JW subtitle extractor

Noa—Imani Ilimchochea Kutii

Video Other languages Share text Share link Show times

Siku tatu kabla
ya Yesu kuuawa,
wanafunzi wake
walimuuliza swali ambalo
ni muhimu sana kwetu leo.
Walimuuliza Yesu,
“Ni nini itakayokuwa
ishara ya kuwapo kwako
na ya umalizio wa
mfumo wa mambo?”
Yesu aliwajibu kwa kutabiri
mambo ambayo
yangetokea ulimwenguni
kabla ya kuja kwa
ulimwengu mpya.
Mambo hayo ni vita,
matetemeko ya ardhi,
upungufu wa chakula,
na magonjwa.
Kisha Yesu akasema:
“Kwa maana
kama walivyokuwa
katika siku hizo
kabla ya Gharika,
wakila na kunywa,
wanaume wakioa na
wanawake wakiolewa,
mpaka siku ambayo Noa
aliingia ndani ya safina,
nao hawakujali
mpaka Gharika ikaja
na kuwafagilia mbali wote,
ndivyo kuwapo kwa Mwana
wa binadamu kutakavyokuwa.”
Kwa maneno hayo,
Yesu alithibitisha kwamba
Noa alikuwa mtu halisi,
na kwamba gharika lilikuwa
tukio halisi la kihistoria.
Pia alituonya kwamba
mambo yanayotokea siku zetu,
yangefanana kabisa
na mambo yaliyotukia
kabla ya gharika.
Hivyo, ni muhimu
kuchunguza kwa makini
mambo yaliyotukia
katika siku za Noa
na masomo tunayoweza kujifunza.
Sura za kwanza
za kitabu cha Mwanzo
zinatusaidia kuwazia
jinsi maisha yalivyokuwa
baada ya Adamu na Hawa
kufukuzwa katika
bustani ya Edeni
—mamia ya miaka
kabla ya siku za Noa.
Watu wote
walizungumza lugha moja
na inawezekana
walibuni mfumo
wa kuandika maneno.
Walijenga jiji,
labda majiji kadhaa.
Walijifunza kufua
shaba na chuma.
Walitengeneza
vifaa vya muziki
kama vile filimbi na vinubi.
Kwa sababu walikuwa
wazao wa karibu
wa Adamu na Hawa,
ambao mwanzoni
walikuwa wakamilifu,
watu hao waliishi
kwa muda mrefu sana
mamia ya miaka.
Lakini,
hali haikuwa nzuri.
Watu walimwacha Yehova
hivyo wakawa wakatili
na wenye maadili mabaya.
Mambo yalikuwa
mabaya sana
kiasi kwamba Yehova
alimwongoza Enoko,
aliyezaliwa
miaka 600 baada ya
Adamu kuumbwa,
kutoa unabii kwamba Mungu
hangeendelea kuvumilia
ulimwengu huo uliojaa uasi.
Angewahukumu
watu wasiotii.
Bila shaka watu
hao wa siku za Enoko
hawakupenda
ujumbe aliotangaza.
Walimchukia sana
na huenda walijaribu kumuua.
Enoko alikufa bila kuona
unabii huo ukitimizwa.
Miaka mingine 600 ilipita
na kufikia wakati huo
hali duniani
ilikuwa mbaya zaidi.
Tusome Mwanzo 6:1-7.
“Sasa idadi ya
wanadamu ilipoanza
kuongezeka duniani,
nao wakazaa mabinti,
wana wa Mungu wa kweli
wakaanza kuona kwamba
mabinti wa wanadamu ni warembo.
Basi wakaanza kuwachukua
wote waliowachagua
ili wawe wake zao.
Ndipo Yehova akasema:
“Roho yangu haitamvumilia
mwanadamu daima,
kwa sababu
yeye ni mwili tu.
Kwa hiyo,
jumla ya siku zake
itakuwa miaka 120.”
Wanefili walikuwa duniani
siku hizo na baadaye.
Wakati huo
wana wa Mungu wa kweli
waliendelea kufanya ngono
na mabinti wa wanadamu,
nao wakawazalia wana.
Wana hao walikuwa
watu wenye nguvu
wa nyakati za kale,
wanaume maarufu.
Basi,
Yehova akaona kwamba
uovu wa mwanadamu
ulikuwa mkubwa duniani
na kwamba kila mwelekeo
wa mawazo ya moyo wake
ulikuwa mbaya
tu wakati wote.
Yehova akaghairi kwamba
aliwaumba wanadamu duniani,
na moyo wake ukahuzunika.
