JW subtitle extractor

Nehemia: “Shangwe ya Yehova Ndiyo Ngome Yenu”—Sehemu ya 2

Video Other languages Share text Share link Show times

Ulikuwa mwezi wa Tishri,
mwanzo wa sherehe ambayo
ingeendelea kwa mwezi mzima.
Tulikuwa tumemaliza kujenga upya
ukuta wa jiji kuu la Yehova.
Sasa wakati ulikuwa umefika
wa kujenga upya hali ya kiroho
ya watu wake waliochaguliwa.
Wengi wao hawakujua Sheria ya Mungu.
Na mtu ambaye angetusaidia
kupata uelewaji huu ni
mwanamume aliyekuwa amerudi
Yerusalemu kabla yangu
Ezra.
. . . masharti na sheria za Yehova.
Yeye na Walawi wengine walisoma kwa sauti
maneno ya Sheria ya Mungu.
-Tafakari kumhusu Mungu
-Na hawakuisoma tu,
-umpende na kumtii Yehova.
-bali waliifafanua waziwazi.
na kueleza maana yake.
Sisi sote,
tulianza kuelewa tulikuwa
tumemhuzunisha Yehova kwa kadiri gani,
Kwa kufanya kazi siku ya Sabato,
kwa kutoa dhabihu za wanyama
walio vilema,
na kuwataliki wake zetu
ili kuoa wanawake wa kigeni.
Ingawa mioyo yetu iliumia,
kwa kusoma sheria ya Mungu,
tulikuwa tukijifunza
kuwa watu wa Yehova tena.
Msiomboleze wala kulia.
Sasa kwa kuwa mnajua
kinachomchukiza Mungu,
mnaweza kufanya kinachompendeza.
Nendeni.
Mkale vitu bora,
na kunywa vitu vitamu,
na mwape chakula wale ambao hawana.
nanyi msihuzunike,
kwa maana shangwe ya Yehova
ndiyo ngome yenu.
Tulifuata maagizo ya Yehova
tuliposherehekea sherehe ya vibanda.
Kwa siku nyingi tulikuwa na shangwe
na tukamshukuru
Yehova kwa baraka zake.
Kisha kwenye siku ya 24,
tulikusanyika ili kusoma sheria ya Mungu,
kutubu dhambi zetu,
na kuomboleza kwa sababu ya makosa yetu.
Tulifanya mapatano thabiti kwa maandishi.
Tuliazimia kutii sheria ya Yehova.
Amina!
Amina!
Lakini
upesi wengine wakasahau ahadi yao.
Pelethi!
Rahamu,
ndio hii kodi yetu.
Niingizie ndani ya mfuko.
Ni vigumu kubeba kikapu.
Umesikia kuhusu wazo jipya la Nehemia?
Unamaanisha mpango wa watu
kuhamia Yerusalemu?
Namaanisha wazo lake la ajabu
la kulazimisha familia zirudi ndani ya jiji
familia 1 kati ya 10.
Ndiyo, nimesikia.
Sielewi nimechaguliwaje.
Kwa nini nichaguliwe?
Hajali jinsi sisi
tunaomiliki mashamba tunavyoathiriwa?
Oh!
Wewe unapaswa kuhama lini?
Eti nihame?
Mimi sihami.
Nina haki ya kuishi ninapotaka,
nawe pia.
Mimi sikuchaguliwa.
Utachaguliwa tu.
Na wakati huu unapaswa
kujiunga na mimi kukataa kuhama.
Rahamu,
mfalme alimtuma Nehemia hapa
kujenga upya jiji.
Nehemia ndiye gavana.
Magavana huja
nao huondoka.
Mfalme anamsubiri Nehemia arudi,
na atakaporudi,
hali zitabadilika.
Hata Nehemia atakapoondoka,
Yehova bado atakuwa hapa.
Na ni mapenzi yake
Yerusalemu lijengwe upya,
wewe huamini hilo?
Kwa hiyo utamuunga mkono Nehemia?
Unawezaje kunisaliti hivyo?
Rahamu,
kodi yako!
Wewe na Rahamu
mlikuwa mnazungumzia nini?
Rahamu anagoma kuhamia Yerusalemu
na anataka tumuunge mkono.
Ulimwambia nini?
Nilimwambia,
Nehemia anafanya mapenzi ya Yehova.
Rahamu haelewi
jinsi anavyoweza kuwa na furaha,
ikiwa tu angefuata mwongozo wa Yehova.
