JW subtitle extractor

Utangulizi wa Ruthu

Video Other languages Share text Share link Show times

Utangulizi wa kitabu cha Ruthu
Inaaminika kwamba
nabii Samweli ndiye
aliyeandika kitabu hiki.
Kitabu cha Ruthu kilikamilishwa
mwaka wa 1090 K.W.K hivi.
Mambo yanayosimuliwa
yalitokea mapema
katika kipindi cha Waamuzi.
Jina la kitabu hicho
linatokana na mmoja wa
wahusika wakuu,
Ruthu Mmoabu.
Wahusika wengine wakuu ni
Naomi na Boazi.
Katika sura ya kwanza,
ukame unamfanya
mwanamume anayeitwa Elimeleki,
ahamishe familia yake
kutoka Bethlehemu hadi
nchi ya Moabu.
Elimeleki anakufa akiwa Moabu.
Watoto wake Maloni na Kilioni,
wanawaoa wanawake wa Moabu,
Ruthu na Orpa.
Miaka 10 hivi baadaye,
wana hao wawili wanakufa pia.
Naomi
akiwa na huzuni nyingi
anaamua kurudi Bethlehemu.
Anawahimiza binti zake wakwe
warudi kwa familia zao.
Orpa anawarudia watu wake,
hata hivyo, Ruthu
anashikamana na Naomi.
Wajane hao wawili
wanawasili Bethlehemu
baada tu ya
mavuno ya shayiri kuanza.
Katika sura ya 2,
bila kukusudia
Ruthu anaokota masalio
katika shamba la Boazi
ambaye ni mtu wa ukoo
wa mume wa Naomi.
Boazi anatambua sifa
nzuri za Ruthu
na kumwomba aendelee
kuokota masalio katika
shamba lake.
Baadaye Ruthu
anapomwambia Naomi
kwamba aliokota masalio
katika mashamba ya mwanamume
anyeitwa Boazi,
Naomi anasema:
“Mwanamume huyo ni
mtu wetu wa ukoo,
yeye ni kati ya watu
wanaoweza kutukomboa.”
Katika sura ya 3,
Naomi anamwagiza Ruthu
amwombe Boazi awe
mkombozi wao.
Boazi na Ruthu wangezaa
mtoto kwa ajili ya Naomi
ili kuendeleza uzao
wa Elimeleki.
Boazi yuko tayari kuchukua
jukumu hilo
linaloonyesha upendo,
lakini anamwambia Ruthu
kwamba Naomi ana mtu
wa karibu zaidi wa ukoo
ambaye anaweza kuwa
mkombozi wake.
Katika sura ya 4,
Boazi anaenda
kwenye lango la jiji la Bethlehemu
ambapo anakutana na mwamamume
yule mwingine wa ukoo.
Mwanamume huyo anarejelewa
kuwa fulani wa fulani.
Wakiwa mbele ya wazee
kumi wa jiji hilo,
mwanamume huyo
anapotambua majukumu yake,
anakataa kusaidia.
Basi Boazi anakubali
mbele ya wote majukumu ya
kuwa mkombozi.
Boazi akamwoa Ruthu
nao wakapata mwana
ambaye wanawake majirani
walimwita
Obedi.
Je, ulijua?
Boazi anatuwekea
mfano mzuri wa kumtii Yehova.
Alifanya yote aliyoweza
kuwasaidia Naomi na Ruthu
kutimiza sheria ya Mungu
kuhusu ukombozi
bila kutumia njia za mkato.
Kitabu hicho kinamalizia
kwa kusema:
“Obedi akamzaa Yese,
na Yese akamzaa Daudi,”
ambaye alikuja kuwa
mfalme wa Israeli
na mmoja
wa mababu wa Masihi.
Unaposoma kitabu cha Ruthu,
ona jinsi
Yehova anavyobadili majonzi
kuwa shangwe,
jinsi anavyowathawabisha
wale wanompenda
na kumtii,
na jinsi kitabu hiki
kinavyochangia kutuonyesha
historia ya ukoo wa Daudi
ambao ulitokeza Mfalme
wa Ufalme wa Mungu.