Kwa hiyo Yehova akasema:
Nitawafagilia mbali
kutoka duniani
wanadamu ambao
nimewaumba,
wanadamu pamoja na
wanyama wa kufugwa,
wanyama wanaotambaa,
na viumbe wanaoruka angani,
kwa sababu ninaghairi
kwamba niliwaumba.”
Wakati huo,
baadhi ya malaika
waliwaona mabinti wa wanadamu
kuwa ni warembo.
Hivyo, wakaanza kusitawisha
tamaa ya kufanya nao ngono.
Malaika hao walimwasi Mungu
kwa kuja duniani
na kuvaa miili ya kibinadamu
ili wafanye
ngono na wanawake.
Wakawa wabinafsi,
roho waovu.
Huenda walikuwa
wenye kuvutia,
wana akili nyingi,
watanashati,
na walikuwa na nguvu
zisizo za kawaida.
Lazima walikuwa
wenye kutamanisha
hasa kwa wanawake ambao
hawakumpenda Mungu.
Huenda malaika
hao waliwachukua
baadhi ya wanawake kwa lazima.
Vyovyote vile,
malaika waliwachukua
“wote waliowachagua.”
Hakuna mwanadamu
yeyote wakati huo
angeweza kuwazuia
roho hao waovu.
Kwa sababu ya
viumbe hao waovu
watu walipoteza binti zao,
dada zao,
na huenda,
hata wake zao.
Wanawake wakapata mimba,
wakazaa wana,
lakini wana hao walikuwa
tofauti na wavulana wengine.
Walikuwa na nguvu,
wanyanyasaji,
wenye hasira, na wakatili
na waliendelea
kuwa na sifa hizo
hata walipokuwa watu wazima.
Wavulana hao
wakawa wanaume
lakini wakawa
wakatili kupita kiasi.
Waliitwa Wanefili
huenda inamaanisha
wale wanaowaangusha
wengine chini
na watu waliwaogopa sana.
Kama baba zao,
Wanefili hawakumpenda Mungu.
Walitaka tu kujulikana
kuwa wenye
nguvu na wakatili.
Malaika hao waovu
na watoto wao
waliuongoza ulimwengu
na watu waliwaiga.
Yehova akaona
uovu wa mwanadamu
ulikuwa mkubwa
na kwamba kila mwelekeo
wa mawazo ya moyo wake
ulikuwa mbaya tu wakati wote.
Lazima Shetani
alifurahi sana
kuona wanadamu wengi zaidi
wakimkataa Yehova
na wapotovu zaidi na zaidi.
Lakini
kulikuwa na
mwanamume mwaminifu
katikati ya ulimwengu
huo uliopotoka.
Tusome kumhusu
kwenye Mwanzo 6:8.
Lakini Noa
akapata kibali
machoni pa Yehova.
Hii ndiyo historia ya Noa.
Noa alikuwa mtu mwadilifu.
Alijithibitisha mwenyewe
kuwa mtu asiye na kosa
miongoni mwa
watu wa siku zake.
Noa alitembea pamoja 
na Mungu wa kweli.
Baada ya muda,
Noa alizaa wana watatu,
Shemu, Hamu, na Yafethi.
Lakini dunia
ilikuwa imeharibika
machoni pa Mungu wa kweli,
nayo dunia ilikuwa
imejaa ukatili.
Naam, Mungu aliitazama dunia,
nayo ilikuwa imeharibika;
watu wote walikuwa
wameharibu njia yao duniani.
Baadhi ya watu leo
husema kwamba Noa
hakuwa mtu halisi
na simulizi la safina na gharika
ni hekaya tu au
hadithi ya kutungwa.
Lakini mwandishi
wa Biblia alijua
Noa alikuwa mtu halisi
na kwa hakika
gharika ilitokea.
Nabii Isaya na Ezekieli,
wote walimzungumzia Noa.
Ezra na Luka,
waandikaji wa vitabu vya Biblia
wote walimtaja Noa
kwenye historia ya
familia walizozitaja.
Mtume Petro na Paulo,
wote walithibitisha kwamba
gharika ilitokea.
Na kama tulivyotaja awali,
Mwana wa Mungu mwenyewe
alithibitisha
kwamba Noa
alikuwa mtu halisi
na gharika ilitokea.
Noa alikuwa na
imani yenye nguvu.
Aliishi kwenye ulimwengu mwovu
uliotawaliwa na malaika waovu
na watoto wao wakatili
na jamii isiyomwogopa Mungu.
Noa hakuwa na
vitu vilivyomsaidia
kuimarisha imani yake
kama tulivyonavyo leo.
