JW subtitle extractor

Yehova Husamehe

Video Other languages Share text Share link Show times

Ulikuwa usiku wa mwisho wa Yesu
pamoja na mitume wake
Nyinyi ndio mmeshikamana nami
katika majaribu yangu
Baada ya muda mfupi
Yesu angekamatwa
na wanafunzi wangekabili
hali ngumu sana
nyinyi nyote mtakwazika
kuhusiana nami usiku wa leo
kwa maana imeandikwa:
“Nitampiga mchungaji,
nao kondoo wa kundi watatawanyika.”
Wanafunzi wote wangekimbia
na kumwacha Yesu
Lakini Petro akasema:
“Hata wengine wote
wakikwazika kuhusiana nawe,
mimi sitakwazika kamwe!”
Hongera sana Caleb
Petro alifikiri yeye ni mwenye nguvu
na wala hatawahi
kumhuzunisha Yehova
Petro ninakuambia
Leo “kabla jogoo hajawika,
utanikana mara tatu.”
Ku- ku-ruu!
Hapana, ni ku-ku-ru-ruu!
Ah-ah, huyo si jogoo
Haya basi watoto jambo muhimu
si jinsi jogoo anavyowika
Mimi sitawahi kumhuzunisha Yehova
Mimi pia
Tunajua kwamba hamtaki kumhuzunisha . . .
. . . lakini Yesu alijua kwamba
Petro angeogopa
na unapoogopa . . .
Aiyaa! Jamani mmechelewa!
Chukueni mfuko wenu
ni muda wa kuondoka!
Taratibu!
-Kwaheri baba
-Kwaheri
-Kwaheri mama
-Kwaherini, nawapenda
Hodi
Nimerudi
Watu wako wapi?
Amerudi akiwa na huzuni
Eti eh?
Kuna nini?
Caleb
We’ mzima?
Vipi ikiwa Yehova hataki
kuwa rafiki yangu tena?
Hm!
Yehova anataka kuwa rafiki yako
lakini kama ulifanya jambo baya
anataka utueleze
Sawa
Leo shuleni nilikuwa nje uwanjani
Caleb
Oh! Habari?
Uh, nilikuwa tu niki . . .
Uh . . .
Unaweza kula
Subiri! Caleb hawezi kula
Haya! Tuambie?
Uh . . .
Sikuwa nataka kula
Nilifikiri Biblia inasema huwezi kula?
Uh . . .
Inasema . . .
-Inasemaje?
-Uh . . .
Sina uhakika
Lakini si ulikuja nyumbani kwetu
kuzungumza kuhusu Biblia?
Kwani umesahau?
Uh . . .
Labda huyo alikuwa mtu mwingine
Wapi! Ilikuwa wewe lakini unaogopa
Hello
Siwezi kuzungumza sasa hivi . . .
Ah, kweli ulikuwa na siku ngumu
Je, unakumbuka Petro
aliposema kwamba hatawahi kukwazika?
Baadaye usiku huo, Yesu alikamatwa
Twende!
Petro alimpenda
na alitaka kumsaidia
Lakini kufanya jambo linalofaa
si rahisi nyakati zote
Wewe! Hata wewe
ulikuwa na Yesu Mgalilaya!
Ah, sijui unachosema
Subiri!
Huyu ni mmoja wao!
Simjui mtu huyo!
Wewe!
Wewe ni mfuasi wa Yesu!
Nilikuona katika bustani
pamoja naye, sivyo?
Ninaapa simjui mtu huyo
Petro alijua jambo sahihi la kufanya
Lakini aliogopa
kwa hiyo akakosea
Ni kama tu shuleni
Ndiyo
Petro hakutaka
kurudia kosa hilo tena kamwe
Lakini alijiuliza ikiwa Yesu na Yehova
bado wangekuwa rafiki zake
Baada ya Yesu kufufuliwa
alizungumza na Petro
Simoni, mwana wa Yohana
Je, unanipenda?
Ndiyo
Bwana
unajua ninakupenda
Yesu alimsamehe
Yehova pia alimsamehe
Lakini Petro alipaswa kwanza
kuongea na Yesu
Wewe ukimkasirisha Yehova
unafikiri unapaswa kufanya nini?
Kusali kwa Yehova
Kweli kabisa
Unahitaji kusali uombe msamaha
Na Yesu alimwonyesha Petro
kwamba amesamehewa
kwa kumpa kazi zaidi
Chunga kondoo wangu wadogo
Kwa hiyo Petro alipokosea
kwa nini hakukata tamaa?
Kwa sababu Yehova husamehe
Njooni niwaambie!
Aiyaa!
Lazima niwaeleze kuhusu
siku za kuzaliwa
Utanisaidia?
Bila shaka.