JW subtitle extractor

Unaweza Kufanya Nini Magonjwa ya Mlipuko Yakitokea?

Video Other languages Share text Share link Show times

Magonjwa ya kuambukiza
yamekuwepo kwa
muda mrefu sana.
Huenda zamani
ulisikia kuhusu
milipuko ya magonjwa
katika maeneo mengine.
Lakini utafanya nini ugonjwa
ukisambaa mpaka
eneo unaloishi?
Kwa kuwa huwezi
kuuzuia usisambae,
huenda ukaogopa sana.
Lakini unaweza kujilinda
na kuwa na afya nzuri.
Unaweza kujilinda
kwa njia rahisi
kama vile kunawa
mikono mara kwa mara.
Ikiwa utatumia sekunde
ishirini au zaidi
kunawa mikono
kwa maji na sabuni,
utaua bakteria au
virusi vya magonjwa.
Pia unaweza kutumia
dawa ya kusafisha mikono,
yaani ‘sanitizer.’
Unapokohoa au
kupiga chafya
tumia tishu au
kiwiko cha mkono.
Na pia, epuka
kugusa uso wako
hasa baada ya
kugusa vitu vingine.
Fuata maelekezo
ya wenye mamlaka
kama vile kukaa nyumbani
kwa muda fulani,
kuvaa barakoa,
au kudumisha umbali unaofaa
kati yako na watu wengine.
Na ukiwa mgonjwa,
wasiliana na daktari mara moja.
Ni muhimu pia
kujali hisia zako.
Unaweza kupata mkazo
ukisikiliza habari
nyingi mbaya,
zilizopotoshwa, au zinazopingana.
Ni muhimu kupata habari
lakini uwe na usawaziko
ili zisikupe mkazo.
Uwe na mambo
mengi ya kufanya
na uwasiliane na
ndugu na marafiki.
Unaweza kuwafurahisha
na ukajihisi vizuri.
Kuna jambo lingine
ambalo ni muhimu sana.
Biblia inasema
Yesu alitenga wakati
wa kuwa peke yake
ili asali na kutafakari.
Tumia muda kutunza
afya yako ya kiroho.
Ikiwa utakazia fikira
tumaini la wakati ujao,
itakuwa rahisi
kukabiliana na matatizo.
Mashahidi wa Yehova
huimarisha tumaini lao
kwa kuwaeleza wengine
kulihusu kwa njia salama.
Wanawafundisha wengine Biblia.
Pia, wanawakaribisha
kwenye mikutano.
Hali zikiruhusu
hukutanika pamoja.
Zisiporuhusu hukutanika
kwa njia ya video.
Andiko la Isaya 33:24
linasema kwamba wakati ujao
hakuna mtu atakayesema,
“mimi ni mgonjwa.”
Hadi wakati huo ufike
Andiko la Isaya 30:15
linasema kwamba
tunahitaji kuendelea
“kuwa watulivu
na kuwa na tumaini.”
Hivyo, ugonjwa unapotokea
jitahidi kuwa mtulivu,
kupata habari,
na kudumisha afya yako.