Hakuwa na Biblia
ambayo ingemsaidia
kumpenda Yehova,
kuelewa njia zake.
Hakujua kwamba kungekuwa
na wanaume na wanawake
wengi waaminifu
ambao wangeishi baada yake.
Na Noa hakuwa na kutaniko
la waabudu wenzake
ambao wangemtia moyo
na kuimarisha imani yake.
Lakini kuna mambo
mengi ambayo alijua.
Alijua mambo yaliyotokea
katika bustani ya Edeni
na aliona matokeo
mabaya ya uasi.
Aliona watu
wakizeeka na kufa.
Alijua hakuna
mtu anayeruhusiwa
kuingia katika
bustani ya Edeni
na kwamba ardhi
ya nje ya bustani
ilikuwa imelaaniwa.
Alijua kuhusu unabii
ambao Enoko alitabiri.
Na Noa alijua
kwamba baba yake,
Lameki, alimpa jina
ambalo huenda linamaanisha
pumziko au faraja
kwa sababu kama
baba yake alivyotabiri,
“atatufariji katika
kazi yetu ngumu
na katika kazi
inayoumiza mikono yetu
kwa sababu ya ardhi
iliyolaaniwa na Yehova.”
Kwa kweli Noa alikuwa
na maswali mengi
kuhusu unabii huo.
Angewezaje kuleta faraja?
Ni wakati gani na jinsi gani
Mungu angetekeleza hukumu
dhidi ya waovu?
Kwa mamia ya miaka Noa
alijiuliza maswali hayo
na kusali.
Alipofikisha umri wa miaka 500
tayari alikuwa ameoa
na alikuwa na watoto watatu.
Ingawa aliishi katika
ulimwengu mwovu,
Noa aliendelea kuwa
mwaminifu kwa Mungu
na aliisaidia familia
yake iwe hivyo.
Kisha Yehova
akamjulisha Noa jambo fulani
lililomshangaza sana.
Tuendelee kusoma pamoja
Mwanzo 6:13
Baada ya hayo Mungu
akamwambia Noa:
“Nimeamua kuwaangamiza
wanadamu wote,
kwa sababu wameijaza
dunia ukatili,
kwa hiyo nitawaangamiza
pamoja na dunia.
Jitengenezee safina
kwa mbao za mti
wenye utomvu.
Utatengeneza vyumba
ndani ya safina
na uifunike kwa lami
ndani na nje.
Hivi ndivyo utakavyoitengeneza:
Safina inapaswa kuwa
na urefu wa mikono 300,
upana wa mikono 50,
na kimo cha mikono 30.
Utatengeneza
dirisha la kuingiza
mwangaza kwenye safina,
mkono mmoja kutoka juu.
Unapaswa kutengeneza
mlango ubavuni mwake,
na utengeneze ghorofa ya chini,
ghorofa ya pili,
na ghorofa ya tatu.
“Nami kwa upande wangu,
nitaleta gharika
ya maji duniani
ili kuangamiza viumbe wote
wenye pumzi ya uhai
walio chini ya mbingu.
Kila kitu kilicho
duniani kitaangamia.
Nami ninafanya pamoja
nawe agano langu,
nawe lazima uingie
ndani ya safina,
wewe, wanao, mke wako,
na wake wa wanao.
Nawe uingize
ndani ya safina
viumbe hai wawili
wawili wa kila aina
ili kuwahifadhi
hai pamoja nawe,
dume na jike;
viumbe wanaoruka angani
kulingana na aina zao,
wanyama wa kufugwa
kulingana na aina zao,
na wanyama
wote wanaotambaa
kulingana na aina zao,
watakuja ndani kwako viumbe
wawili wawili wa kila aina
ili uwahifadhi hai.
Nawe unapaswa kukusanya
na kuchukua kila
aina ya chakula,
kwa ajili yako na wanyama.”
Basi Noa akafanya
kulingana na mambo yote
ambayo Mungu
alikuwa amemwamuru.
Hivyo ndivyo alivyofanya
Kwa miaka mingi
Noa alijiuliza
Yehova angewatendea
nini watu wasiomtii?
Sasa alipata jibu.
Gharika kubwa
ingeusafisha ulimwengu.
Pia alijua kile
ambacho yeye
na familia yake
walipaswa kufanya,
uhai wa kila kitu
ulimtegemea yeye.
Lazima mawazo hayo
yalimlemea sana,
safina ingekuwa
kubwa sana!
Sasa alianza kujiuliza
maswali mengine.
Miti
angewezaje kukata miti mingi,
kisha atengeneze mbao
na kuziunganisha pamoja?