Kwa hiyo,
sisi tutahama tukichaguliwa?
Ndiyo.
Afadhali niwe kama Nehemia
kuliko Rahamu,
unakubaliana nami?
Ndiyo.
Mimi pia.
Wakati wa kuzindua kuta,
tulijaza Yerusalemu nyimbo za kumsifu
na kumshukuru Mungu.
Shangwe yetu kubwa ingeweza kusikika
kutoka mbali sana.
Niliendelea kufikiria kuhusu siku hiyo
hata baada ya kurudi Uajemi.
Lakini yaliyofuata yalinionyesha
laiti nisingaliondoka.
Yehova alimtokeza
mjumbe ambaye aliandika
mambo yaliyotokea Yerusalemu
baada ya mimi kuondoka.
Aliitwa Malaki.
Tobia,
ambaye hakuwa Myahudi,
alipata chumba katika hekalu.
Tobia,
-Alitumia watu wake wa ukoo
-na uwe na amani.
-waliokuwa Wayahudi
-Na uwe na amani pia.
kujifaidi mwenyewe.
Nini kimekuleta hekaluni
baada ya muda mrefu?
Nilitaka tu kukusalimu,
oh, na kukuletea zawadi hii ndogo.
Tobia,
wewe ni mkarimu sana.
Ni kitu kidogo tu.
Kwa hiyo,
kuna chochote ninachoweza kukufanyia?
Kwa kuwa umeuliza,
eeh, nina ombi moja dogo tu.
Niambie,
ungependa nikufanyie nini?
Eeh, kwa kuwa sisi ni familia moja . . .
Watu wetu wa ukoo
wanapotutembelea kutoka Samaria,
ingependeza sana ikiwa
tungekuwa na mahali pa kula pamoja.
-Mmh
-Hapa hapa ndani ya hekalu.
Isitoshe, nao wanamwabudu Yehova pia.
mara nyingi.
Au tuseme mara chache.
Eti chumba ndani ya hekalu?
Unajua siwezi kufanya hivyo,
yaani vyumba vyote vinatumika.
Eti vyote vinatumika?
Si vingine ni vya kuhifadhia vitu tu?
Hayo ni maandalizi ya Walawi.
Huwezi kuyahamisha nipate kimoja?
Kimoja tu?
Ninahitaji kimoja tu.
Lakini Nehemia atasema nini?
Nani anajali atasema nini?
Nehemia alisharudi kule Shushani.
Lakini vipi akijua?
Nani atamwambia?
Unapanga kumwambia?
La,
-la!
-Basi,
kwa nini uwe na hofu?
Kwa hiyo kwa mara nyingine tena
kuhani mkuu amefanya kile Tobia anataka.
Niweke wapi hizi nafaka?
Kuna nafasi hapa.
-Uwe mwangalifu!
-Sawa, asante.
Angalia nani anakuja.
Mnaweza kuharakisha?
Wakishaondoka,
tutaweka meza hapa.
Halafu,
vitu tutavipanga ukutani.
Tobia,
hebu nieleze,
unafikiri tutahifadhia wapi vitu vyetu?
Popote tu.
Hiyo si shida yangu.
Sasa, tafadhali ondokeni.
Ondoeni hilo gari.
Ondokeni.
Kwa hiyo, tutashushia hapa,
kisha kama nilivyosema,
viti pale, meza hapo,
halafu chakula.
Eliashibu angewezaje kumruhusu yeyote,
acha tu Tobia
ajichukulie chumba
kwa matumizi yake mwenyewe.
Baada ya kazi yote ya Nehemia
ya kurudisha utakatifu wa hekalu?
Lakini kikweli watu wengi
walishaacha kutoa sehemu ya kumi.
Ikiwa tunataka kula
tunapaswa kwenda
kuchunga mifugo yetu na kulima.
Hakuna faida kumtumikia Mungu.
Samahani,
ndugu zangu!
Tusiruhusu matendo yao mabaya
yatunyime shangwe.
Kwa nini?
Sisi tumefaidikaje kwa kumtumikia Yehova?
Kweli,
si andiko linasema:
“Watunze vizuri kondoo wako”?
Na linasema pia:
“Mtu mwaminifu atapata baraka nyingi.”
Tunapaswa kumtumaini Yehova,
hatimaye
yeye atanyoosha kila kitu.
Malaki aliona hali mbaya sana ya watu.
Walawi,
ambao wakati fulani
walikuwa watetezi wakuu
wa viwango vya Yehova,
sasa walianza kuwa na shaka
kuhusu utumishi wao wenyewe.
