JW subtitle extractor

Nehemia: “Shangwe ya Yehova Ndiyo Ngome Yenu”—Sehemu ya 1

Video Other languages Share text Share link Show times

Kama tulivyojifunza katika
drama ya kusikiliza,
Wayahudi walirudi Yerusalemu
kujenga upya hekalu
katika mwaka wa 537 K.W.K.
Kufikia 515 K.W.K.,
lilikuwa limekamilishwa.
Hata hivyo, kuta za jiji
bado zilikuwa magofu.
Sasa wakati wa Yehova ulikuwa umefika
wa kujenga upya kuta hizo,
naye alimtumia mwanamume mwaminifu
aliyeitwa Nehemia
kuongoza kazi hiyo.
Hiyo ingekuwa kazi kubwa kwa Wayahudi.
Na kwa mara nyingine
kungekuwa na wapinzani.
Nehemia aliliambia taifa la Israeli
“shangwe ya Yehova ndiyo ngome yenu.”
Angewezaje kuwatia moyo
wawe wenye shangwe
licha ya upinzani wote waliokabili?
Mfano wao unaweza
kutufunza masomo gani?
Masomo mengi,
lakini fikiria haya matatu unapotazama:
Sala ilitimiza fungu gani
kumsaidia Nehemia
kuwa jasiri anapomtegemea Yehova?
Mbali na mashambulizi
ya moja kwa moja,
ni hila zipi ambazo maadui walijaribu
kutumia kupinga kazi hiyo?
Na licha ya changamoto,
ni nini kilichokuwa chanzo kikuu
cha shangwe ya Nehemia?
Uko tayari?
Sawa basi,
kumbuka mambo hayo.
Sasa
acheni tufurahie
kutazama video yenye kichwa
“Shangwe ya Yehova Ndiyo Ngome Yenu.”
Lilikuwa pendeleo kubwa kwangu
kushiriki katika kazi ya kurudisha
ibada ya Yehova.
Watu wanajua kwamba tulijenga upya
kuta za Yerusalemu,
lakini kuna mambo mengi
ambayo hawajui.
Acheni nianzie mwanzo.
Katika mwaka wa 20
wa Mfalme Artashasta Longimano,
nilikuwa katika makao ya mfalme
huko Shushani.
Nilikuwa msimamizi
wa vinywaji vya mfalme.
Aliniamini kabisa
kwa kuwa uhai wake
ulikuwa mikononi mwangu.
Ingawa nilikuwa mbali na Yerusalemu,
nilipata shangwe kubwa kufikiria
kuhusu watu wetu waliokuwa huko
wakimtumikia Yehova.
Lakini mambo yalibadilika siku moja
nilipotembelewa na ndugu yangu Hanani.
Kuna nini Hanani?
Watu wetu wakoje?
Mambo si mazuri.
Hali ya huko
ni mbaya sana.
Kuta za Yerusalemu
zimebomolewa,
na malango yake
yameteketezwa kwa moto.
Vipi kuhusu hekalu?
Hekalu lipo,
lakini dhabihu zinatolewa kidesturi tu.
Watu wengi na hata makuhani
wanapuuza Sheria ya Mungu.
Njoo twende Yerusalemu pamoja.
Dhamiri yangu ilinisumbua kwa siku nyingi
nilipofikiria hali hiyo.
Je, mfalme ataniruhusu niende?
Watu wetu walikuwa wametenda dhambi
kwa kutotii amri za Yehova,
lakini sasa nilihisi
mimi ndiye ninayetenda dhambi
kwa kutowasaidia.
Nilimwomba Yehova anisaidie nifanikiwe.
Nehemia,
kwa nini una huzuni
wakati wewe si mgonjwa?
Lazima uwe una huzuni moyoni.
Kwa nini nisiwe na huzuni
wakati lile jiji,
mahali ambapo
mababu zangu wamezikwa
ni magofu,
na malango yake yameteketezwa
kwa moto?