Angefanyaje hivyo?
Angewezaje kukusanya
wanyama wa aina mbalimbali?
Angewezaje kupata chakula
kwa ajili ya
wanyama wote hao
na família yake?
Na vipi kuhusu watu
waovu waliomzunguka,
wangefikiria nini?
Noa alijua
kilichowapata wanaume
waadilifu waliomtangulia.
Abeli aliuliwa
na ndugu yake, Kaini.
Na inaelekea Enoko
alikuwa kwenye hatari
ya kuuwawa na watu waovu
hivi kwamba Mungu aliamua
kukatisha uhai wake
ili asiangukie mikononi
mwa watu hao.
Watu waliona
Noa anafanya nini,
na hatimaye wangejua
kwa nini anafanya hivyo.
Inawezekana watu
wasiomheshimu Mungu
walioongozwa na Wanefili
wangemtendea kikatili.
Hata hivyo,
Noa alimtegemea Yehova
naye akaanza kazi.
Alifanya yote awezayo.
Familia ya Noa ilijenga
safina kwa muda mrefu,
labda miaka 40 au 50.
Lazima kulikuwa na changamoto
lakini Biblia haisemi
kwamba Noa alilalamika.
Hawakupata msaada
wa watu wengine.
Kumbuka kwamba Yesu
alisema watu hawakujali
mpaka gharika ikaja
na kuwafagilia mbali wote.
Bila shaka watu walijua
kwamba Noa anajenga safina.
Lazima majirani
zake walimuuliza
kwa nini anajenga
jengo kubwa hivyo
na Noa aliwaeleza
sababu za kulijenga.
Lakini watu walioishi siku za Noa
walipuuza ukweli kwamba
Mungu alimbariki Noa
na jitihada zake za ujenzi.
Hawakufikiria jinsi kazi
ya Noa ilivyowahusu.
Badala yake watu walifikiria
tu shughuli za kila siku
kula, kunywa, kuoa
hayo ndiyo mambo
waliyofikiria na kuyajali.
Watu hao walimwona
Noa na família yake
kuwa wajinga,
wamechanganyikiwa.
Waliwatukana, wakawadhihaki,
na inawezekana waliwatisha.
Hatimaye safina ilikamilika.
Unaweza kuwazia
Noa na família yake
wakiiangalia kwa fahari
na wakikumbuka jinsi
Yehova alivyowasaidia.
Sikuzote Yehova
huwapa mwongozo
watumishi wake wanapouhitaji.
Sasa,
Yehova anazungumza tena na Noa.
Tusome sura ya 7
kuanzia mstari wa 1.
Baada ya hayo Yehova
akamwambia Noa:
“Ingia ndani ya safina,
wewe pamoja na watu wote
wa nyumbani mwako,
kwa sababu nimekuona wewe
peke yako kuwa mwadilifu
mbele zangu miongoni
mwa kizazi hiki.
Ingia pamoja na wanyama
safi wa kila aina,
saba saba,
dume na jike;
na wanyama wawili tu wasio safi
wa kila aina,
dume na jike;
pia viumbe wanaoruka
angani saba saba,
dume na jike,
ili kuhifadhi hai uzao
wao duniani pote.
Kwa maana baada
ya siku saba tu,
nitafanya mvua inyeshe duniani
siku 40 mchana na usiku,
nami nitafagilia
mbali kutoka duniani
kila kiumbe kilicho
hai nilichokiumba.”
Basi Noa akafanya yote ambayo
Yehova alikuwa amemwamuru.
Hakukuwa na
muda wa kupoteza
walihitaji kufanya
kazi hiyo haraka.
Mvua ingeanza kunyesha
baada ya siku saba.
Wanyama wengi walihitaji
kuingizwa ndani ya safina.
Walihitaji kutunza vyakula.
Noa alisikiliza na kutii.
Kwa mara ya pili katika simulizi
hili lililoongozwa na roho,
tunaambiwa Noa
alifanya yote aliyoamriwa.
Sasa tusome Mwanzo 7:6:
Noa alikuwa na
umri wa miaka 600
maji ya gharika
yalipokuja duniani.
Kwa hiyo Noa,
pamoja na wanawe,
mke wake, na wake wa wanawe,
wakaingia ndani ya safina
kabla ya maji
ya gharika kuja.
Kila aina ya
mnyama aliye safi
na kila aina ya
mnyama asiye safi
na kila aina ya kiumbe
anayeruka angani
na kila aina ya kiumbe
anayetambaa ardhini,
wakaingia wawili wawili
na kumjia Noa ndani ya safina,
dume na jike,
kama Mungu alivyokuwa
amemwamuru Noa.