Kijana!
Mbona usitoe dhabihu ya kondoo?
Toa dhabihu kubwa,
upate baraka kubwa.
Na usisahau,
majirani wako watakuheshimu.
Asante.
Tayari nina dhabihu yangu.
Sawa, sawa. Subiri!
Unaonekana kama mtu mzuri.
Kwa hiyo wewe leo
nikuuzie kwa bei maalumu
ya chini hata kuliko njiwa wako.
Karibia uangalie.
Huyo kondoo ni kipofu!
Halafu anachechemea!
Kijana sikiliza,
aina hii ya kondoo wanakuwa hivyo.
Sheria inasema
tusitoe wanyama vilema, vipofu
au wagonjwa.
Nitakapoweza kutoa kondoo,
atakuwa mwenye afya.
Huko ni kutupa pesa!
Huyu kondoo yuko sawa.
-Tena bei nzuri!
-Niache niondoke.
Tumia akili,
hiyo ni desturi tu.
Aah!
Mambo hekaluni yamebadilika sana.
Ni kana kwamba
watu wote hawamkumbuki Yehova tena.
Azuba!
Kuna nini?
Azuba
Nini kimetokea?
Rahamu anaendeleaje?
Eti cheti cha talaka?
Nilijaribu kuwa mke mzuri,
lakini hakuridhika.
Rahamu amenifukuza.
Usiogope Azuba.
Unaweza kuishi hapa,
na sisi.
Unakaribishwa.
Jamani!
Ni makosa yangu.
Hupaswi kufikiri hivyo.
Lakini sikumzalia watoto.
Muwe mna watoto au la.
Ndoa ni takatifu.
Mtegemee Yehova.
Yeye hatawahi kukuacha.
Asante.
Rahamu!
Tulipata mgeni jana usiku.
Mke wako,
au tuseme mke wako wa awali.
Rahamu,
hujali kumuumiza mwenzi
wako asiye na hatia?
Unawezaje kuwa na moyo mgumu hivyo?
Musa alisema ukiona
jambo fulani lisilofaa kwa mke wako,
mwandikie cheti cha talaka,
mpe na umruhusu aondoke.
Nieleze nini kingine hakifai
mbali na kukosa kunipa watoto.
Na pia nimechoka kuishi naye,
namwoa Gisla leo.
Gisla?
Yule msichana Mmoabu?
Nilikusikia ukijifunga kiapo na laana
kwamba hutachukua
mwanamke kutoka kwa mataifa!
Sheria inasema
“Watawapotosha wana wenu waache
kumfuata Mungu
na kuanza kuabudu miungu mingine;
kisha hasira ya Yehova itawaka dhidi yenu”!
Wewe ni nani,
unishauri mimi?
Kila mtu lazima ajitafutie
raha mwenyewe,
na mimi najitafutia yangu.
Rahamu,
ni Yehova tu anayeweza
kukupa shangwe ya kweli.
Unafikiri unaweza kujipatia shangwe
kuliko ile anayotoa?
Yehova,
kwa nini tunatendeana kwa hila hivi,
na kulinajisi agano lako?
Malaki!
Waambie makuhani
wanaolidharau jina langu:
“Mwana humheshimu baba yake,
na mtumishi bwana wake.
Basi ikiwa mimi ni baba,
iko wapi heshima ninayostahili?
Na ikiwa mimi ni bwana,
iko wapi hofu ninayostahili?”
Rafiki yangu!
karibu, naona huna dhabihu.
Kwa nini ninyi Walawi mmelidharau
jina la Yehova?
-Eti kulidharau?
Vipi?
Mnamtoa mnyama kipofu
kilema,
au mgonjwa
kuwa dhabihu na mnasema: “Si vibaya.”
Je, Yehova anapaswa
kukubali dhabihu hizo?
Nyama inapopikwa ndani ya chungu,
hakuna anayeweza kujua
ikiwa mnyama huyo alikuwa kilema.
Namna gani Yehova?
Yeye hawezi kutofautisha?
Siku moja Yehova atakuja hekaluni mwake.
Naye atawasafisha
ninyi wana wa Lawi kwa moto.
Malaki, kwani wewe una shida gani?
Kwa nini wewe ulalamike
wakati hakuna mtu mwingine
anayeona tatizo?
“Enyi makuhani
mkikataa kuitia
moyoni mwenu” asema Yehova
“Nitawaletea laana,
nami nitabadili baraka zenu ziwe laana.”
