JW subtitle extractor

Danieli: Alionyesha Imani Maisha Yake Yote —Sehemu ya 2

Video Other languages Share text Share link Show times

Viko hapa
Msifuni Nebo, Ishtari, na Marduki
Mungu mkuu kuliko wote.
Waite watu wenye hekima
waite watu wenye hekima
Sijui hicho ni kitu gani
hakuna jambo lolote
kama hilo kwenye vitabu
Wanaume wote wenye
hekima ndio hawa?
Hawa ndio bora
katika ufalme wote
Tafadhali nahitaji
kuzungumza na mfalme
Eeh mfalme,
Mama yako anataka
kuzungumza nawe
Eeh mfalme, na uishi milele
kuna mwanamume
kwenye ufalme wako
aliye na roho ya
miungu mitakatifu
atakueleza maana yake.
Ni nani huyo?
Danieli.
Danieli,
Danieli ni nani?
Wewe ndiye Danieli?
Ndio bwana wangu.
Nimesikia kukuhusu
kwamba unaweza kueleza
maana ya mafumbo
sasa,
ukifaulu kusoma
maandishi haya,
na kuniambia maana yake,
utavishwa mavazi ya zambarau
na mkufu wa dhahabu
shingoni mwako,
nawe utakuwa
mtawala wa tatu
katika ufalme,
sio lazima unipe
zawadi zako,
unaweza kuwapa
wengine zawadi hizo,
hata hivyo,
nitakusomea maandishi
haya Eeh mfalme
Mungu aliye juu zaidi
alimpa Nebukadneza ufalme,
ukuu na heshima yote
lakini moyo wake
ulipokuwa na kiburi
alishushwa kutoka kwenye
kiti chake cha ufalme
naye akanyang’anywa
heshima yake.
Lakini wewe Belshaza
hukunyenyekeza moyo wako,
ingawa ulijua
mambo haya yote.
Badala yake
ulijikweza mwenyewe
dhidi ya Bwana wa mbinguni,
ukaamuru wakuletee
vyombo vya nyumba yake,
kisha wewe,
wakuu wako,
masuria wako
na wake zako wadogo
mkavitumia kunywea divai,
na kuisifu miungu
ya fedha na dhahabu
miungu ambayo
haioni chochote
na haisikii chochote,
na haijui chochote,
lakini hujamtukuza Mungu
ambaye pumzi
yako na njia zako,
zote zimo mikononi mwake,
Hivyo, mkono huo,
ulitoka kwake.
Hii ndio maana
ya maneno hayo,
MENE,
Mungu amehesabu
siku za ufalme wako
na kuukomesha
TEKELI,
wewe umepimwa katika mizani
na umepungukiwa
PERESI,
ufalme wako umegawanywa
wakapewa Wamedi na Waajemi.
Mfalme Dario huyu ni Danieli,
Myahudi aliyetekwa na Wababiloni.
Je, wewe
ndiye uliyetafsiri
maandishi haya
kutoka kwa miungu?
La! si mimi, Eeh mfalme,
ni Mungu wangu
Mungu wa Israeli.
Liwali anayewafahamu vizuri watu
anaweza kutufaa.
Nakiri kwamba
unastahili cheo kikubwa zaidi,
kuliko uliwali
uliopewa na Belshaza.
Bwana wangu,
Danieli alikataa
zawadi zote na heshima
ambazo Belshaza
alitaka kumpa.
Mwanamume asiyekubali rushwa,
hustahili kuwa liwali tu,
nataka uwasimamie.
Tura,
tangaza cheo kipya cha Danieli
katika ufalme wote.
Nataka watu wote
wanaoiba katika hazina,
wajue kwamba
sasa watawajibishwa.
Danieli,
utakuwa ofisa
mkuu mzuri sana.
Kwa msaada wa Yehova tu.
Kwa nini kodi ya
ardhi iko juu hivi?