Na siku saba baadaye
maji ya gharika yakaja duniani.
Katika mwaka wa 600
wa maisha ya Noa,
mwezi wa pili,
siku ya 17 ya mwezi huo,
siku hiyo
chemchemi zote za
kilindi kikubwa cha maji
zilifunguka kwa nguvu
na malango ya mbinguni
ya mafuriko yakafunguliwa.
Na mvua ikamwagika
duniani kwa siku 40,
mchana na usiku.
Siku hiyohiyo,
Noa aliingia ndani ya safina
pamoja na wanawe,
Shemu, Hamu, na Yafethi,
pamoja na mke wake
na wake watatu wa wanawe.
Waliingia ndani pamoja
na kila mnyama wa mwituni
kulingana na aina yake,
na kila mnyama wa kufugwa
kulingana na aina yake,
na kila mnyama
anayetambaa duniani
kulingana na aina yake,
na kila kiumbe anayeruka
kulingana na aina yake,
kila ndege, kila kiumbe
mwenye mabawa.
Waliendelea kumjia
Noa ndani ya safina,
wawili wawili,
kila aina ya kiumbe
mwenye pumzi ya uhai.
Basi wakaingia ndani,
dume na jike,
viumbe wa kila aina,
kama Mungu alivyokuwa
amemwamuru.
Baada ya hayo
Yehova akaufunga mlango.
Gharika ikaendelea
kwa siku 40 duniani,
na maji yakazidi kuongezeka,
yakaanza kuibeba safina,
nayo safina ikaelea
juu sana duniani.
Maji yakafurika na kuzidi
kuongezeka sana duniani,
lakini safina ilielea juu ya maji.
Maji yalifurika sana
duniani hivi kwamba
milima yote mirefu chini
ya mbingu ikafunikwa.
Maji yalipanda kufikia
mikono 15 juu ya milima.
Basi viumbe wote walio hai
waliotembea duniani wakafa
viumbe wanaoruka,
wanyama wa kufugwa,
wanyama wa mwituni,
viumbe wanaoishi katika
makundi makubwa,
na wanadamu wote.
Kila kiumbe katika nchi kavu
aliyekuwa na pumzi ya uhai
katika mianzi ya pua yake akafa.
Basi Mungu akafagilia mbali
kila kiumbe hai kutoka duniani,
kutia ndani, wanadamu,
wanyama,
wanyama wanaotambaa,
na viumbe wanaoruka angani.
Wote walifagiliwa
mbali kutoka duniani;
ni Noa peke yake
na wale waliokuwa pamoja naye
ndani ya safina
waliookoka.
Na maji yakaendelea
kuifunika dunia
kwa siku 150.
Ikiwa Noa alijiuliza jinsi
ambavyo angewakusanya wanyama,
sasa alipata jibu.
Wangemfuata!
Yehova angewapeleka kwake.
Noa hakuhitaji
kwenda kuwatafuta,
wanyama walimfuata,
kila aina ya mnyama
wengine saba saba,
na wengine wawili wawili.
Wazia makundi
ya aina mbalimbali
ya wanyama wakitembea,
wakitambaa, wakirukaruka
kuelekea kwenye safina.
Tunaweza kuwazia
família ya Noa
ikiwatayarishia wanyama
mahali pa kukaa,
wakicheza na baadhi ya wanyama,
wakiwaepuka wanyama
wenye pembe zilizochongoka
na wenye ngozi zenye miiba,
na wakiwapisha wanyama
wakubwa ili waingie.
Ndege pia walikuja,
wakipigapiga mabawa, wakipaa.
Wazia rangi zao,
harufu, sauti.
Lazima Noa na família yake
walihitaji kuongea
kwa sauti kubwa
ili wasikilizane.
Wote walipoingia ndani,
Yehova akafunga mlango.
Jaribu kuwazia família hiyo,
wakiwa wameketi karibu karibu,
wakisikiliza mambo
yanayotokea nje.
Ghafla, mvua ikaja!
Labda ilianza
kama manyunyu
lakini hatimaye ikawa
mvua kubwa sana
na sauti yake ilikuwa kubwa.
Jambo walilikuwa wakitarajia
sasa linatokea.
Walikuwa wamechoka sana
lakini inawezekana
hawakupata usingizi usiku huo.
Kulikuwa na wanyama
wa kuangalia,
kelele za mvua,
na walisali sana.
Unafikiri walianza
kuwafikiria wale walio nje?
Bila shaka!
Waliwajua watu hao
na hata waliwahubiria.
Wengi walikuwa ndugu zao,
waliwahuzunikia sana.