“Nirudieni,
nami nitawarudia”
asema Yehova.
Sisi tutamrudiaje?
“Je, mwanadamu
anaweza kumwibia Mungu?
Lakini ninyi mnaniibia.”
asema Yehova.
Tumemwibiaje?
“Katika sehemu za kumi
na michango mnaniibia.
Naam, taifa zima linafanya hivyo.
“Leteni ghalani sehemu yote ya kumi,
ili kuwe na chakula nyumbani mwangu;
tafadhali, nijaribuni,
mwone kama sitawafungulia
malango ya mbinguni ya mafuriko
na kuwamwagia baraka
hivi kwamba hamtakosa chochote.”
Na kuna jambo lingine mnalotenda,
hivi kwamba hakubali
chochote mnachotoa.
Kwa nini?
Kwa sababu mnamsaliti mke wa ujana,
ingawa ni mwenzi wako,
mke wako halali.
Lakini kuna baadhi yenu
ambao hawafanyi hivyo
kwa sababu bado wana roho ya Mungu.
Basi jilindeni kuhusiana na roho yenu,
na usimtendee kwa hila
mke wa ujana wako.
“Kwa maana ninachukia talaka,”
asema Yehova Mungu wa Israeli.
Midomo ya kuhani inapaswa kulinda ujuzi,
na watu wanapaswa kutafuta sheria
kutoka kinywani mwake.
Lakini nyinyi
mmewafanya wengi wajikwae.
Ujumbe wa Yehova ulifunua kwamba
tatizo lilikuwa moyoni mwao.
Licha ya hilo,
Malaki aliwatafuta wale waliokuwa na
shangwe katika kufanya lililo sawa.
Pelethi.
Malaki.
Nimefurahi kukuona?
Azuba,
usiwe na hofu.
Utaona tofauti kati ya mwadilifu
na mwovu,
kati ya mtu anayemtumikia Mungu
na asiyemtumikia.
Lazima wewe ni nabii.
Ninamtumikia Yehova kama nyinyi tu.
Na niwaambie,
unapozungumza na mwenzako
kuhusu Yehova
anasikiliza.
Anaandika kitabu
kwa ajili ya wanaomwogopa
na wanaolitafakari jina lake.
Yehova na awe pamoja nanyi.
Kwa miaka mingi nilikuwa
mbali na Yerusalemu
lakini sikuzote moyo wangu
ulikuwa pamoja na watu wangu.
Kwa hiyo niliomba ruhusu
nirudi Yerusalemu.
Nilichoona kilinishtua.
Eliashibu!
Na uwe na amani.
Nehemia!
Sikuwa nikikutarajia . . .
Wako wapi Walawi wote na waimbaji?
Baadhi yao wameondoka kwa muda.
Eti wameondoka?
Kwa nini wameondoka?
Umm,
Pedaya yuko hapa.
Pedaya mtembeze Gavana Nehemia.
Samahani kidogo.
Sawa tu.
Pedaya nieleze kuhusu
huduma za hekalu.
Je, mnapata maandalizi yote mnayohitaji?
Gavana Nehemia,
hatuna maandalizi yoyote hapa.
Hilo linawezekanaje?
Kwa muda mrefu sana,
makuhani na Walawi
hawajachukua majukumu yao
kwa uzito.
Watu walipoona hivyo
wakaacha kutoa sehemu ya kumi.
Bila sehemu ya kumi,
Walawi na waimbaji
wengi walirudi kwenye mashamba yao.
Kwa nini wewe hujarudi?
Ninaridhika na ninachopata.
Sikuzote nimeamini Yehova
huwasaidia wanaomtegemea.
Najua
atarekebisha mambo kwa wakati wake.
Kwani Eliashibu hakuwaambia
watu walete maandalizi?
Ulipoondoka
nabii Malaki alimwonya
na makuhani wengine wote.
Lakini Eliashibu
alichukua chumba chetu,
akaondoa maandalizi yetu
na kumpa Tobia
kiwe chumba chake cha kulia chakula.
Pedaya,
tusaidie kuondoa vitu hivi.
Unafanya nini?
Eliashibu!
Wewe umekuwa ukifanya nini?
Kwa nini wewe na watawala wasaidizi
mmeipuuza nyumba ya Mungu?
Nehemia.
Tafadhali takasa chumba hiki
na urudishe vyombo vilivyotolewa.
-Ndio bwanangu.
Na uwakusanye Walawi wote,
waimbaji na watawala wasaidizi.