Mgomo mwingine tena?
Hali ni mbaya zaidi,
nimetoka kuchukua kodi
ya ardhi kwa msimamizi,
Alilipa?
Ndio lakini yeye hukataa
kutupatia malipo yetu.
Nimekumbana na
shida hiyo pia.
Eti wanasema malipo
hayo ya ziada ni wizi.
Kwa nini wamebadilika?
Ni Danieli.
Mmejaribu kumpa kitu
chochote kidogo ili atulie?
Hakubali hata shekeli moja.
Danieli anadai kwamba
kile anachopata
kinamtosha kabisa.
Msipumbazike,
anajifanya kuwa mnyoofu
ili ampendeze mfalme.
Atashindwa tu,
Dario atamchoka
punde si punde
Inaonekana kuna
upungufu kwenye kodi,
zinazopaswa kulipwa
kwenye hazina,
bwana wangu.
Asante kwa
ujasiri wa kutaja hilo.
Najua si habari nzuri.
Nitachunguza ushahidi.
Muda ulioishi hapa
umekufanya uwe
na hekima nyingi sana.
Umeishi hapa kwa muda gani?
Zaidi ya miaka sabini.
Nipe habari zaidi
Nieleze kuhusu ndoto
ulizomfafanulia Nebukadneza.
Yehova Mungu wangu
ndiye aliyeniwezesha,
alinifunulia ndoto hizo.
Kweli,
nimekaa Babiloni kwa
zaidi ya miaka sabini?
Aha, unabii wa Yeremia.
Miaka sabini itakapotimia,
nitamfanya mfalme
wa Babiloni awajibike,
na pia taifa hilo kwa
sababu ya kosa lao.
Unabii huo umetimia
Belshaza amekufa.
Jambo hili
linamaanisha nini
kwa watu wa Mungu?
Miaka sabini
itakapotimia huko Babiloni,
nitawakazia ninyi fikira.
Nami nitatimiza ahadi yangu
kwa kuwarudisha mahali hapa.
Aha, Yuda.
Lazima nisali kwa Yehova,
ili niungame dhambi
za watu wangu.
Eeh Yehova,
sikia, samehe,
Eeh Yehova,
sikiliza kwa makini,
na uchukue hatua.
Usikawie kwa ajili
yako mwenyewe.
Eeh Mungu wangu.
Eeh Danieli,
sasa nimekuja kukupa
ufahamu na uelewaji.
Ulipoanza kusali,
jibu lilitolewa,
nami nimekuja
kukujulisha jibu hilo.
Kuna majuma sabini
ambayo yameamriwa
kwa ajili ya watu wako
na kwa ajili ya jiji lako takatifu,
ili kukomesha uasi
Danieli,
Azareli na Hana wamekuja
Habari Danieli!
Nimefurahi sana kuwaona.
Eferi njoo tukae pamoja.
Nina habari nzuri sana.
Ni habari gani?
Yehova alikuwa
ametuambia tangu zamani,
tutarudi Yuda.
Niliuchunguza tena
unabii wa Yeremia.
Hivi ndivyo Yehova anavyosema,
Miaka sabini
itakapotimia huko Babiloni
Nitatimiza ahadi yangu
kwa kuwarudisha mahali hapa.
Miaka sabini,
watu wa Mungu watarudi
Yuda hivi karibuni.
Unawezaje kuwa na uhakika?
Yehova alimtuma
malaika aniambie.
Malaika?
Alisema,
jiji na hekalu lake,
litajengwa upya.
na mwishowe Masihi atakuja.
Wewe,
utajionea hekalu
likijengwa upya.
Si itakuwa hatari sana.
Yehova anatamani sana,
kutimiza mahitaji ya watu wake,
alimwambia Isaya
kwamba hatutazaa
watoto ili wataabike.
Kwa sababu wao,
ni uzao wa watu
waliobarikiwa na Yehova.