Kama Yehova,
Noa hakufurahia
kifo cha mwovu.
Alihuzunika kuona
watu wengi wakifa.
Lakini alijua watu
hao walioangamizwa
walionywa mapema kuhusu
mambo ambayo yangetokea.
Hata ikiwa hawakuona safina
ambayo Noa
alikuwa akijenga,
walisikia kuihusu.
Walijua kwa nini
alikuwa akiijenga.
Lakini sasa
ilikuwa kuchelewa.
Yehova alikuwa
amefunga mlango.
Família ya Noa iliendelea
kusikiliza mvua
ikipiga safina bila kuacha.
Ukafika wakati ambao
hawangeweza kuusahau.
Safina ilianza kusogea!
Walianza kuhisi safina
hiyo kubwa ya mbao
ikiinuka kutoka ardhini.
Ilikuwa ikielea!
Mapigo yao ya moyo
yakaanza kwenda mbio.
Je, safina inaweza kuhimili?
Tusome Mwanzo sura ya 8
kuanzia mstari wa 1
ili tuone kilichotokea.
Lakini Mungu akamwelekezea
uangalifu Noa
na wanyama wote wa mwituni
na wanyama wa kufugwa
waliokuwa pamoja naye
ndani ya safina,
na Mungu akavumisha
upepo duniani,
maji yakaanza kupungua.
Chemchemi za kilindi cha maji
na malango ya mbinguni
ya mafuriko yakafungwa,
kwa hiyo
mvua kutoka mbinguni
ikaacha kunyesha.
Kisha maji yakaanza kupungua
hatua kwa hatua duniani.
Kufikia mwishoni
mwa siku 150,
maji yalikuwa
yamepungua sana.
Katika mwezi wa saba,
siku ya 17 ya mwezi huo,
safina ikatua kwenye
milima ya Ararati.
Na maji yakazidi kupungua
hatua kwa hatua
mpaka mwezi wa kumi.
Katika mwezi wa kumi,
siku ya kwanza ya mwezi huo,
vilele vya milima vikaonekana.
Basi mwishoni mwa siku 40,
Noa akafungua
dirisha la safina
alilokuwa ametengeneza
na kumtuma nje kunguru;
kunguru alikuwa
akienda na kurudi,
mpaka maji
yalipokauka duniani.
Baadaye akamtuma njiwa
ili aone ikiwa maji yalikuwa
yamepungua ardhini.
Njiwa huyo hakupata
mahali pa kutua,
kwa hiyo akarudi kwa Noa
ndani ya safina
kwa sababu maji
yalikuwa bado
yameifunika dunia yote.
Kwa hiyo akaunyoosha
mkono wake nje
na kumwingiza
ndani ya safina.
Noa akangojea
siku saba zaidi,
akamtuma tena
njiwa nje ya safina.
Njiwa huyo alipomrudia
Noa ikielekea jioni,
aliona kwamba alikuwa na jani
bichi la mzeituni
mdomoni mwake!
Basi Noa akajua kwamba maji
yalikuwa yamepungua duniani.
Akangojea tena
siku nyingine saba.
Kisha akamtuma
nje njiwa huyo,
lakini hakurudi tena.
Kwa siku 40
mchana na usiku,
kelele za mvua kubwa
zilikuwa zikisikika.
Kisha mvua ikaacha kunyesha.
Wazia Noa na família yake
wakichungulia nje ya safina
na kitu wanachoona ni maji tu.
Upepo ukavuma
na maji yakapungua.
Hatimaye,
siku 150 tangu
mvua ianze kunyesha
safina ikatua ardhini.
Ilikuwa siku ya
furaha sana kwao.
Lakini ilikuwa
salama kutoka nje?
Hapana,
maji yalihitaji
kupungua zaidi.
Bado família hiyo
ilikuwa na mambo
mengi ya kufanya.
Kulikuwa na wanyama wa
kuwalisha na kuwatunza.
Lakini
lazima walitamani
sana kutoka nje
wawe na uhuru
wa kutembea
tena kwenye ardhi.
Walihitaji kuwa na subira.
Wazia família hiyo
wakiwa wameketi pamoja,
wakipanga mambo
watakayofanya
watakapotoka nje ya safina.
Siku nyingine 73 zikapita.
Sasa wangeweza
kuona vilele vya milima.
Je, sasa ilikuwa
salama kutoka.
Noa alichungulia
nje ya dirisha.
Akamchagua kunguru
akamtoa nje
lakini kila mara
alirudi kwenye safina.
Noa akamwingiza ndani kunguru
kisha akamtoa njiwa.
