mimi mwenyewe
kuwa makao ya kifalme?
Kwa nguvu zangu mwenyewe
na kwa ajili ya utukufu
wa ukuu wangu?
Unaambiwa hivi
Ee mfalme Nebukadneza,
ufalme umekuponyoka,
nawe unafukuzwa mbali
kutoka kati ya wanadamu.
Utaishi na wanyama wa mwituni
nawe utapewa majani ule
kama ng’ombe dume.
Na nyakati saba zitapita
mpaka utakapojua
kwamba Aliye Juu Zaidi
ni mtawala katika
ufalme wa wanadamu
na Yeye humpa ufalme huo
yeyote anayetaka kumpa.
Hapana,
Baba!
Baba!
Wewe na wanaume
wako wenye hekima
mmeshindwa kabisa.
Mnawezaje kusema kwamba
Danieli alikuwa na hila?
Hiyo ni njama.
Danieli alitunga njama
dhidi ya baba yako.
Eti njama?
Na aliwezaje kuitekeleza?
Mambo yote
aliyosema yametimia,
lakini mliyosema
hayajatimia.
Baba yangu aliwaamini
na niliwaamini pia.
Nyote mlikosea,
nyinyi au Marduki,
vyovyote vile.
Hebu niambieni,
huyu Mungu wa mbinguni,
Yehova, ni nani?