JW subtitle extractor

Utangulizi wa 2 Samweli

Video Other languages Share text Share link Show times

Utangulizi wa 2 Samweli
Katika maandishi ya awali
ya Kiebrania,
Samweli cha Kwanza na cha Pili
vilikuwa kitabu kimoja.
Nabii Gadi na Nathani
ambao walikamilisha kuandika
1 Samweli
waliandika 2 Samweli.
Simulizi hilo linazungumzia
mambo yaliyotendeka katika
kipindi cha miaka 37.
Kuanzia 1077 hadi 1040 K.W.K.
2 Samweli kinaanza
na masimulizi ya
punde tu baada ya
Mfalme Sauli kufa.
Na kwisha kabla tu
ya kifo cha Mfalme Daudi.
Kitabu hicho kinasimulia
maisha ya Daudi kwa unyoofu
na kwa njia ya wazi.
Alivyojitahidi kumtumikia Yehova
kwa moyo wake wote.
Katika sura ya 1,
Daudi anapata habari
zenye kuhuzunisha.
Sauli na Yonathani mwanawe
wamekufa vitani.
Akiwa na huzuni nyingi
Daudi anatunga wimbo
wa maombolezo,
na anauita “Upinde.”
Sehemu inayosalia ya
2 Samweli inaweza
kugawanywa mara mbili.
Sura ya 2 hadi ya 4
inazungumzia Daudi akiwa
mfalme juu ya Yuda.
Na sura ya 5 hadi 24
zinazungumzia Daudi
akiwa Mfalme wa Israeli yote.
Katika sura ya 2,
Daudi anaenda Hebroni
ambapo anatawazwa kuwa
mfalme juu ya Yuda.
Wakati huohuo
Abneri, mkuu wa jeshi la Sauli
anamtawaza Ish-boshethi,
mwana wa Sauli kuwa mfalme
juu ya makabila yale mengine.
Hata hivyo, katika sura ya 3 na ya 4
Abneri na Ish-boshethi wanauawa,
na katika sura inayofuata
watu wanamtawaza Daudi
kuwa mfalme juu ya Israeli yote.
Kisha Daudi anateka
ngome ya Wayebusi ya Sayuni,
na anahamisha mji mkuu kwenda huko
kutoka Hebroni.
Sayuni linakuja kujulikana pia
kama jiji la Daudi.
Katika sura ya 6,
Daudi analileta
sanduku la agano Yerusalemu.
Katika sura ya 7,
Daudi anamwambia Nathani
kwamba angependa
kumjengea Yehova nyumba
au hekalu.
Lakini Mungu anasema
pendeleo hilo litakuwa la
mwana wa wakati ujao wa mfalme.
Hata hivyo, kwa kuwa
Mungu anampenda Daudi
anafanya agano naye
kwa ajili ya Ufalme
utakaodumu miele.
Sura ya 8 na ya 10,
zinazungumzia ushindi wa Daudi
dhidi ya Waamaleki,
Wamoabu,
Wafilisti,
na maadui wengine.
Sura ya 11,
inatusimulia
pindi yenye kuhuzunisha zaidi
katika maisha ya Daudi.
Anafanya uzinzi na Bath-sheba
ambaye ansika ujauzito
kisha Daudi anafanya mume wake,
Uria auawe vitani.
Katika sura ya 12,
kwa mwongozo wa Yehova
Nathani anamkaripia Daudi.
Pia, anasema kwamba
nyumba ya Daudi
itapatwa na msiba.
Na kwamba mtoto aliyetoka
kuzaliwa na Bath-sheba atakufa.
Bath-sheba ambaye
sasa ni mke wa Daudi,
anashika tena ujauzito
na kujifungua mwana
anayeitwa Sulemani.
Katika sura ya 13 hadi ya 18,
misiba iliyotabiriwa dhidi ya
nyumba ya Daudi inaanza.
Absalomu, mwana wa Daudi
anapanga njama ya kunyakua utawala.
Na Daudi analazimika
kukimbia kutoka Yerusalemu.
Katika sura ya 18,
wanaume wa Daudi
wanawashinda wanaume wa Absalomu.
Naye Yoabu anamuua Absalomu.
Je, ulijua?
Samweli 2 kinafunua
unyoofu wa Biblia kwa njia ya pekee.
Hata makosa ya viongozi wa Israeli
yanafunuliwa waziwazi.
Tunaona pia kwamba
watenda-dhambi wanaotubu kikweli
wanaweza kusamehewa
licha ya kwamba
watapatwa na madhara.
Katika sura ya 23,
kwa unyenyekevu Daudi anasema:
“Roho ya Yehova
ilisema kupitia mimi;
Neno lake lilikuwa kwenye ulimi wangu.
Katika sura ya 24,
Daudi anachochewa
kuliandikisha taifa lote.
Tendo hilo baya linamkasirisha Yehova,
naye akawapiga watu
kwa ugonjwa hatari.
Akifuata mwongozo wa Nathani,
Daudi ananunua uwanja
wa kupuria nafaka
wa Arauna Myebusi,
anajenga madhabahu hapo
na kumtolea Mungu dhabihu.
Kwa amri ya Yehova,
ugonjwa wa hatari
uliowakumba Waisraeli unakomeshwa.
Unaposoma 2 Samweli
Ona jinsi manabii wa Mungu
walivyorekodi historia ya Israeli
kwa unyooofu.
Ona jinsi dhambi inavyoweza
kuwa na matokeo mabaya sana.
Na uone ahadi ya Mungu
ya kumpa Daudi ufalme wa kudumu,
ahadi iliyotimizwa na Yesu Kristo,
“Mwana wa Daudi”
na Mfalme wa Ufalme wa Mungu.