Nehemia,
Unasema nini?
Nieleze unachotaka.
Usinifiche chochote.
Mara moja nikasali
kwa Mungu wa mbinguni.
Ukipenda, Ee mfalme,
na ikiwa mimi mtumishi wako
nimepata kibali chako,
niruhusu niende Yuda,
kwenye jiji ambalo
mababu zangu wamezikwa
ili nilijenge upya.
Unaweza kwenda.
Yehova alikuwa pamoja nasi.
Mfalme alinipa mahitaji yangu,
jeshi,
na akaniweka rasmi kuwa gavana.
Tulikuwa tukisafiri kwenda Yerusalemu
kujenga upya kuta zake.
Nilikuwa nimeona sehemu fulani tu ya jiji,
lakini haikuwa hadi usiku
nilipoamka kukagua kuta,
ndipo nilipoona jinsi
jiji la Mungu lilivyokuwa limeharibiwa.
Subirini hapa.
Nilishangaa kuona jinsi
kuta zilivyokuwa zimeharibika sana.
Wakati ulikuwa umefika
wa kuwafunulia watu kusudi la Yehova
kuelekea Yerusalemu.
Kwa hiyo, nikawakusanya viongozi.
Mwanamume huyu ni nani?
Nimesikia anaitwa Nehemia,
msimamizi wa vinywaji vya mfalme.
Kwa nini ametuita hapa?
Wanaume!
Jiji takatifu
halina ulinzi wowote.
Acheni tujenge upya kuta za Yerusalemu,
ili tusiendelee kuaibishwa kwa njia hii.
Majirani wetu watasemaje?
Tuna maadui wengi wenye nguvu.
Artashasta ndiye aliyeniagiza
kujenga upya kuta hizi na jiji lote.
Kwani hamkuwaona wapanda farasi wake?
Na mbao nilizokuja nazo?
Vyote hivyo vimetoka kwake.
Ndugu zangu,
mkono mwema wa Mungu wetu
uko juu yangu.
Tumwogope yeye,
si wanadamu.
Yeye atafanikisha kazi yetu!
Si wote waliofurahi
kwamba tulikuwa tumekuja
kuwafanyia Waisraeli mambo mema.
Kwa hiyo, hilo ndilo jambo
ambalo Nehemia anapanga.
Geshemu,
hali hii itatuletea matatizo?
Bila kuta,
tunaweza kuwadhibiti Wayahudi.
Wakizijenga upya,
hawatahitaji chakula wala mali zetu.
Inamaanisha anapanga kuasi.
Hatutamruhusu,
tunapaswa kutenda,
tusimame pamoja.
tuko pamoja?
Mimi nakuunga mkono.
Mimi pia,
kama kawaida.
Sawa!
Lazima twende Yerusalemu
tuone Nehemia anapanga kufanya nini.
Wapinzani walitaka kudhibiti mambo
na kufaidika kutoka kwa watu wa Yehova.
Mara moja wakaanza kujaribu kututisha.
Wale ni nani?
Yule ni Sanbalati;
gavana wa Samaria.
Kando yake ni Tobia,
ofisa Mwamoni,
anamiliki ardhi ambamo
watu wengi wanaishi.
Na wanamheshimu sana.
Na yule ni Geshemu;
Mwarabu tajiri
na rafiki wa karibu wa Sanbalati.
Nehemia,
unamwasi mfalme wa Uajemi?
Mfalme ndiye ametupa mamlaka.
Ya kujenga upya jiji na kuta zake?
Mfalme anatarajia tujenge upya
jiji hili na kuta zake.
Kwa nini basi hukunipasha habari?
Mimi ndiye gavana wa Samaria.
Ni sawa,
lakini mfalme alimweka Nehemia
kuwa gavana wa Yuda.
Basi kwa nini hamjatuomba msaada?
Sisi pia tunamwabudu Yehova.