Na Yehova akisema kitu,
lazima kitimie.
Lakini nchi ni magofu!
Ndio sababu
tutahitaji wajenzi stadi
ili wajenge upya.
Inamaanisha na wewe
utarudi Yuda?
Ninatamani sana kurudi.
Panga kikundi cha wafanyakazi
warekebishe barabara,
la sivyo hali
itakuwa mbaya zaidi
msimu wa mvua.
Tura, fanyia kazi jambo hilo.
Inawezekanaje kwamba
unajua mambo mengi hivi?
Sistahili kusifiwa bwana wangu.
Tuna wanaume wengi
wenye akili
wanaotupatia habari,
Eeh mfalme.
Danieli,
kuhusu yule liwali wa Susa,
unafikiri anahitaji kubadilishwa?
Watu wangu wamefanya
uchunguzi wa kina,
na wamegundua kwamba
amekuwa akiiba
pesa za serikali
Aha, hapana hapana,
hiyo haiwezekani kabisa,
si huyo ni mpwa wako,
Otane?
Ndio,
nakuhakikishia
kabisa ni mwaminifu.
Lazima kuna tatizo
mahali fulani.
Huyu Danieli,
anawezaje kumjua
vizuri kuliko mimi?
Nitazungumza na mpwa wangu
nione tatizo liko wapi.
Sisi Wamedi na
Waajemi tuna huruma,
si kama hawa Wayahudi.
Tutasuluhisha jambo hili.
Sawasawa,
lisuluhisheni haraka
mnaweza kuondoka.
Bwana wangu,
samahani sana una wageni.
Mnachojua tu ninyi
Wayahudi ni kusali
Nisingeweza kumtumikia mfalme
kama ninavyofanya
bila msaada wa Mungu.
Kumtumikia mfalme eeh,
kwa kuwatisha maliwali?
Nimefanya tu
nilichopaswa kufanya.
Mgeni hawezi kutuambia
jinsi tunavyopaswa
kufanya mambo.
Ninahangaikia masilahi ya mfalme
Eeh, tumesikia
ulivyokuwa ukihangaikia
masilahi ya Nebukadneza
na ukamfanya
awe mwendawazimu
Huo ulikuwa ujumbe wa Yehova.
Sema chochote utakacho
lakini usiingilie
masilahi yetu
Ikiwa ilikuwa rahisi
kumwondoa liwali,
fikiria itakavyokuwa rahisi
kukinyamazisha
kibabu cha Kiyahudi.
Ni heshima kubwa kuwa hapa,
mnajua kwa nini nimewaita?
Hapana bwana wangu
Kuhusu yule liwali
ambaye Danieli
alipendekeza aondolewe,
Je, mlifuatilia?
Naam ndio
Tulifanya uchunguzi
wa kina sana
Je, alikuwa mzembe?
Hata kidogo.
Hakutimiza wajibu
wake vizuri?
si hivyo.
Aliwasilisha kodi
zote zilizokusanywa?
Hakuna shekeli
yoyote ya dhahabu,
au lita ya bia
inayokosekana.
Lakini Danieli
ana maoni tofauti na hayo,
Aha, aliwatumikia
wafalme wa Babiloni vizuri,
lakini, amezeeka sana.
Otane anamaanisha kwamba
maamuzi ya Danieli
na uzee wake
hayawezi kutegemeka
mawazo yake ni
ya kizamani sana.
Isitoshe, yeye ni Myahudi tu
Katu, hatumbagui mtu yeyote.
Hicho ndicho ninachomaanisha.
Danieli tulikuwa
tukizungumza kukuhusu.
Ulikuwa sahihi,
vurugu zimetokea kule Susa
wanadai wapewe liwali mpya
ambaye hatawaibia.
Lakini bwana wangu, Imetosha
nimewatuma wakaguzi
ninaowaamini.
