JW subtitle extractor

Jinsi Neno la Mungu Lilivyoandikwa

Video Other languages Share text Share link Show times

Mungu aliwaongoza watu 40
kuandika Biblia
Umewahi kujiuliza,
Walitumia nini kuandika?
Kwasababu
sehemu za zamani zaidi za Biblia
ziliandikwa zaidi ya miaka 1000
kabla ya karatasi kubuniwa.
Hati za kale za Biblia ziliandikwa
juu ya kitu kinachoitwa mafunjo.
Mafunjo hutoka kwenye mmea
unaokua kwenye maji yasiyo na kina
na mmea huo unaweza kukua
kufikia mita 4.6 hivi.
Zaidi ya miaka 4000 iliyopita,
Wamisri walibuni
njia ya kufanya mafunjo
yawe kifaa laini
ambacho kinaweza kuandikiwa
kama karatasi.
Hata ukitumia vifaa vya kisasa,
utaona hiyo ilikuwa kazi nyingi sana.
Vipande vyembamba vya katikati
vilihitaji kulainishwa,
na kutiwa ndani ya maji
kisha vingepangwa katika safu.
Halafu vingegongwa na kubanwa
ili kuviunganisha.
Kurasa hizo zilipokauka,
zilizonyooshwa kwa kutumia
kipande cha jino la tembo,
gamba, au jiwe laini.
Na hapo ndipo ukurasa mwororo
ungepatikana wa kuandikia.
Ili kufanyiza kitabu cha kukunjwa,
kurasa kadhaa
ziliunganishwa kuwa gundi
na kufanyiza kitabu cha kukunjwa
chenye urefu wa mita 6 hivi.
Hata hivyo kufikia karne ya pili
wakati wa kawaida,
wanakili
walianza kutumia mbinu nyingine
ambayo ilifanya iwe rahisi
kutumia kurasa hizo za mafunjo
iliitwa Kodeksi.
Ili kutengeneza Kodeksi
kurasa za mafunjo zilikunjwa
kisha zikashonwa
na hivyo kuunganishwa
ili kufanyiza kitu kama kitabu cha kisasa.
Wazia ilichukua saa nyingi kadri gani
ili kutengeneza vifaa hivi vyote
ili kuandika.
Lakini kwa kuwa hawakuwa
na kalamu kama za sasa,
walitumia nini kuandikia?
Mara nyingi kalamu walizotumia
zilitengenezwa kutokana
na utetee mgumu kama huu
zilichongwa kwa uangalifu
ili kufanyiza ncha kali kama hii.
Katika nyakati za Biblia
rangi ambayo kwa kawaida
iliyotumiwa na kalamu hizi
ilitengenezwa kwa
masinzi meusi kama ya mkaa
na kuunganishwa na aina fulani ya
mpira unaonata.
Kisha yakichanganywa na maji.
Tatizo la mafunjo ni kwamba
iwe yalitengenezwa
kama kitabu cha kukunjwa
au kama Kodeksi,
yaliharibika upesi.
Inashangaza kwamba,
kuna vipande vingi
vya hati za Biblia
zilizoandikwa kwenye mafunjo
ambazo zimeokoka hadi leo hii.
Hapa kuna vipande vya mafunjo
ambavyo viliandikwa
miaka 2000 iliyopita.
Baada ya muda
hati za Biblia zilianza kunakiliwa
kwenye vifaa vinavyodumu zaidi.
Kufikia karne ya nne
ngozi za wanyama
zilianza kutumiwa sana
na hasa wanyama kama kondoo,
ndama, na mbuzi.
Mchakato ulianza
kwa kutumbukiza ngozi hiyo
ndani ya maji yenye limao.
kisha manyoya na nyama yeyote
iliyosalia zikaondolewa.
Baadaye ngozi hiyo ilinyooshwa
na kuondolewa kitu chochote
kilichosalia kama vile mafuta.
Kisha ngozi hiyo ingekazwa hata zaidi
ili ikaushwe.
Hilo lingeifanya iwe ngumu na inyooke.
Halafu ingenyunyuziwa chokaa
na kupigwa msasa
kwa jiwe la kukwaruzia
ili kufanyiza sehemu laini ya kuandikia.
Kama unavyoona
ilikuwa kazi kubwa sana
kutengeneza ukurasa mmoja tu wa ngozi.
Hata hivyo leo
kuna hati nyingi sana
ambazo zimeokoka
ambazo ziliandikwa kwenye ngozi
kama hizi mbili.
Hati nyingine maarufu
ni Kodeksi Amiatinus,
iliyoko Italia
iliandikwa miaka 1300 iliyopita.
Hiyo ndiyo Biblia ya zamani zaidi
ya Kilatini
iliyowahi kupatikana katika buku moja.
Wanahistoria wanasema
ngozi za wanyama zaidi ya 400
zilitumika kuitengeneza.
Huu ni mfano tu wa Biblia hiyo
na kama uonavyo ni kubwa sana
hata hivyo Biblia yenyewe ni kubwa zaidi
na ina uzito wa kilo 34.
Wazia ni kazi nyingi kadiri gani
iliyohusika ili kutengeneza
Biblia hiyo moja tu.
Lakini vifaa hivyo vyote
vinaweza kudhoofika
na kuharibika kadiri muda unavyopita.
Hata hivyo ili kuhakikisha kwamba
Neno lake linahifadhiwa
Yehova alihakikisha Biblia inanakiliwa
tena na tena kwa umakini
hivi kwamba leo tuna maelfu ya hati
zinazotuonyesha
sehemu mbalimbali za Biblia.
Kwa hiyo wakati ujao
unaposoma tu mstari
kwa kubofya kiunganishi,
tafakari ni kazi gani
iliyohusika ili kuandika maneno haya
na jinsi inavyostaajabisha
kwamba licha ya kuandikwa kwenye
vifaa vya kale vinavyoharibika,
Neno la Mungu
bado linapatikana leo.