Tumemtolea dhabihu kwa miaka mingi.
Pamoja na kutoa dhabihu
kwa miungu mingine mingi.
Mungu wa mbinguni,
ndiye atakayetufanikisha,
nasi watumishi wake
tutasimama na kujenga.
Hakuna mtu anayepaswa
kuruhusu imani yake
ivuruge umoja wa taifa.
Hamna fungu wala haki,
wala kumbukumbu katika Yerusalemu.
Sanbalati,
huoni kwamba ni wewe
unayemwasi Mfalme mkuu kuliko wote?
Licha ya upinzani
-watu waliendelea kufanya kazi kwa bidii.
-Nehemia,
unaonaje tukihamisha yale?
Walikabili hali ngumu
mbali tu na kujenga kuta.
Yehova anawakumbuka
ndugu kama vile Pelethi.
Nilipomwona akishughulikia
matatizo yake mwenyewe,
imani yangu iliimarika.
Pelethi.
Rahamu.
Hii kazi haitaisha.
Huu ukuta ni rundo la mawe tu.
Lakini angalau tunajaribu kufanya kitu.
Siku zote unatarajia mema tu.
Na kwanza, umechelewa tena kunilipa kodi
ama umesahau?
Rahamu,
samahani;
ninahitaji muda zaidi.
-Kwa sababu ya kazi hii ya ujenzi, . . .
-Aah!
Nina shida zangu mwenyewe.
Usiponilipa kufikia mwisho wa mwezi
wewe na familia yako mhame.
Hakuna mpango tunaoweza kufanya?
Ninaweza kukufanyia kazi
-halafu ufute kodi yetu.
-Acha mzaha!
huna wakati wa kunifanyia kazi,
binti yako anaweza kusaidia.
Anaweza kuja kuishi nasi.
-Eti awe mtumwa?
-Hapana
atamsaidia mke wangu Azuba,
ili kulipia deni lako.
Najaribu tu kukusaidia,
kwa sababu sioni ikiwa una njia nyingine.
Fikiria,
halafu utanijulisha.
Eeh.
Rahamu alinitafuta leo.
Anatakaje?
Anataka kumwajiri Simka
amsaidia Azuba kazi za nyumba.
Anasema atamtunza
kama binti yake mwenyewe.
Aaah,
Ima,
nimewafahamu Rahamu na Azuba
tangu tuliporudi na Ezra.
Rahamu alitusaidia.
Nyumba yetu ni mali yake.
Mimi simwamini.
Eti anataka binti yetu
akaishi kwake?
Ima, . . .
Vipi kuhusu amri ya Yehova
kwamba wazazi walee
watoto wao wenyewe?
Kwani hutaki awe na maisha mazuri?
Mimi
siwezi
kukubali aishi mbali na sisi,
hata ikiwa lazima
tuendelee kukusanya masalio.
Unajuaje ikiwa masalio yatatutosha?
Kwa sababu Yehova huwatunza
wale wanaompenda na kumtii.
Wanaume kama Pelethi
walimtupia Yehova mzigo wao
na kuendelea kufanya kazi.
Sanbalati alipiga kambi
karibu na Yerusalemu
ili kuangalia maendeleo ya kazi yetu.
Kwa hiyo,
kuna nini?
Bwanangu.
Sema?
Kimo cha ukuta
kimefikia nusu kuzunguka jiji lote.
Sasa,
tumewaachilia sana!
Geshemu,
itakuchukua muda gani
kukusanya kikosi cha jeshi?
Kikosi cha jeshi?
Bwanangu, Sanbalati,
kuwashambulia Wayahudi
ni kumshambulia mfalme.
-Unajaribu kumaanisha nini?
-Ni kweli.
Nehemia amepewa mamlaka
na mfalme wa Uajemi mwenyewe.
Uliona mfalme alimtuma
na wapanda farasi wangapi?
