JW subtitle extractor

Jifunze Uvumilivu Kupitia Uumbaji

Video Other languages Share text Share link Show times

Nini humsaidia ngamia kuishi katika mazingira haya magumu?
Yehova amempatia ngamia uwezo wa pekee unaomsaidia kuishi jangwani.
Ngamia huhifadhi nini kwenye nundu yake?
Mafuta. Nundu ya ngamia mwenye afya nzuri inaweza kufikia uzito wa kilogramu 36.
Kunapokuwa na shida ya chakula ngamia hutumia mafuta hayo.
Anapopata nafasi, ngamia mwenye kiu anaweza kunywa
lita 95 za maji ndani ya dakika chache sana.
Ingawa hivyo, hata wakati wa joto kali miili yao hutoa jasho kidogo sana.
Kwa hiyo wanaweza kuishi kwa majuma au hata miezi kadhaa bila kunywa maji.
Uwezo wa pekee wa ngamia wa kupokea na kuhifadhi virutubisho na maji
humwezesha kuvumilia.
Kwenye maeneo ya juu ya milima ya Amerika Kaskazini,
mazingira hayaruhusu mimea mingi kukua.
Hata hivyo, misonabari aina ya bristlecone
hukua na kusitawi kwenye kimo cha meta 3,000
[sawa na futi 10,000] juu ya usawa wa bahari.
Miti hii yenye kustaajabisha inaweza kuishi kwa maelfu ya miaka.
Siri moja inayoiwezesha kusitawi ni mizizi yake.
Mizizi mingi midogo iliyosambaa huiwezesha miti hiyo kupata maji kwa wingi.
Halafu mizizi mikubwa na imara huitegemeza dhidi ya upepo mkali.
Misonabari hii imeumbwa kwa njia ambayo inaweza kustahimili mazingira magumu.
Hivyo, ni kati ya mimea inayoishi miaka mingi zaidi duniani.
Vipepeo wanatimiza jukumu muhimu sana katika kuchavusha maua.
Pia wanaweza kuvumilia kwa kadiri kubwa sana.
Kila mwaka huko Amerika Kaskazini, vipepeo aina ya monarch karibu milioni 300,
husafiri umbali wa kilometa 4,000 hivi, kutoka kaskazini mwa Kanada
hadi kwenye msitu nchini Mexico.
Vipepeo pia wana uwezo mkubwa wa kustahimili hali ngumu.
Baadhi ya vipepeo wameonekana wakiendelea kula na kuruka,
mabawa yao yakiwa yameharibika kwa asilimia 70.
Huenda vipepeo wakaonekana kuwa dhaifu,
lakini viumbe hao wadogo huonyesha uvumilivu wa hali ya juu sana.
Membe wengi wa aktiki hutagia mayai yao maeneo ya kaskazini mwa dunia,
na kutumia kipindi kifupi cha joto kwenye maeneo hayo kulisha na kulea makinda yao.
Lakini majira ya baridi yanapokaribia, wao huhamia maeneo ya Antaktika
ambapo hukuta majira ya joto yakiwa tu yameanza.
Majira ya joto yanapoisha, wanarudi Aktiki,
na kukamilisha safari ndefu zaidi kuliko kiumbe mwingine yeyote
inayofanywa ndani ya mwaka mmoja.
Ni nini humwongoza membe wa aktiki katika safari yake?
Wanasayansi wanaamini kwamba ndege hao
hutumia nguvu za sumaku za dunia kuwaongoza.
Wanawezaje kufanya hivyo?
Bado haijulikani.
Yehova amewapatia membe wa aktiki mfumo sahihi wa kuwaongoza
ambao huwawezesha kusafiri umbali huo mrefu.
Kiluwiluwi ni aina ya ndege wanaopatikana barani Afrika.
Wao hujenga viota vyao ardhini, mara nyingi kando ya maji.
Hayo ni maeneo ambayo wanyama wakubwa hupita.
Viota vyao vinapokuwa hatarini, wao hutoa sauti kali ya kuonya.
Nyakati fulani kiluwiluwi hujaribu kumpumbaza adui aende mbali na kiota chake.
Wakati mwingine, kwa ujasiri ndege huyo humzuia adui kwa kusimama,
kutanua mabawa, na kutoa sauti kali.
Viluwiluwi hujaribu kuwashambulia wanadamu, tembo na nyati,
na nyakati fulani huwashambulia kwa midomo yao yenye ncha kali.
Yehova amempa ndege huyu ujasiri wa kulinda makinda yake,
na hivyo kumwezesha abaki salama.
Nyika ya Sinai hupata kiasi kidogo sana cha mvua.
Migunga ni kati ya miti michache inayoota kwenye eneo hilo.
Mti huo ni mzito, mgumu, na hauwezi kuharibiwa na wadudu.
Aina fulani ya migunga hulindwa na gome nene na miiba mirefu yenye ncha kali.
Mara nyingi, migunga huota karibu-karibu.
Matawi ya baadhi ya migunga huungana na kuwa kama mwavuli.
Migunga mingine hukua pamoja na kufanyiza vichaka.
Ulinzi huu wa asili huiwezesha migunga kuvumilia.