JW subtitle extractor

Unabii wa Kimasihi Watimizwa!—Alikuwa Mzao wa Mfalme Daudi na Alitiwa Mafuta Kuwa “Masihi Aliye Kiongozi"

Video Other languages Share text Share link Show times

Maelfu ya miaka
hata kabla ya Yesu kuzaliwa,
unabii ulitolewa kumhusu Masihi,
kwenye Mwanzo 3:15
ulitabiri jukumu lake akiwa Masihi
yaani mzawo ambaye angetimiza
kusudi la Yehova.
Vitabu vya Biblia vya
Mathayo na Luka
vinatupatia orodha ya ukoo wa Yesu.
Vinataja wazao wa Adamu
kutia ndani Abrahamu.
Abrahamu aliahidiwa na Mungu
kwamba masihi angekuwa uzao wake.
Kadiri miaka ilivyosonga
manabii waliendelea kutoa unabii
kumhusu Yesu
na hata kufunua majina ya
watu wake wa ukoo.
Ilitabiriwa kwamba masihi angekuwa mzawo
wa mfalme Daudi.
Luka ameorodhesha watu
wa ukoo wa yesu
kupitia Nathani wa Ukoo wa Daudi
hadi kufikia Maria mama yake.
kwa upande mwingine Mathayo ameorodhesha
majina ya wana wa Daudi
waliokuwa na haki ya kisheria
ya kuketi kwenye
kiti chake cha ufalme
kuanzia Sulemani hadi Yosefu
aliyekuwa baba mlezi wa Yesu.
Nasaba ya Yesu ni utimizo
wa unabii uliotimizwa
katika kipindi cha mamia ya miaka
jambo hilo lilitupa uhakika kwamba
yeye ndiye Masihi.
Zaidi ya miaka mia tano
kabla ya kuzaliwa kwa Yesu,
malaika Gabrieli alimfunulia nabii Danieli
wakati hususa ambapo
Masihi angewekwa rasmi.
Malaika wa Yehova alimwambia Danieli
“tangu kutolewa kwa lile neno
la kurudisha na kuujenga upya Yerusalemu
mpaka atakapotokea Masihi aliye kiongozi,
kutakuwa na majuma 7,
na pia majuma 62.”
Jumla ya majuma 69.
Majuma 69 ni siku 483
Neno la kujenga upya Yerusalemu
lilitolewa mwaka wa 455 K.W.K.
huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa yale majuma 69.
Hata hivyo Masihi hakutokea
siku 483 baadaye,
lakini tukitumia kanuni ya hesabu
inayopatikana katika maandiko ambayo ni
“siku moja kwa mwaka mmoja”
tukihesabu miaka 483
badala ya siku 483
kuanzia mwaka wa 455 K.W.K.
tutafika mwaka wa 29 W.K.
Biblia inaonyesha kwamba Yesu alibatizwa
mwaka wa 29 W.K.
na kutiwa mafuta
kwa roho takatifu kuwa Masihi.
kutimizwa kwa unabii
ulio kwenye Danieli 9
kunaimarisha imani yetu katika Biblia
kumwelekea Yesu aliye Masihi aliyetabiriwa
na katika Yehova mtunza wakati mkuu.