Danieli,
umejidhihirisha kuwa tofauti
na hawa watu
wazia mambo
ambayo ningetimiza
ikiwa ungekuwa
waziri mkuu
Unaonaje tukizungumza
na mfalme?
Haitasaidia,
Danieli anampotosha sana.
Tunahitaji kumshtaki Danieli
kwa kitu ambacho hata
Dario mwenyewe hatapinga.
Hajawahi kupatikana na shtaka.
Litapatikana tu.
Tafuta watu watakaochunguza
kwa umakini zaidi sheria zetu
lazima amevunja sheria fulani.
Wewe, wahoji
wafanyabiashara,
wakaguzi na maofisa,
yeyote yule mwenye
shtaka dhidi yake,
mwakikishie yule atakayeshtaki
atapata zawadi nono.
Tuna rekodi za Babiloni,
tafuta jambo lolote
litakalomchafua.
Aha, hatujaona chochote.
Umepata jambo lolote?
Hakuna hata shekeli
moja inayokosekana,
isitoshe Danieli
anaposimamia mambo,
hasara na ufisadi
unapungua sana.
Endelea kukagua
Hakuna atakayemshtaki,
wote wanampenda,
na mfalme anamwamini.
Kwa kawaida
wafanyabiashara wa kigeni
hupuuzwa wanapoibiwa.
Lakini Danieli huwatetea,
na kufanya uchunguzi.
Anawalazimisha wezi
warudishe chochote kilichoibiwa.
Hata rafiki zake
hawana lawama.
Kuna wakati Nebukadneza
aliwakataza watu
wasizungumze vibaya
kuhusu Mungu wao
Inasemekana huyu, Yehova
aliwakomboa kutoka
katika tanuru la moto
walipokataa kumwabudu
mungu fulani wa Babiloni,
Wayahudi hawaabudu
miungu mingine Eeh,?
Inaonekana hivyo
Nafikiri sasa
umesuluhisha tatizo letu
Katu, Otane,
mnataka nini?
Eeh mfalme Dario,
uishi milele
Hii Babiloni
unayotawala ni kubwa,
hata hivyo ina
watu mbalimbali
Kuna Wababiloni, Wamisri,
Wagiriki na wengine
naam Otane
nafahamu mambo hayo
Wewe ndiye mfalme
lakini ni mgeni
aliyekuja hivi karibuni,
lazima watu wazoee
huu utawala mpya,
la sivyo utatetereka.
Mnapendekeza nini?
Maofisa wote wa mfalme,
wasimamizi, maliwali,
maofisa wakuu wa mfalme,
na magavana,
wameshauriana ili
mfalme atoe amri
na kutangaza marufuku
kwamba kwa siku 30
mtu yeyote atakayemwomba
mungu yeyote
au mwanadamu isipokuwa
wewe, Ee mfalme
anapaswa kutupwa
ndani ya shimo la simba.
Tunapaswa kudhibiti uasi,
angalia kilichotokea kule Susa.
Na sasa, Ee mfalme,
itoe amri hiyo
na kuitia sahihi,
ili isiweze kubadilishwa
kulingana na sheria
ya Wamedi na Waajemi,
ambayo haiwezi kufutwa.
Wakati huu milki yetu
ina amani na ufanisi
kuliko wakati mwingine wowote,
vitendo vya hivi karibuni
vya uasi huko Susa
pamoja na matendo
mengine kama hayo
yanayofanywa na vikundi
vidogo vya waasi
yamekusudiwa kubadili
njia yetu ya maisha,
nasi hatutakubali hilo litendeke.
Kwa heshima kubwa ya uhuru
mwingi wenye utukufu,
unaotolewa na milki hii,
na kama kikumbusho
cha mamlaka yake,
Mimi, Dario Mmedi,
natoa amri hii
kwa siku 30,
mtu yeyote atakayemwomba
mungu yoyote
au mwanadamu,
isipokuwa mfalme,
anapaswa kutupwa
ndani ya shimo la simba.
