JW subtitle extractor

Utangulizi wa 1 Samweli

Video Other languages Share text Share link Show times

Utangulizi wa 1 Samweli
Katika maandishi ya awali
ya Kiebrania,
1 Samweli na 2 Samweli
kilikuwa kitabu kimoja
Inasemekana kwamba
maandishi hayo yaliandikwa
na nabii Samweli,
Gadi,
na Nathani.
Na Samweli ndiye aliyeandika
sura 24 za kwanza.
1 Samweli
kinazungumzia mambo yaliyotendeka
katika miaka 100 hivi
kuanzia 1180
mpaka 1078 K.W.K
wakati ambapo huenda maandishi
hayo yalikamilishwa.
Kitabu hicho kinazungumzia hasa
viongozi wanne wa Israeli,
Kuhani Mkuu Eli,
nabii Samweli,
Mfalme Sauli,
na Daudi.
Katika sura ya 1,
mwanamke tasa anayeitwa Hana,
anamsihi Yehova ampe mwana,
na kuahidi kwamba,
atamtoa kwa ajili ya
utumishi wa Mungu.
Mungu anajibu sala yake.
Mwana wake, Samweli,
anapoachishwa kunyonya,
anampeleka kule Shilo,
na kumkabidhi
kwa Kuhani Mkuu Eli.
Katika sura ya 3,
Yehova anamwambia kijana
Samweli, awasilishe ujumbe
wa hukumu
dhidi ya nyumba ya Eli,
kwa sababu ameshindwa
kuwakemea watoto wake waovu.
Katika sura ya 4,
Wafilisti wanaliteka
sanduku la agano
kutoka katika kambi ya
jeshi la Israeli,
na kuwaua wana wawili wa Eli,
Hofni na Finehasi.
Eli mwenye umri
wa miaka 98
alipopata habari hizo,
alianguka nyuma kutoka
kwenye kiti chake,
na kufa.
Katika sura ya 5 hadi ya 7
Wafilisti wanarudisha sanduku
hilo Israeli
baada ya kuadhibiwa vikali
mara kadhaa,
na Yehova.
Katika sura inayofuata,
Waisraeli wanaonyesha
ukosefu wa imani
kwa kudai wapewe mfalme.
Katika sura ya 9,
Yehova anamwambia Samweli,
amtie mafuta Sauli
wa kabila la Benjamini,
awe kiongozi wa Israeli.
Sura ya 11,
inaonyesha kwamba
Sauli alianza vizuri,
lakini baada ya muda mfupi,
akakosa kutii.
Katika sura ya 13,
kimbelembele kinamfanya
atoe dhabihu ya kuteketezwa.
Katika sura ya 15,
anawashinda Waamaleki,
lakini kwa kutotii
anamwacha hai Mfalme Agagi,
pamoja na ng’ombe
na kondoo walio bora.
Samweli anamwambia,
kutiii ni bora kuliko dhabihu.
Kisha anamwambia Sauli kwamba,
Mungu amemkataa,
asiwe tena Mfalme.
Katika sura ya 16,
Samweli anamtia mafuta Daudi,
mwana wa Yese,
awe mfalme anayefuata.
Katika sura inayofuata,
Daudi akiwa tu na
kombeo na jiwe,
analiua lile jitu Goliathi,
shujaa wa Wafilisti.
Sura ya 18,
inaonyesha jinsi
urafiki wa kudumu,
kati ya Daudi na Yonathani,
mwana wa Sauli,
ulivyoanza.
Sauli alipoona
ujasiri wa Daudi,
alimweka asimamie wanajeshi vitani.
Daudi anafanikiwa sana
katika kampeni za vita
hivi kwamba anapokea
sifa nyingi kuliko Sauli.
Na hilo linamfanya Sauli
aanze kumwonea wivu.
Katika sura ya 19,
Daudi anakimbia ili asiuawe.
Na anaendelea kuwa mkimbizi,
hadi Sauli anapokufa.
Je, ulijua?
1 Samweli
kinatupatia masomo muhimu kuhusu,
imani na utii
Eli na Sauli,
walikosa kumtii Yehova
na wakafa.
Hata hivyo,
Samweli na Daudi,
walimtumika Yehova
kwa uaminifu
tangu utotoni,
na hivyo kufurahia baraka
za Yehova
maisha yao yote.
Katika sura ya 24 na 26,
Daudi anapata nafasi
za kumuua Sauli,
lakini anakataa kumdhuru
mtiwa mafuta wa Yehova.
Katika sura ya 25,
Samweli anakufa,
na taifa lote la Israeli
linaomboleza.
Daudi,
ambaye sasa yuko kwenye
nyika ya Parani,
anawatuma vijana 10,
waende kwa Nabali,
mmiliki wa kondoo
aliyekuwa tajiri,
wamwombe maandalizi yoyote,
anayoweza kuwapa.
Nabali anapokataa kuwasaidia,
kwa dharau,
Daudi anajiandaa
kwenda kulipiza kisasi.
Hata hivyo,
Abigaili, mke wa Nabali,
anachukua maandalizi upesi
na kwenda kukutana na Daudi,
na hivyo kuepusha msiba!
Katika sura ya 31,
1 Samweli,
kinamalizia kwa kuonyesha
kifo cha Sauli
pamoja na watoto
wake watatu
ambao wanazikwa
chini ya mti wa mwesheli,
huko Yabeshi-Gileadi.
Unaposoma 1 Samweli,
ona jinsi,
Eli na Sauli
walivyojiletea aibu.
Ujionee sababu zilizomfanya
Yehova awapende
Samweli na Daudi.
Na uone jinsi Yehova
alivyomjengea Daudi
nyumba ya kudumu,
ambayo hatimaye,
ilimtokeza Masihi,
Mfalme,
wa Ufalme wa Mungu.