Yeye pia aliruka
lakini akarudi
kwa sababu hakukuwa
na mahali pa kutua.
Baada ya juma moja
akamtoa tena nje
kisha akarudi na
jani la mzeituni
mdomoni mwake.
Siku saba baadaye
Noa akamtoa tena
lakini wakati huu hakurudi.
Kisha nini kilifuata?
Tuendelee kusoma
sura ya 8 mstari wa 13.
Sasa katika mwaka wa 601,
mwezi wa kwanza,
siku ya kwanza ya mwezi huo,
maji yalikuwa
yamepungua duniani;
Noa akaondoa
kifuniko cha safina
na kuona kwamba ardhi
ilikuwa ikikauka.
Katika mwezi wa pili,
siku ya 27 ya mwezi huo,
dunia ilikuwa imekauka.
Sasa Mungu
akamwambia Noa:
Toka ndani ya safina,
wewe, mke wako,
wanao, na wake zao.
Toka pamoja na viumbe wote
walio hai wa kila aina,
viumbe wanaoruka, wanyama,
na wanyama
wote wanaotambaa,
ili wazaane duniani
na kuongezeka na
kuwa wengi duniani.
Basi Noa akatoka nje,
pamoja na wanawe,
mke wake,
na wake wa wanawe.
Kila kiumbe aliye hai,
kila mnyama anayetambaa
na kila kiumbe anayeruka,
kila kiumbe anayetembea duniani,
akatoka ndani ya safina
kulingana na familia yake.
Kisha Noa akamjengea
Yehova madhabahu,
akachukua baadhi
ya wanyama walio safi
na baadhi ya viumbe
wanaoruka walio safi,
akawatoa kuwa
dhabihu za kuteketezwa
juu ya madhabahu hiyo.
Na Yehova akaanza kusikia
harufu ya kupendeza.
Kwa hiyo Yehova
akasema moyoni mwake:
Sitailaani ardhi tena
kwa sababu ya mwanadamu,
kwa maana mwelekeo wa
moyo wa mwanadamu
ni mbaya tangu
wakati wa ujana;
nami sitamwangamiza
tena kamwe
kila kiumbe aliye hai
kama nilivyofanya.
Kuanzia sasa na kuendelea,
dunia haitakosa kamwe
kuwa na majira ya
kupanda mbegu na kuvuna,
baridi na joto,
kiangazi na masika,
na mchana na usiku.
Njiwa alipokosa kurudi,
Noa aliondoa sehemu
ya paa la safina
na aliona sehemu
kubwa ya ardhi
ilikuwa imekauka.
Inawezekana aliona
mimea ikikua na kunawiri
tofauti na ilivyokuwa
kabla ya gharika
wakati dunia
ilipokuwa imelaaniwa.
Lakini Noa aliendelea kusubiri
mwongozo wa Yehova.
Kisha,
Yehova akatoa amri:
“Toka ndani ya safina.”
Hatimaye!
Lazima ilikuwa siku
ya furaha sana kwao.
Walikuwa kwenye
safina kwa siku 370.
Wazia família hiyo
wakitoka ndani ya safina,
wakicheka,
wakivuta hewa safi,
wakitazamia kwa hamu
kuanza maisha mapya.
Wanyama pia walitoka nje,
na família hiyo iliwaangalia
wakitawanyika kila mahali.
Huenda sasa
walihitaji kuwaaga
wanyama walioanzisha
urafiki nao.
Hakukuwa na wale
malaika waovu,
Wanefili, au
wanadamu waovu.
Walimshukuru sana Yehova.
Noa hakupoteza muda.
Alijenga madhabahu
na kutoa dhabihu kwa Yehova
na Mungu alifurahishwa nayo.
Na Yehova aliihakikishia
família hiyo kwamba
hataangamiza tena
kamwe kila kiumbe.
Lakini alifanya
zaidi ya hilo.
Alifanya agano na
Noa na watoto wake
na akawapa ishara
ambayo hata sisi
tunaweza kuiona.
Tusome kuihusu
kwenye Mwanzo
sura ya 9
kuanzia mstari wa 8.
Kisha Mungu akamwambia
Noa na wanawe:
Sasa ninafanya agano
langu pamoja nanyi
na pamoja na wazao
wenu baada yenu,
na pamoja na kila
kiumbe aliye hai
ambaye yupo
pamoja nanyi,
ndege, wanyama,
na viumbe wote walio hai
duniani pamoja nanyi,
wote waliotoka
ndani ya safina
kila kiumbe
aliye hai duniani.