Kwa hiyo sasa utaacha kusali?
Ooh Azareli,
unanijua
na hata maadui
wangu wananijua,
ninasali dirishani kwangu
mara tatu kwa siku, kila siku.
Nikifanya wafikiri
eti nimelegeza
msimamo wangu,
watasemaje?
Umeacha kabisa kusali
na kibaya zaidi,
eti nimeacha ibada yangu
ili niokoe uhai wangu?
Ninamjua Yehova
na nikimtumaini
atanithawabisha.
Sijui jinsi gani
lakini atafanya hivyo.
Salini nidumishe imani yangu.
Sote tudumishe imani yetu,
hata matokeo yaweje.
Hii ni zawadi yako,
chakula tayari
Yehova ni nuru,
wokovu wangu,
siogopi
Nisikie, Eeh Yehova,
ninapolia kwa sauti,
nionyeshe kibali,
na kunijibu,
nitautafuta uso wako,
Eeh Yehova.
Wewe ni msaidizi wangu,
usinitupe,
wala usiniache,
Mungu wa wokovu wangu
Eeh mfalme na uishi milele,
Je, hukutia sahihi
marufuku ukisema,
kwamba kwa siku 30,
mtu atakayemwomba mungu
au mwanadamu yoyote
isipokuwa wewe Eeh mfalme,
atupwe ndani ya
shimo la simba?
Naam,
ndivyo ilivyo kulingana na
sheria ya Wamedi na Waajemi,
kwani mnataka nini?
Danieli, mhamishwa kutoka Yuda,
hajakuheshimu
wewe, Eeh mfalme
wala marufuku uliyotia sahihi.
Badala yake anasali
mara tatu kwa siku.
Danieli.
Haiwezekani, mna hakika?
na hakatai kwamba anasali.
Kuna mashahidi wowote?
Sote watano bwana wangu
tumeshuhudia hilo.
Lakini amezeeka,
anajua anachofanya?
Akiwa afisa mkuu
kwa kweli anajua
kinachomaanisha
na kumtii mfalme.
Ondokeni.
Tunaweza kumkamata Danieli?
Nitaamua la kufanya.
Nitamwadhibu Danieli
ili awe mfano kwa wengine,
nitamng’oa madaraka,
na kumfukuza jijini
kesho asubuhi.
bwana wangu.
Wote watajifunza
wanapaswa kutii sheria zetu,
lakini sheria iko wazi
mshtakiwa anapaswa
kutupwa ndani ya shimo
la simba bwana wangu
Nimetambua mnachotaka,
hamna hata aibu.
Sheria ya Wamedi
na Waajemi inasema,
marufuku au amri
yoyote ya mfalme
haiwezi kubadilishwa.
Tunatamani mfalme
apate heshima anayostahili.
Mtupeni shimoni
Mungu wako
unayemtumikia
daima atakuokoa.
Ondoa jiwe,
Danieli,
Danieli
Eeh mfalme, uishi milele.
Yuko hai!
mtoeni
Mungu wangu
alimtuma malaika wake,
akafunga vinywa vya simba,
nao hawajanidhuru,
kwa sababu sikupatikana
na hatia mbele zake
wala sijakutendea jambo
lolote baya, Eeh mfalme
Maeneo ya kaskazini ni yangu,
Danieli hakuyatumia ipasavyo.
Tunahitaji farasi wao bora
kwa ajili ya magari yetu
na wachache kwa ajili yangu
Sawa, wewe chukua
maeneo hayo,
nataka eneo la Baktria
na madini yake
Ni mapema sana
kugawanya maeneo ya Danieli
Angalia chumba cha nyuma,
Ni nini kinaendelea?
mnakamatwa kwa
sababu ya makosa
mliyomfanyia mfalme Dario
Mfalme aliagiza Danieli
akamatwe sio sisi.