Nawarudisha kwenye migawo yao hekaluni.
Pedaya,
Ninakuweka wewe, Shelemia, na Sadoki
kusimamia maghala.
Hanani atakuwa msaidizi wako.
Ni jukumu lako kuwagawia
ndugu zako maandalizi.
Nehemia,
subiri kidogo.
Acha nikueleze.
Nami nitawaambia watu wote wa Yuda
walete sehemu ya kumi ya nafaka,
ya divai mpya
na mafuta.
Acha nikueleze.
Hapana,
subirini, subirini.
Unikumbuke mimi, Ee Mungu wangu,
usiyafutilie mbali
matendo yangu ya upendo mshikamanifu
kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.
Mbali tu na kuipuuza nyumba ya Yehova
baadhi ya Wayahudi waliendelea
kufanya bishara siku ya Sabato.
Siku ambayo Yehova
alikuwa ameitangaza kuwa takatifu.
Unauza nini leo?
Samaki bora zaidi kutoka Tiro.
Mnafanya nini?
Hamjui kwamba leo ni Sabato?
Nehemia.
Huu ni uovu gani ambao mnafanya?
Hii ndio sababu Yehova aliangamiza jiji hili!
Watu wanaona kwamba ni sawa sasa.
Na Yehova ana maoni gani?
Nilizuia biashara ya kununua na kuuza
na nikaamuru malango yafungwe
ili kudumisha utakatifu wa siku ya Sabato
Lakini juma lililofuata
wafanyabiashara walijaribu tena.
Kwani kuna nini kinaendelea?
Jana nimelazimika kulala hapa chini.
Mnajua sheria ya Mungu:
Hakuna kazi,
wala biashara,
siku ya Sabato!
Ondokeni!
Walawi mtalinda malango,
Sabato idumishwe ikiwa takatifu.
Usimruhusu mtu aingie!
Ee Mungu wangu,
unikumbuke pia kwa jambo hili
na unihurumie kwa sababu ya
upendo wako mwingi mshikamanifu.
Kuna jambo lingine ambalo nilihitaji kufanya.
Njoo twende.
Ana la mitbayen.
Wewe!
Unaenda wapi?
Rudi hapa.
Mimi ni baba yako, nakuambia urudi!
Watoto wana shida gani?
Aah!
Hawapendi kuja hekaluni.
Binti yangu,
kwani wewe hulipendi hekalu?
Shvok Y-ati!
Wewe!
Ah!
Rudi hapa.
Samahani bwana wangu.
Mke wangu hajui Kiebrania.
Je, hukuapa kwamba hutawahi
kumwoa mtu asiyemwabudu Yehova?
Nehemia hakuna mtu anajali.
Je, uliapa?
Ndiyo!
-Ndiyo!
-Basi kwa nini umepuuza
amri ya Yehova
na kiapo chako mwenyewe?
Niache!
Ndio sababu watoto wako
hawampendi Yehova.
Ulifikiri ungefanikiwa
bila baraka za Yehova?
Nilisali Yehova anibariki!
Kweli?
Basi kwa nini hukumtii?
Rahamu,
Yehova atabarikije kitu kilicho
kinyume na mapenzi yake?
Sikupaswa kushangaa?
Watu walikuwa wakiiga mfano mbaya
wa wale waliokuwa wakiongoza.
Mjukuu wa Eliashibu alioa Mhoroni,
binti ya Sanbalati.
Kwa nini huheshimu sheria ya Mungu?
Msikubali binti zenu waolewe na wana wao
na msikubali mabinti wao
waolewe na wana wenu!
Au ninyi wenyewe?
Je, mfalme Sulemani wa Israeli
hakutenda dhambi kwa sababu yao?
Babu, si useme kitu?
Tulia mwanangu.
Je, si jambo linaloshangaza kwenu
kutenda uovu huu mkubwa
kwa kuoa wanawake wa kigeni?
Umeuchafua ukuhani!
Huwezi tena kuendelea kuwa kuhani
wala kuishi Yerusalemu
Sawa.
Nitaenda Samaria.
Huko watanikubali.
Lakini yeye ni mjukuu wangu.
Basi kwa nini ulimruhusu
avunje sheria ya Yehova?
Wewe unajua
utumishi wa hekalu
ndio unaotuwezesha
tuwe na uhusiano na Mungu!
Lakini mara tu nilipoondoka,
ninyi nyote,
mliruhusu mambo yakazorota.