Naam,
ninafanya agano
langu pamoja nanyi:
Viumbe wote
hawataangamizwa tena kamwe
kwa maji ya gharika,
na gharika haitaiharibu
dunia tena kamwe.
Na Mungu akaendelea kusema:
Hii ndiyo ishara ya agano
ninalofanya pamoja nanyi
na pamoja na
kila kiumbe hai
aliye pamoja nanyi,
kwa vizazi vyote vijavyo.
Ninauweka upinde wangu
wa mvua mawinguni,
nao utakuwa ishara ya agano
nililofanya na dunia.
Kila mara ninapoleta
mawingu juu ya dunia,
kwa hakika upinde wa mvua
utaonekana mawinguni.
Nami hakika nitakumbuka
agano langu
nililofanya pamoja nanyi
na pamoja na kila aina
ya kiumbe aliye hai;
na kamwe
hakutakuwa tena
na gharika ya maji
itakayowaangamiza viumbe wote.
Na upinde wa mvua
utatokea mawinguni,
nami hakika nitauona
na kukumbuka agano
la milele ambalo
mimi Mungu
nilifanya pamoja
na kila aina ya
kiumbe hai duniani.
Yehova aliwapa ishara
yenye kuvutia sana.
Kila mara upinde huo
unapotokea unamkumbusha Mungu
na wanadamu ahadi hiyo.
Lazima família ya Noa
ilistaajabishwa kuona
rangi hizo angani
zambarau, urujuani, bluu,
kijani, njano,
machungwa, na nyekundu.
Dunia haingekumbwa
tena na gharika.
Lakini Yehova
hatavumilia uovu milele.
Tusome kile ambacho
Mtume Petro aliandika.
Fungua 2 Petro 2:5.
Mtume huyo aliandika:
“Naye [Mungu]
hakujizuia kuuadhibu
ulimwengu wa kale,
bali alimlinda salama Noa,
mhubiri wa uadilifu,
pamoja na wengine
saba alipoleta gharika
juu ya ulimwengu wa watu
wasiomwogopa Mungu.”
Leo tunaishi katika ulimwengu
unaofanana na ule
wa kabla ya gharika.
Kuna jeuri
na watu wanafanya
mambo yote mabaya
ambayo Yehova anachukia.
Watu wanakazia fikira tu
mahangaiko ya kila siku
hata hawajali
ujumbe wa wokovu
ambao tunatangaza.
Wadhihaki wa watu wa Mungu
wanadhihaki kwa kusema:
“Kuko wapi huko kuwapo
kwake kulikoahidiwa?
Mambo yote
yanaendelea kama yalivyokuwa
tangu mwanzo wa uumbaji.”
Wanakosea sana!
Yehova alichukua hatua
dhidi ya uovu wakati wa Noa
na atachukua hatua sasa.
Kama Noa,
watu waaminifu wataokolewa.
Neno la Mungu linatuhakikishia:
“Yehova anajua
jinsi ya kuwakomboa
kutoka kwenye jaribu watu
wenye ujitoaji-kimungu,
lakini kuwaweka akiba
watu wasio waadilifu
ili waangamizwe
katika siku ya hukumu.”
Yehova ataifanya
dunia kuwa paradiso
kama alivyokusudia
mwanzoni.
Watu wazuri ndio
watakaoirithi paradiso.
Hakutakuwa na watu
wanaomwasi Mungu.
Namna gani viumbe
wa kiroho walioasi?
Gharika ilipokuja
katika siku za Noa,
malaika waasi walivua
miili ya kibinadamu
na kurudi mbinguni
kwa aibu.
Hata hivyo roho
hao waovu
wanaendelea
kuwaongoza vibaya
wanadamu mpaka leo hii.
Lakini Yehova
atakapochukua hatua tena,
roho waovu
na mtawala wao Shetani
wataangamizwa kabisa.
Neno la Mungu
linasema hivi:
“Kwa imani,
Noa baada ya
kuonywa na Mungu
kuhusu mambo ambayo bado
hayakuwa yameonekana,
alimtii Mungu
kwa kujenga safina
kwa ajili ya kuiokoa
nyumba yake.”
Imani ilimchochea Noa
kumtii Yehova.
Hivyo,
yeye na família yake
waliokoka gharika.
Noa aliishi
kwa muda mrefu
miaka 950.
Lakini mwanamume
huyo mwaminifu
atakapofufuliwa
atakuwa na nafasi
ya kuishi milele.
Ikiwa tutaonyesha
imani kama ya Noa
na kumtii Yehova,
tunaweza kutembea
na rafiki yetu Yehova,
na urafiki huo
utadumu milele!