Danieli alikamatwa,
akatolewa shimoni
na hajajeruhiwa
Haiwezekani
lazima simba
walikuwa wameshiba,
labda walikuwa wanaumwa.
Simba walikuwa
wanaumwa eeh,
hawakuwa na njaa eeh?
Watupe na familia zao
ndani ya hilo shimo
wakathibitishe wanachosema
Dario, hapana, usifanye
hivyo, tumekutumikia,
Ninatoa agizo kwamba
katika kila eneo
la ufalme wangu,
watu wanapaswa
kutetemeka kwa woga
mbele za Mungu wa Danieli
kwa maana yeye
ndiye Mungu aliye hai
naye huishi milele.
Ufalme wake
hautaangamizwa kamwe,
Huokoa,
naye hufanya ishara na maajabu
mbinguni na duniani.
Kwa sababu alimwokoa Danieli
kutoka katika makucha ya simba.
Dario ameandika hivyo?
Na itawafikia raia wote.
Tulikuwa na wasiwasi sana.
Uliogopa?
Niliogopa sana
lakini Yehova
hutusaidia tunapoogopa.
Baba na mama wanaogopa
kwenda Yerusalemu.
Jamani Eferi, mh
Bado tunafikiria jambo hilo
Utaenda, mfalme amesema
wote tunaruhusiwa kwenda.
Ningependa kurudi nyumbani,
lakini nimezeeka sana
Basi na mimi siendi.
Ooh jamani, jamani usilie
Ukienda utaona jiji bora zaidi
kuliko nililoacha.
Utajionea unabii ukitimizwa,
jiji lililojaa watu
wanaomwabudu Yehova
na hekalu jipya,
jengo maridadi zaidi duniani
Mama ulimwona
jirani yetu leo?
sijamwona kuna nini?
Nilishangaa yaani Eli
anakuwa na shida sana.
Kaa karibu na Yehova,
naye atakubariki
Jambo moja,
nimemwomba Yehova,
kwamba nikae,
katika nyumba ya Yehova,
sikuzote za maisha yangu,
ili kuutazama,
uzuri wa Yehova
na kutazama
kwa uthamini hekalu lake
Danieli,
endelea kupumzika,
Ee Danieli,
wewe mtu mwenye
thamani sana
nimetumwa kwako.
Usiogope, Ee Danieli.
Maneno yako yamesikiwa
tangu siku ya kwanza
ulipoukaza moyo wako
kupata uelewaji
na kujinyenyekeza
mbele za Mungu wako,
Nimekuja kukuelewesha
mambo yatakayowapata watu wako
katika kipindi cha
mwisho cha zile siku,
Sina nguvu kabisa,
na pumzi imeniishia,
Usiogope, Ee mtu
mwenye thamani sana.
Uwe na amani.
Uwe na nguvu,
naam, uwe na nguvu.
Sema bwana wangu,
kwa maana umenitia nguvu.
nitakwambia
mambo yaliyoandikwa
katika kitabu cha kweli.
Tazama!
Wafalme watatu zaidi
watasimama kwa ajili ya Uajemi,
na wa nne atajikusanyia
utajiri mwingi zaidi
kuliko wengine wote.
Ee bwana wangu,
matokeo ya mambo
haya yote yatakuwa nini?
Mwenye furaha ni yule
anayeendelea kutarajia
Endelea mpaka mwisho.
Utapumzika,
lakini utasimama
kwa ajili ya fungu lako
mwishoni mwa zile siku
Tukila vyakula hivyo
tutamkosea Mungu wetu,
Mnamwogopa Mungu wako,
ndio
Mungu wangu Yehova
anajua maana ya ndoto,
ninajua Yeye atanifunulia.
Yehova anatamani sana,
kutimiza mahitaji
ya watu wake,
ninamjua Yehova
na nikimtumaini
atanithawabisha.
Sijui jinsi gani?
lakini atafanya hivyo