Ilichukua muda,
lakini ibada ya kweli
ilirudishwa.
Ninapotafakari mambo yote
ambayo Yehova alituwezesha kutimiza . . .
Licha ya upinzani tuliokabili
Mimi napendekeza
tumshtaki Nehemia kuwa mwasi na mhaini.
Sauti inayofuata watakayosikia
ni kishindo chetu cha vita
Unataka kusubiri
hadi watakapoanza kutuua?
. . . uvutano mbaya tulioepuka . . .
Nina haki ya kuishi niapotaka, nawe pia.
Unapaswa kujiunga na mimi kukataa kuhama.
Huko ni kutupa pesa!
Tumia akili!
Hiyo ni desturi tu.
Ikiwa tunataka kula,
tunapaswa kwenda kuchunga mifugo yetu
na kulima.
Hakuna faida kumtumikia Mungu.
. . . usiku wote tuliokesha bila kulala, . . .
Lazima twende Yerusalemu
tuone Nehemia anapanga kufanya nini.
Hawafurahishwi na tunachofanya
wanatuchukia.
Na wewe huishi na kufanya kazi
karibu nao kama sisi.
. . . jasho na kazi ngumu . . .
Na pia hii kazi ni kubwa mno kwetu.
Tumechoka kabisa.
Kwani ukuta wenyewe hata ni wa nini? . . .
Ninakumbuka tu shangwe tuliyohisi
kwa sababu tulikuwa tunamtumikia Yehova
kwa njia inayofaa
Tulifikiri kwamba tulikuwa
tunajenga ukuta tu,
lakini Yehova alikuwa
akijenga upya imani yetu.
Sitasahau jinsi Yehova alivyotuunganisha
ili kutimiza mapenzi yake.
Alitufundisha kumtegemea
na alituimarisha.
Mkale vitu bora,
na kunywa vitu vitamu,
na mwape chakula wale ambao hawana.
Nanyi msihuzunike,
kwa maana shangwe ya Yehova
ndiyo ngome yenu.
Unikumbuke na kunitendea wema,
Ee Mungu wangu.
Nehemia alikuwa mwanamume jasiri.
Angeweza kukaa kwenye
makao ya mfalme kule Shushani
na amtumikie Yehova akiwa huko.
Hakufanya hivyo.
Kulipokuwa na uhitaji
alikuwa tayari kusafiri kwenda mbali
hadi Yerusalemu
ili kuunga mkono ndugu zake.
Lakini haikuwa rahisi.
Kwanza, alihitaji kumwomba
mfalme wa Uajemi amruhusu kuondoka.
Ni nini kilichomsaidia Nehemia atende
kwa ujasiri kwa ajili ya Yehova?
Je, alitegemea utu wake
au kwamba mfalme alimpenda
na kumheshimu?
Acheni tutazame sehemu hii tena.
Mahali ambapo mababu zangu
wamezikwa ni magofu
na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Nehemia, unasema nini?
Nieleze unachotaka.
Usinifiche chochote.
Mara moja nikasali kwa Mungu wa mbinguni.
Ukipenda ee mfalme,
na ikiwa mimi mtumishi wako
nimepata kibali chako
niruhusu niende Yuda,
kwenye jiji ambalo mababu zangu wamezikwa,
ili nilijenge upya.
Unaweza kwenda.
Yehova alikuwa pamoja nasi.
Mara moja
Nehemia alitoa sala
kwa unyenyekevu kwa Yehova
ambaye ndiye Chanzo cha ujasiri wa kweli.
Alisali mara nyingi wakati wa mgawo wake
na Yehova alibariki jitihada zake.
Kwa hiyo somo la kwanza kwetu leo,
hali zinapokuwa ngumu
huenda ikawa rahisi kumtegemea Yehova.
Lakini vipi ikiwa mambo ni shwari?
Je, bado tunaendelea kumtegemea Yehova?
Au je, sasa tunajikuta
tukistarehe tu,
na labda hata kujiambia:
“Maisha yangu ni raha mstarehe.
Najua kuna kazi nyingi ya kufanya
lakini nimemtumikia Yehova
kwa miaka mingi sana sasa.
Nimetimiza sehemu yangu.
Acha mtu mwingine sasa afanye.”?
Je, Yehova atabariki mtazamo kama huo?
Je, isingefaa kutoa sala
kwa Yehova na kumwomba
akupe ujasiri na shangwe
ya kuendelea kujitoa zaidi
katika utumishi wako kwake?