Ungesema tuwashambulie
ikiwa bado wapanda farasi
hao wangekuwepo?
Na mfalme anaweza kuwarudisha.
Huo ni upuuzi!
Iwe kuna wapanda farasi au la.
Huu ni mkoa wangu!
Tukiwa hapa,
mimi ndiye mwamuzi.
Tunahitaji kuwatisha Wayahudi.
Geshemu,
wewe kawalete wanajeshi Wasamaria
mwingie upande huu.
Wanapanga kutushambulia!
Unajuaje watatushambulia?
Niliwasikia wakizungumza.
Ndugu zangu
tulieni.
Wamemshambulia mtu yeyote?
Lazima.
Kuna kitu alichoona.
Unataka kusubiri
hadi watakapoanza kutuua?
Hapana.
Sijasema hivyo!
Hanani,
wapange wanaume kwa kutegemea familia,
mahali ambapo ukuta umebomoka.
Sawa Nehemia.
Hiyo ni kazi bure.
Ndugu zangu,
vitisho vyao
vikituogopesha kuacha kazi,
watakuwa wamefaulu.
Tuache tu.
Kwani huoni?
Hawafurahishwi na tunachofanya.
Wanatuchukia.
Na wewe huishi na
kufanya kazi karibu nao kama sisi.
Ndugu zangu,
imani yenu iko wapi?
Ni mapenzi ya Yehova
tujenge ukuta huu.
Ikiwa ni mapenzi yake,
kwa nini tunakabili upinzani?
Huenda wakati wa kujenga haujafika.
Na pia hii kazi ni kubwa mno kwetu.
Tumechoka kabisa.
Kwani ukuta wenyewe hata ni wa nini?!
Ni wa kuwalinda watu wa Yehova.
Ndugu zangu.
Msiwaogope
watu hawa.
Mkumbukeni Yehova,
ambaye ni mkuu
na mwenye kutisha sana.
Na mwapiganie ndugu zenu,
mwapiganie wana na binti zenu,
wake zenu na nyumba zenu.
Mtakaposikia sauti ya pembe
jikusanyeni mahali tutakapokuwa.
Mungu wetu atatupigania.
Isubirini ishara.
Vitisho vyetu havifanyi kazi.
Sauti inayofuata watakayosikia
ni kishindo chetu cha vita.
Subiri,
Tulishazungumzia hili.
Kuwashambulia moja kwa moja
ni kumwasi mfalme.
Isitoshe wao pia wana silaha.
Jamani!
Bwanangu,
Geshemu hajakosea.
Tukithubutu,
mfalme atatuadhibu.
Umesahau ni nani aliyemwagiza Nehemia?
Ni mfalme.
Mfalme wa Uajemi mwenyewe.
Nehemia anajaribu
kujifanya kuwa mfalme.
Mimi napendekeza
tumshtaki Nehemia kuwa mwasi
na mhaini.
Hiyo ni mbinu yenye akili!
Ndiyo,
atatusihi tumsaidie.
Acheni turudi Samaria.
Hanani,
inaonekana umekuwa ukichapa kazi.
Lazima ninanuka sana.
Ndiyo!
Kweli unanuka sana.
Ndugu zangu!
Tuko karibu sana kumaliza kujenga kuta.
Yehova anatusaidia.
Lakini tusiruhusu mikono yetu ilegee.
Kuanzia sasa,
sote tutalala Yerusalemu.
Tutapeana zamu za kulinda.
Hanani atapanga migawo hiyo.
Muwe na siku njema.
Kila mtu alikuwa akifanya kazi
kwa bidii kujenga ukuta.
Lakini tulikuwa na changamoto nyingine.
Ndugu zangu,
mngependa niwasaidieje?
Nehemia,
sisi na wana wetu na binti zetu,
ni wengi.
Tunahitaji chakula ili tuishi.
Tulitoa mashamba yetu
na mizabibu
na nyumba zetu
kuwa rehani
ili tupate nafaka wakati wa njaa.
Tuliweka rehani
mashamba yetu na mizabibu
ili kulipa ushuru wa mfalme.
Na tulilazimika kuwauza watoto wetu
kuwa watumwa.
Hatuna uwezo wa kuzuia jambo hili
kwa sababu mashamba yetu
yamechukuliwa na wengine.
Asanteni kwa kunijulisha.
Lazima nitafakari mliyonieleza.
-Asante sana.
-Asante Nehemia.
Hanani,
tafadhali waambie wakuu
na watawala wasaidizi
waje kwangu kesho asubuhi.
Kwa msaada wa Mungu
tutarekebisha tatizo hili.
Wanaume wa Yuda,
kila mmoja wenu anamtoza riba
ndugu yake mwenyewe.
Jambo mnalofanya si jema.
Je, hampaswi kutembea
kwa kumwogopa Mungu wetu,
ili mataifa,
maadui wetu
wasitushutumu?
Tafadhali
tuache kukopesha kwa riba.
Tafadhali warudishieni mashamba yao,
mashamba ya mizabibu,
mizeituni,
na nyumba zao
na pia riba.
Nehemia,
nitawarudishia mashamba
leo,
jua linapotua.
Sisi sote tutawarudishia
ndugu zetu vitu hivyo.
Mbele za Yehova,
je, mnaapa kutimiza ahadi hizo?
Tunaapa!
Yehova na amkungu’te
kutoka nyumbani kwake
mwanamume yeyote ambaye
hatatimiza ahadi hii.
Amina!
Meshulamu,
lazima tumjulishe Tobia
kuhusu jambo hili.
Jambo hili litafanikiwa.
Yehova atalibariki.
Rahamu!
Nina habari njema.
Eti eh?
Ndiyo!
Tuna kodi yako.
Ala?
Pitia wakati wowote uichukue.
Nilifikiri tuli—
Vipi kumhusu Simka?
Atabaki nasi.
Ulifauluje kuikusanya upesi hivi?
Yehova huwatunza wale wanaompenda
na kumtii.
Tangu Nehemia aliporudi,
hali zimezidi kuwa nzuri.
Nehemia anafikiri bado sisi ni vijana
kama tuliporudi na Ezra.
Nilifanya kazi kwa bidii.
Lakini Nehemia anafanya ionekane
kama kila kitu kilianguka kutoka mbinguni.
Nilifanyia kazi mali zangu, sivyo?
Ndiyo, umefanya kazi.
Nikirudisha mashamba yangu,
nitakula nini?
Nitakunywa nini?
Kuna ubaya gani kukopesha kwa riba?
Ukikopa,
lipa na riba.
Rahamu,
Yehova anataka tuwe
tukiwatendea ndugu zetu kwa haki.
Hujasikia nilichosema?
Mimi huwatendea wote kwa haki!
Basi kwa nini umekasirika?
Sijakasirika!
Kwa nini unaniongelesha hivyo?
Nahisi tu nimesalitiwa.
Na nani?
Na watu ambao nimewakopesha pesa!
Sasa mimi nikusaidieje?
Fanya kile mke anachopaswa kufanya!
Nizalie mwana!
Ikiwa si mwana zaa binti.
Siwezi kukupa kile ambacho
Yehova hajatupatia.
Siku moja,
muda wako utakwisha.
Tumwandikie mfalme barua.
Tusubiri tuone kijana
ataripoti nini anaporudi.
Bwanangu, Sanbalati.
Nini tena?
Ukuta wameziba mianya yote.
Eti unasemaje?
Wamefauluje kufanya kazi hiyo
upesi hivyo?
Pia hii ni barua ya Tobia.
Nehemia
anawalazimisha watu warudishe
mashamba kwa walioimiliki awali.
Tunapaswa kutenda haraka.
Imetosha!