Huenda ukashangaa
kuona milango
ambayo Yehova atakufungulia.
Sasa, Nehemia alipowasili Yerusalemu,
hakuanza kuwaamuruamuru watu, sivyo?
Biblia inasema kwamba
kila siku alifanya kazi
pamoja na Waisraeli wenzake
“kuanzia mapambazuko
mpaka nyota zilipoonekana.”
Kwa njia hiyo,
sisi pia tunapoonyesha roho ya kujidhabihu,
Yehova atatupatia nguvu tunazohitaji
ili kutimiza kazi iliyo mbele yetu.
Waisraeli walikamilisha kazi ya
ujenzi wa ukuta katika siku 52 tu!
Hilo lilikuwa jambo lenye kushangaza
hasa ukifikiria upinzani waliokabili!
Mwanzoni, upinzani ulikuwa ni dhihaka.
Halafu wapinzani wakatisha kushambulia!
Kaskazini kulikuwa na Wasamaria,
Waamoni walikuwa upande wa mashariki,
Waarabu upande wa kusini,
na Waashdodi upande wa magharibi.
Yerusalemu lilizungukwa na maadui.
Ingekuwa rahisi kujihisi wamenaswa
na kuruhusu hofu iwalemaze.
Nehemia alifanya nini?
Unakumbuka kawaida yake?
Kwa maneno yake mwenyewe alisema:
“Tulisali kwa Mungu wetu.”
Kisha Nehemia
akawaimarisha watu kwa kuwaambia:
“Msiwaogope.
Mkumbukeni Yehova,
ambaye ni mkuu na mwenye kuogopesha.”
Na basi wakaendelea kujenga.
Maadui wa Nehemia walipotambua
kwamba vitisho vyao vilikuwa vimeshindwa,
je, walikata tamaa?
La.
Walianza kutumia
mbinu nyingine za upinzani.
Walijaribu mbinu tatu
ili kumkengeusha Nehemia
aache kufanya kazi.
Ulitambua mbinu hizo?
Tutazame video hiyo tena.
Walimwambia Nehemia wakutane katikati.
Nenda umwambie Nehemia:
“Njoo,
tupange wakati ili tukutane
kwenye vijiji vya Bonde Tambarare la Ono.”
Ni mbinu ya kunitoa nje ya Yerusalemu.
Walieneza habari za uwongo.
Geshemu,
wakati umefika wa kutumia mbinu yako.
Tobia,
andika maneno haya:
“Kuna habari zinazoenezwa katika mataifa,
na Geshemu
anasema pia
kwamba wewe
na Wayahudi
mnapanga kuasi.
Hii ndiyo sababu unajenga ukuta.”
Na walitumia msaliti
kujaribu kumdanganya Nehemia.
Wanakuja kukuua.
Watakuja usiku!
Tunapaswa kuingia ndani ya hekalu
na tufunge milango.
Shemaya,
je, mtu kama mimi anapaswa kukimbia?
Naona huelewi.
Hapana,
Kufanya hivyo
kutaathiri ujasiri wa taifa lote?
Hapo tu ndipo utakuwa salama.
Na usisahau mimi si kuhani.
Nikiingia hekaluni, ninastahili kufa.
Kwa hiyo, sitaingia.
Huo ni uamuzi wa kipumbavu Nehemia.
Sasa nimeelewa!
Tobia na Sanbalati walikutuma
uje uniambie maneno hayo, sivyo?
Mnafiki.
Yehova na awakumbuke wao.
Na akukumbuke wewe
na manabii wenzako wa uwongo
wanaojaribu kuniogopesha.
Tuondoke Hanani,
tuna kazi ya kufanya.
Njama tatu
na zote zilishindwa.
Basi hili ndilo somo la pili:
Huenda tukakumbana
na wapinzani ambao kwa ujanja watajaribu
kutuzuia
tusiendelee kumtumikia Yehova
kwa ushikamanifu.
Huenda baadhi yao wakajaribu
kutufanya tukutane katikati
kwa njia ya mfano,
labda kwa kujaribu kutusadikisha kwamba
tukipunguza bidii ya kumtumikia Yehova
tunaweza kufuatia miradi
ya kilimwengu wakati huohuo.
Hata hivyo,
kwa kuwa tunatanguliza
Ufalme wa Mungu maishani mwetu
tunaweza kuwa kama Nehemia
na kukataa kuunga mkono.
Tunajua mahali ambapo
ulimwengu huu unaelekea.
Pia wapinzani wetu hutoa
mashtaka ya uwongo dhidi yetu.
Katika nchi fulani,
tunashtakiwa kwamba sisi ni
hatari kwa serikali.
Tumefanikiwa kushinda
mashtaka fulani mahakamani.
Lakini vyovyote vile,
tuna uhakika
kwamba Yehova ataongoza mambo
kulingana na mapenzi yake.
Pia,
upinzani unaweza kutoka
kwa wale wanaodai
kwamba wanamtumikia Yehova.
Kama vile Myahudi mwenzake
alivyojaribu kumfanya Nehemia
avunje sheria ya Mungu ili kuokoa uhai wake,
ndivyo baadhi ya watu
ambao zamani walikuwa Mashahidi
wanaweza kujaribu kutufanya
tuvunje imani yetu.
Lakini tunawapinga waasi-imani
kwa sababu tunajua tunaokoa maisha yetu,
si kwa kuvunja sheria za Mungu,
bali kwa kuzifuata.
Pindi zote,
Nehemia alikataa
kunaswa na mitego waliyoweka.
Kwa nini?
je, ni kwa sababu alikuwa na akili nyingi?
Hapana!
Ni kwa sababu alimtegemea Yehova,
naye Yehova alimpa ufahamu aliohitaji
ili kutambua njama zao zenye hila.
Baada ya kuta kujengwa,
Nehemia aliondoka Yerusalemu kwa muda.
Lakini hali zilikuwaje aliporudi?
Badala ya kurudi
na kukuta ibada safi ikinawiri,
alikuta hali ikiwa mbaya sana.
Alikuwa amefanya kazi nyingi sana
kuwasaidia watu wamtegemee Yehova
Unafikiri alihisije?
Angeweza kusema:
“Imetosha!
Mimi nimechoka!
Acha mwingine aje arekebishe hali hii,”
halafu aondoke.
Je, alifanya hivyo?
Acheni tuone tena.
Kwa nini wewe na watawala wasaidizi
mmeipuuza nyumba ya Mungu?
Tafadhali takasa chumba hiki.
Mnajua sheria ya Mungu:
Hakuna kazi,
wala biashara,
Siku ya Sabato!
Ondokeni!
Je, hukuapa kwamba hutawahi
kumwoa mtu asiyemwabudu Yehova?
Basi kwa nini umepuuza amri ya Yehova
na kiapo chako mwenyewe?
Nehemia,
mjukuu wa Eliashibu alioa Mhoroni,
binti ya Sanbalati.
Msikubali binti zenu waolewe na wana wao
na wana wenu wasioe binti zao!
Umeuchafua ukuhani!
Huwezi tena kuendelea kuwa kuhani
wala kuishi Yerusalemu.
Ilichukua muda
lakini ibada ya kweli
ilirudishwa.
Nehemia hakuondoka tu,
sivyo?
La,
alidumu katika mgawo wake.
Kwa nini?
Kwa sababu alidumisha shangwe yake.
Chanzo chake kikuu cha shangwe
hakikuwa mambo aliyotimiza,
au usalama ulitokezwa na kuta hizo,
wala haukutegemea
mambo ambayo wengine walifanya.
Shangwe ya kweli inatoka wapi?
Nehemia mwenyewe alituambia:
“Shangwe ya Yehova ndiyo ngome yenu.”
Kwa hiyo hili ndilo somo la tatu kwetu:
Licha ya hali ngumu na changamoto,
tunaweza kuwa na shangwe
kwa sababu shangwe ya kweli huja
kwa kuwa na uhusiano mzuri
pamoja na Yehova.
Nehemia alikuwa mwanadamu
kama wewe na mimi.
Kumbuka,
Nehemia hakuona miujiza ya Yehova
kama vile Musa na Yoshua walivyojionea.
Lakini angeweza kufanya nini?
Angeweza kusali,
angeweza kuonyesha imani
na alikuwa na uhakika.
Mambo hayo yalimtegemeza.
Na hakuna shaka
kwamba Yehova alikuwa akitenda
kwa niaba ya Nehemia,
akiongoza na kubariki jitihada zake.
Sisi tunaweza kutumia mambo hayo leo.
Sali kwa Yehova,
uwe na imani katika Yeye,
na uwe na uhakika kwamba atabariki
jitihada zako za kujidhabihu.
Kama tu Yehova alivyompa Nehemia ujasiri,
nguvu,
ufahamu,
na udumifu wa kutimiza mgawo wake
atafanya hivyo pia,
kwa niaba yako.