Nenda umwambie Nehemia:
“Njoo,
tupange wakati
ili tukutane kwenye vijiji
vya Bonde Tambarare la Ono.”
Ni mbinu ya kunitoa nje ya Yerusalemu.
Nenda kamwambie bwanako:
“Ninafanya kazi kubwa sana,
siwezi kushuka chini.
Kwa nini kazi isimame ili nije kwenu?”
Walinitumia ujumbe huohuo mara kadhaa.
Kila mara,
niliwapa jibu lilelile.
Bwanangu,
kwa mara ya nne amekataa ombi lako.
Geshemu,
wakati umefika wa kutumia mbinu yako.
Tobia,
andika maneno haya
“Kuna habari zinazoenezwa katika mataifa,
na Geshemu anasema pia
kwamba wewe
na Wayahudi
mnapanga kuasi.
Hii ndiyo sababu unajenga ukuta.”
Naam
Mpe Nehemia barua hii.
Mwambie bwanako:
“Hakuna jambo lolote unalosema
ambalo limetendeka;
umeyabuni wewe mwenyewe.”
Ni vitisho.
Wanajaribu kutuogopesha tuache kazi.
Kweli,
wanajua mfalme hawezi
kubadili agizo lake.
Lakini ukweli ni kwamba
hawatatuacha.
Yehova,
itie nguvu
mikono yangu.
Tufanye nini ili tumzuie?
Muda wetu unazidi kwisha.
Ukuta unakaribia kukamilika.
Sanbalati,
Nafikiri ninajua njia.
Shemaya,
ulitaka kuniona.
Ndiyo Nehemia!
Ingieni ndani upesi.
Uhai wenu uko hatarini
na wangu pia
kwa sababu najua kuhusu njama hii.
Ongea mambo yanayoeleweka.
Wanakuja kukuua.
Watakuja usiku,
tunapaswa kuingia ndani ya hekalu
na tufunge milango.
Shemaya,
je, mtu kama mimi anapaswa kukimbia?
Naona huelewi.
Hapana,
kufanya hivyo kutaathiri
ujasiri wa taifa lote?
Hapo tu ndipo utakuwa salama.
Na usisahau
mimi si kuhani.
Nikiingia hekaluni,
ninastahili kufa,
kwa hiyo,
sitaingia.
Huo ni uamuzi wa kipumbavu Nehemia.
Sasa nimeelewa!
Tobia na Sanbalati
walikutuma uje kuniambia maneno hayo,
sivyo?
Mnafiki.
Yehova na awakumbuke wao.
Na akukumbuke
wewe na manabii wenzako wa uwongo
wanaojaribu kuniogopesha.
Tuondoke Hanani,
tuna kazi ya kufanya.
Aah!
Tuliendelea tu
kufanya kazi usiku na mchana.
Na bila kujua
tulikuwa tukimaliza
sehemu ya mwisho kabisa ya ukuta.
Yehova alituwezesha
kutimiza kile ambacho
kilionekana hakiwezekani.
Ingawa tulikuwa tumechoka,
tulipata kitu ambacho tulikuwa tumepoteza
shangwe.
Nehemia,
ukuta umekamilika!
Tumefaulu.
Ndani ya siku 52.
Bwanangu,
ujumbe kutoka kwa Shemaya.
Unasemaje?
Eti ukuta umekamilika?
Heh!
Wamebakisha tu kuweka milango?
Tunapaswa kutenda upesi.
-Sanbalati . . .
-Acha!
Tobia.
Bado tuna muda.
-Mwandikie mfalme barua.
-Tobia,
kwani huoni?
Inaonekana Mungu anawasaidia Wayahudi.
Hatuna la kufanya.
Sasa tutashindwa kuwadhibiti.
Bado hatujashindwa.
Kujenga upya kuta
kulikuwa mwanzo tu.
Tungehitaji msaada wa Mungu
ili kukabiliana na kilichokuwa kikifuata.